Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku tisa za Simba, Yanga kuonyesha ukubwa wao

NONDO Pict


NI takribani siku tisa zimebaki kutoka leo Novemba 13, 2025 hadi Novemba 22, 2025 kwa vita ya mechi za makundi kwa michuano ya CAF kuanza, ambapo wawakilishi wa Tanzania, Simba, Yanga, Azam Fc na Singida Black Stars zitachuana na wapinzani tofauti waliopangwa nao ili kusaka tiketi za kutinga robo fainali.


Hii ni mara ya kwanza katika historia ya michuano ya CAF kwa Tanzania kuingiza timu nne kwa mpigo, mbili zikiwa Kombe la Shirikisho na nyingine mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika.


Kwa mujibu wa ratiba ya mechi za makundi ya michuano hiyo, Simba na Yanga pamoja na Singida zenyewe zitacheza Jumamosi ya Novemba 22 kwa muda tofauti, huku Azam ikimalizia kazi siku inayofuata kabla ya kusubiri wiki nyingine ya kufungia Novemba kwa mechi za raundi ya pili.

Yanga ndio itakayokata utepe kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar kuvaana na FAR Rabat ya Morocco, kabla ya Simba kufuatia saa 1:00 usiku dhidi ya Petro Atletico ya Angola kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Baada ya mechi hizo za vigogo hao wa Tanzania, saa 4:00 usiku wa siku hiyo ya Jumamosi, Singida ikiwa ugenini itakwaruzana na CR Belouizdad ya Algeria na siku inayofuata kuanzia saa 10:00 jioni itakuwa zamu ya Azam FC kuumana na AS Maniema huko DR Congo.

NO 01

Kisha wiki inayofuata timu hizo zitapishana, Yanga na Simba zenyewe zitaenda ugenini kuumana na JS Kabylie ya Algeria na Stade Malien ya Mali mtawalia, ilihali Azam na Singida zitarudi nyumbani kuzikaribisha Stellenbosch ya Afrika Kusini na Wydad Casablanca ya Morocco ya Stephane Aziz KI.

Hakuna ubishi mechi hizi za makundi ni ngumu, lakini zina maana kubwa kwa wawakilishi wa Tanzania katika msako wa kutaka kucheza robo fainali.

Kuna mijadala mingi kuhusiana na makundi yalivyo kwa Ligi ya Mabingwa na Shirikisho Afrika, baadhi wakiamini Yanga na Singida zimepangwa makundi magumu ya michuano hiyo kulinganisha na Simba na Azam FC.

Kwa mujibu wa takwimu na upangaji wa madaraja kwa klabu kutokana na ushindani kwa misimu mitano, timu za Tanzania zina takwimu bora za kiushindani kuliko klabu  nyingine katika makundi waliyopangwa, huku Yanga ikiangukia kwa Al Ahly ya Misri, FAR Rabat na JS Kabylie.

NO 02

Ukiangalia aina ya timu ilizopangwa nazo ni wazi unaweza kuona ni saizi yao, kwa takwimu ila kinachotia shaka ni kiwango cha timu hiyo ya Jangwani tangu kuanza kwa msimu huu ukilinganisha na Yanga ile iliyocheza fainali ya Kombe la Shirikisho au ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Hapo ndipo hofu ya kupata nafasi ya kusonga mbele kundini inaonekana finyu. Lakini Yanga haipaswi kukata tamaa mapema, soka ni mchezo wa maajabu na wakikaza buti vyema ni wazi watajenga heshima kwa kutoboa mbele ya vigogo waliopangwa nao.

Kwa upande wa Simba hakuna tofauti na kundi la Yanga japo wenyewe wamekuwa na muendelezo mzuri wa kushindana Afrika kwa ngazi ya klabu na hii imewajengea heshima na kuzalisha hofu kwa wapinzani hasa mechi za nyumbani pale Kwa Mkapa.

Simba imepangwa Kundi D na Esperance ya Tunisia, mbali na Petro Atletico na Stade Malien na ukiangalia nafasi yao kuvuka hatua hiyo ipo kwa asilimia kubwa, japo haipaswi kubweteka kwani wapinzani wao wengine sio wa kuchukuliwa poa kabisa hasa Waangola.

NO 03

Ni kweli makundi waliopo ni magumu kutokana na wapinzani wao lakini kikubwa ni hali zao kwa sasa ndani ya kiwanja kutokana na mabadiliko ya walimu na maingizo mapya ya wachezaji kuonekana bado hayajafikia ubora wa wachezaji walioondoka hasa kwa Yanga.

Sababu wao walisajili kwaajili ya kuziba nafasi zilizoachwa na wachezaji wao tegemeo walioondoka ndipo msisitizo wa kukaza buti ili kufanya kweli licha ya mtihani mkubwa walionao.

Huku Simba wakijaribu kuongeza ubora kwenye kikosi chao hivyo wachezaji wao hawapimwi kwa kile kilichofanywa na walioondoka bali kile walichoongeza kwenye timu.

NO 04

Katika mechi za Shirikisho sina deni na timu zilizopo hata kama hazitavuka, kwani  nitachukulia wako kwenye darasa la kujifunza, japo sio kichaka cha kujificha sababu Kombe la Shirikisho limekua na farasi mweusi kila msimu. Hata msimu uliopita tuliwaona Stellenbosch kama Yanga na Simba zilizoibuka ghafla ya kucheza fainali kwa misimu tofauti.

Kwa shirikisho inaanza kuonekana kama michuano saizi yetu kwa klabu zetu na ndiko kuna dalili ya timu mojawapo kutwaa ubingwa siku za usoni baada ya kucheza fainali mara mbili bila mafanikio

Kila la kheri kwa wawakilishi wa Tanzania na ujumbe wangu kwa Simba na Yanga ni nafsi ya kutaka kuonyesha ukubwa walionao.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu zibariki timu zetu CAF.