Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga zishindwe zenyewe CAFCL

CAFCL Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hizo za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, wawakilishi watatu kutoka Tanzania Bara ambao ni Simba, Yanga na Singida Black Stars wameanza kwa matokeo yanayowapa matumaini kuelekea mechi za marudiano.

WAWAKILISHI watano kati ya sita wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa barani Afrika, wameanza kupigania nafasi ya kufuzu hatua ya makundi huku mechi za kwanza zikitoa picha tofauti kwa timu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Katika mechi hizo za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, wawakilishi watatu kutoka Tanzania Bara ambao ni Simba, Yanga na Singida Black Stars wameanza kwa matokeo yanayowapa matumaini kuelekea mechi za marudiano.

Hata hivyo, hali ni tofauti kwa wawakilishi wa Zanzibar, KVZ na KMKM, ambao wote wamepoteza mechi zao za kwanza na sasa watalazimika kufanya kazi kubwa katika marudiano ili kubadili mwelekeo wao katika michuano hiyo.

Azam FC ambaye ni mwakilishi wa sita wa Tanzania, bado hajaingia uwanjani katika hatua hii kwa kuwa itaanzia raundi ya pili, matajiri hao wa Chamazi ambao jana Jumatatu walicheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo, wanamsubiri mshindi kati ya ZED ya Misri na ASAS Djibouti huku ZED ikipata ushindi wa mabao 4-0.

Kwa maana hiyo, wikiendi ilikuwa kama mtihani wa kwanza kwa Tanzania katika safari yake ya kutafuta mafanikio ya michuano hiyo na picha iliyojitokeza ni moja, Tanzania Bara imepata mwanzo wenye matumaini, lakini bado kazi haijaisha.


HISI 03

SIMBA SIO KINYONGE

Miongoni mwa matokeo muhimu kwa Tanzania Bara ni ushindi wa Simba wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Anicent Oura dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi.

Kwa mtazamo wa kwanza, ushindi huo unaonekana kuwa mkubwa kwa sababu umepatikana ugenini katika mazingira ambayo Simba ililazimika kucheza mbele ya mashabiki wengi wa wenyeji.

Kocha wa Simba, Steve Barker amesisitiza kuwa ushindi wa ugenini katika mashindano ya Afrika si jambo la kawaida na kwamba hata ushindi wa bao moja una thamani kubwa.

“Haikuwa rahisi hata kidogo, kuna vitu mna weza kuendelea kujenga taratibu lakini ni muhimu kupata matokeo, ulikuwa ni mpango wetu kushinda na hilo tumelifanikisha kwa bahati mbaya tulikosa baadhi ya wachezaji wetu lakini ambao walipata nafasi kama vile Ketso ameonyesha kuwa na kitu,” alisema.

Simba imeondoka Malawi ikiwa na faida ya bao moja, lakini haijaondoka ikiwa na picha kwamba ilikuwa bora kwenye kila eneo yapo mapungufu ambayo yalijitokeza kwa mchezaji mmojammoja na timu kwa ujumla.

Barker hakuficha hilo na ndio maana alimpon geza kipa wa kikosi hicho, Djibrilla Kassali kwa kufanya kazi muhimu wakati timu ilipomuhitaji zaidi, akisisitiza kuwa kazi ya kipa ni kusimama katika nyakati ambazo timu inahitaji msaada.

Barker sasa ana kazi mbili, kwanza ni kuhakikisha Simba haiingii kwenye mtego wa kuamini kwamba bao moja linatosha kuifanya iwe salama.

Pili ni kuhakikisha timu inakuwa na uwezo wa kudhibiti mchezo mapema ili isijipe presha ambayo inaweza kuwaweka kwenye wakati mgumu.


HISI 04

YANGA HAKUNA NAMNA

Kwa Yanga, safari ya Botswana haikuwa rahisi kama ambavyo sare ya bao 1-1 inaweza kuonyesha. Mabingwa hao wa Tanzania walienda kukutana na Gaborone United wakiwa na matarajio ya kupata matokeo mazuri ugenini, lakini walijikuta wakilazimika kusubiri hadi dakika za mwisho kabisa kupata bao la kusawazisha kupitia Seleman Mwalimu.

Gaborone United ilikuwa karibu kupata ushindi dhidi ya Yanga, hivyo Mwalimu alifunga katika muda wa nyon geza na kuiokoa Yanga isiondoke Botswana mikono mitupu. Matokeo hayo yameipa Yanga nafasi nzuri zaidi kabla ya mchezo wa marudiano, lakini pia yameacha maswali kuhusu uwezo wa timu kutengeneza nafasi. Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi amekiri kuwa timu haikucheza kwa ubora ambao ulitarajiwa, hivyo wana kazi ya kufanya katika mchezo wa marudiano.

“Tuna siku chache za kujiandaa kabla ya mchezo wa marudiano, naamini itakuwa mechi tofauti kabisa, hivyo tunatakiwa kuhakikisha tunaboresha uchezaji wetu hasa katika kutengeneza nafasi ili tunafanya vizuri,” alisema.

Kwa mujibu wa Mngqithi, Yanga ilitawala sehemu kubwa ya mchezo lakini ubora wa eneo la kuchezea uliathiri kiwango cha timu. Zaidi ya hapo, amesisitiza kwamba wachezaji wanapaswa kuwa na ‘njaa ya ukatili’ wanapofika kwenye nafasi za kufunga.


MOMA 02

KISHINDO CHA SINGIDA BS

Kama kuna timu ambayo imeanza kampeni yake ya CAF kwa kishindo, basi ni Singida Black Stars. Timu hiyo imeichapa Al-Ghazal ya Sudan Kusini mabao 7-1 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Huu ni ushindi ambao unaipa Singida faida kubwa sana kabla ya mchezo wa marudiano. Kocha Papy Kimoto na kikosi chake wameweka msingi mkubwa wa kuvuka hatua hii baada ya kupata tofauti ya mabao sita.

Ushindi huo pia unaendelea kuonyesha mabadiliko ambayo Singida imekuwa ikiyapitia katika mashindano ya Afrika.

Msimu uliopita timu hiyo iliandika historia kwa kufika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza na sasa imeingia kwenye kampeni mpya ikiwa na lengo la kwenda mbali zaidi. Kabla ya mchezo huo, Kimoto aliweka wazi kwamba lengo lao la kwanza lilikuwa kuvuka hatua hii.

Kwa ushindi wa mabao 7-1, Singida imejiweka katika nafasi nzuri sana ya kutimiza sehemu hiyo ya kwanza ya mpango.

Singida inahitaji kwenda kwenye mchezo wa pili ikiwa na nidhamu ileile iliyoiwezesha kupata ushindi mkubwa kwenye mchezo wa kwanza.


KMKM Pict

KAZI YA KUPINDUA MEZA

Wakati Tanzania Bara ikipata matokeo mazuri, wawakilishi wawili wa Zanzibar wamejikuta kwenye mazingira tofauti kabisa. KVZ imepoteza bao 1-0 ugenini dhidi ya Asswehly ya Libya katika Kombe la Shirikisho.

Hata hivyo, kwa KVZ bado kuna nafasi. Bao moja si tofauti kubwa ya matokeo ya ukizingatia watakuwa nyumbani katika mchezo wa marudiano.

Kwa KMKM, hali ni ngumu zaidi, timu hiyo imepoteza kwa mabao 3-0 nyumbani dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya. Hii ni tofauti kubwa ambayo si rahisi kuigeuza.

Zaidi ya yote, Al Ahli Tripoli ina uzoefu na ubora wa kutosha huku mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele, akiwa miongoni mwa wafungaji wa mchezo huo.

Kwa KMKM, mchezo wa marudiano unahitaji zaidi ya hamasa. Inahitaji kuingia na mpango wa wazi wa namna ya kupata bao la kwanza mapema bila kupoteza uwiano wa timu. Bao la mapema litakuwa muhimu sana wakati wakijaribu bahati yao.

Likifungwa mapema, linaweza kubadilisha kabisa hali ya kisaikolojia ya mchezo lakini kama Al Ahli Tripoli itapata bao, kazi ya KMKM itakuwa ngumu.