Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba imefeli padogo tu msimu huu

KATIKA muendelezo wa makala yetu ya anguko la Simba katika misimu miwili ya hivi karibuni miongoni mwa sababu kuu ni pamoja na kutokuwa na ubavu wa kushindana sokoni kusajili wachezaji walio katika kiwango bora kwa nyakati husika.

Ni ukweli mchungu lakini unaoponya kwamba Simba imekuwa na utamaduni wa kutumia bajeti ndogo katika usajili jambo linalopekea kukosa wachezaji bora ambao wanakuwa sokoni kwa wakati husika.

Ubabe wa Simba katika misimu minne ile iliyobeba taji la ligi mfululizo kuanzia msimu wa 2017/2018 hadi 2021/2022 ulichagizwa na wachezaji wengi waliokuwa wa bei rahisi na wengi wao walikuwa huru.

Unakumbuka msimu wa 2017/2018 ilizama Azam na kuwachukua kina Aishi Manula, John Bocco na Shomari Kapombe waliokuwa huru na kuchukua mastaa wengine wengi ambao ushindani wao ulikuwa wa kawaida?.

Usajili wa kina Manula na Bocco ulitiki lakini wachezaji wengine kama kina Said Mohamed 'Nduda', Jamal Mwambeleko, Paul Bukaba na Jamal Mnyate ulikuwa wa kawaida.

Hata hivyo Simba ile kulingana na ushindani uliokuwepo kwenye ligi kuwa mdogo kutokana na wapinzani wake wa karibu Yanga na Azam kuyumba basi ilibeba ubingwa na kuonekana bora lakini kiuhalisia haikuwa hivyo.

Msimu uliofuata wa 2018/2019 Simba pia iliingia sokoni na hapa kwa kiasi kikubwa ilifanikiwa kupata watu walioibeba zaidi timu.

Hapa iliwasaini kini Paschal Wawa, Clatous Chama na Meddie Kagere na wengine wachezaji hao licha ya kwamba hawakuwa na thamani kubwa sokoni lakini walifika Simba na kufanya kazi ya maana na kuficha aibu ya uongozi.

Kwa wakati huo Kagere ndiye angalau ungesema alikuwa anawika sokoni kutokana na kufanya vizuri kwenye mashindano ya Sportpesa lakini kwa Wawa haikuwa hivyo kwani ilimpata bure baada ya kuachwa na El Merrekh ya Sudan huku Chama naye akisajiliwa kama mchezaji wa kawaida lakini ubora aliouonyesha kwenye mechi dhidi ya Asante Kotoko katika tamasha la Simba Day ikawafanya mashabiki waanze kumuelewa.

Hata hivyo kwa wakati huo Simba iliionea sana Yanga iliyokuwa 'masikini' kwani kina Kagere na Wawa wote walianza kuongea na Yanga lakini mwisho wa siku Simba ikapindua meza na kuwachukua kiulaini kwa pesa za madafu.
Hivyo Simba ilitisha lakini wachezaji wake wengi iliowasajili walikuwa wa bei rahisi.

Hali ilizidi kuwa hivyo hadi msimu uliofuata wa 2019/2020 kwani Simba ilisajili wachezaji wengine wa viwango vya kawaida.
Msimu huo ndio Simba iliwavuta Francis Kahata, Sharaff Shiboub, Deo Kanda, na wabrazil watatu, Gerson Fraga, Tairon da Silva na Santos da Silva ambao wengi wao walikuwa mizigo tu kwa klabu na baadae wote kuachwa.

Hata hivyo wachezaji wote hao Simba iliwapata wakiwa huru, kiufupi haikutumia pesa nyingi katika usajili huo.
Mambo yalienda hivyo katika msimu uliofuata wa 2020/2021 ukiwa ni msimu wake wa mwisho kutwa kombe na baada ya hapo wapinzani wake Yanga kufanya mabadiliko na kuamua kumwaga noti jambo loinaloitesa Simba hadi sasa.
Katika msimu huo Simba ilisajili pia lundo la wachezaji wakiwemo Benard Morrison, Larry Bwalya, Chiris Mugalu, Charles Ilamfya, Ibrahim Ame, Joash Onyango na David Kameta 'Duchu'.

Onyango, Mugalu na Bwalya ndio walionyesha makeke katika usajili huo lakini wengine bado walionekana kupwaya  ndani ya jezi ya Simba hata hivyo pia wengi wa wachezaji hao walisajiliwa wakiwa huru.

Hapo ndipo Simba ilianza msimu wa 2021/2022 ikiwa na wachezaji wengine wapya kama Jeremia Kisubi, Henock Inonga, Thadeo Lwanga, Sadio Kanoute, Abdulsamad Kassim, Pape Sakho, Peter Banda na Duncan Nyoni, Kibu Denis na Yusuph Mhilu.

Ni wachache waliofanya vizuri kwenye msimu huo lakini ukiangalia hadi sasa waliobaki ndani ya Simba ni Inonga, Kibu, Kanoute, Sakho na Banda na wengine walishindwa kuonyesha sababu ya kuwasajili.
Baada ya hapo kilichofuata msimu huu ni usajili wa kawaida sana ambao haukuwahi kuisaidia tena Simba kwani katika msimu huu ambao Yanga imeshika usukani, Simba ilisajili wachezaji wengin ambao hawajalipa.
Miongoni mwao ni Mohamed Ouattara,  Victor Akpan, Nelson Okwa, Agustine Okrah, Dejan Georgijevic, Habib Kyombo, ambao wote hawajaisaidia timu.

Sababu kuu za Simba kuwa na usajili wa namna hiyo ni kutokuwa na mifumo rasmi ya usajili lakini pia kwa baadhi ya viongozi kutaka kupata chochote kitu kupitia usajili huo.
Kocha Aussems 'Uchebe' kabla ya kondoka Simba aliwahi kusema ili klabu hiyo iendelee kuna watu wanahitaji kuondoka au kuondolewa kwenye ngazi za juu kwani ndio wanaharibu maendeleo ya Simba kwa faida zao binafsi.

Simba inahitaji kuamua kuishi kwa misingi ya soka sasa, kama mfano usajili unaoendelea kwa sasa asilimia kubwa sio mapendekezo ya kocha wala benchi la ufundi bali wachezaji wengi wanachaguliwa na kusajiliwa na viongozi jambo ambalo kwenye mfumo wa soka halipo hivyo.

Katika wakati huo huo, kuna badhi ya viongozi wanadiriki hadi kuliingilia cbenchi la ufundi katika kupanga kikosi mambo ambayo hayapo kisoka.