Siku 1,826 za ndoa ya Bernardo, Ines Tomaz
Muktasari:
- Bernardo ambaye alifunga ndoa na Ines mnano Julai 2023 huko Ureno, amejiunga na Madrid akiwa kama mchezaji huru akitokea Manchester City na alicheza kwa miaka tisa tena kwa mafanikio ma-kubwa akishinda mataji karibia yote ngazi ya klabu.
HUU ni msimu wa kwanza wa Bernardo Silva, 31, katika kikosi cha Real Madrid, ila kwa upande wa mai-sha binafsi huu ni mwaka wa tatu katika ndoa na mkewe Ines Tomaz, 28, ambaye amejipambanua ka-ma mwanamitindo mwenye ndoto kubwa.
Bernardo ambaye alifunga ndoa na Ines mnano Julai 2023 huko Ureno, amejiunga na Madrid akiwa kama mchezaji huru akitokea Manchester City na alicheza kwa miaka tisa tena kwa mafanikio ma-kubwa akishinda mataji karibia yote ngazi ya klabu.
Ines aliwahi kuzungumza kwa furaha kuhusu uhusiano wake na mashabiki wa Man City, akisema ni jambo zuri kuona jinsi mashabiki wanavyompenda, na mara nyingi aliwasikia wakiimba wimbo kwa ajili yake, kitu kilichomfanya ajisikie vizuri.
Kabla ya kusaini Madrid, Bernardo alihusishwa kuhamia Atletico Madrid, Juventus au Barcelona, huku Atletico ikiaminika inaongoza katika mbio za kumsajili lakini mwishowe akatua Santiago Bernabeu akianza msimu mpya chini ya Kocha Jose Mourinho.
Bernardo na Ines walifunga ndoa Julai 1, 2023, katika sherehe kubwa iliyofanyika kwenye eneo la mas-hamba ya mizabibu katika bonde la Douro nchini Ureno. Walichagua eneo hilo ambalo lipo karibu na nyumbani kwao kwa ajili ya siku hiyo muhimu zaidi katika maisha yao.
Takribani mwezi mmoja baadaye, yaani Agosti 2023, walijaliwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kike, Carlota. Mtoto huyo alizaliwa Ureno kabla ya kuhamia Manchester, England pamoja na familia yake akiwa na umri wa takribani mwezi mmoja.
Kwa sasa familia hiyo ikiwa inajiandaa kupokea mtoto wao wa pili, tayari wameanza maisha mapya His-pania, wakiacha maisha waliyoyazoea England na kuanza ukurasa mpya jijini Madrid na ndipo ilipo mas-kani ya Real Madrid ambayo Bernardo anaitumikia kwa sasa.
Katika mahojiano na mtandao wa HELLO!, Bernardo alisema kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza, Car-lota kulibadilisha kabisa mtindo wa maisha yake pamoja na mkewe Ines kwa kiwango kikubwa sana.
“Sasa hivi kila kitu ninachofanya kinalenga kumfurahisha Carlota. Kila tunachofanya tunajaribu kum-shirikisha, mimi na Ines hatuna tena muda wa kukaa peke yetu, hatuna tena muda huo, lakini yeye ni mtoto mzuri sana. Ana tabia nzuri sana,” alisema.
Bernardo na Ines tayari wana mipango ya kupata watoto zaidi, kuwa na familia ya kubwa moja ya ndo-to wanazotaka kuzitimiza katika maisha yao miaka michache ijayo.
“Siku zote tulitaka kuwa na familia kubwa, na hii ni mwanzo tu. Hatutaki kuishia kwenye mtoto wa pili. Sipendi kufikiria sana mambo ya mbali, lakini bila shaka tunakwenda kupata mtoto wa tatu baadaye. Labda wa nne, alisema Bernardo.
Ines na binti yake Carlota walienda Marekani kwa ajili ya kumshuhudia Bernardo akicheza Kombe la Dunia 2026 akiwa na kikosi cha Ureno. Mrembo huyo alikaa katika hoteli iliyoko umbali wa takribani da-kika tano kwa mwendo wa gari kutoka kwenye hoteli ya timu hiyo. “Tunapaswa kukaa hotelini ka-ma timu. Kutakuwa na utaratibu ambapo tutapewa muda maalum wa kuonana na familia zetu. Ni jam-bo gumu kuwa mbali na familia na hasa watoto, lakini hiyo ni sehemu ya kazi na tumeshazoea,” alisema Bernardo kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ambayo ilishirikisha timu 48 kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo, Ureno chini ya nahodha wake, Cristiano Ronaldo alitupwa nje ya michuano hiyo katika hatua ya 16 bora baada ya kufungwa goli 1-0 na Hispania ambao walikuja kuibuka mabingwa ikiwa ni mara ya pili kwa taifa hilo kubeba Kombe la Dunia la FIFA.
Julai Mosi 2026, Bernardo na Ines walihadhimisha miaka mitatu ya ndoa yao wakikumbuka siku hiyo ilivyokuwa na joto kali katika bonde la Douro, kaskazini mwa Ureno. Miaka mitatu ni sawa na siku 1,826, muda ambao wameishi wakitambulika kama mume na mke.
“Harusi iliisha saa nane au saa tisa hivi usiku, kwa hiyo tulifurahia sana,” alisema Bernardo katika ma-hojiano yake marefu na mtandao wa HELLO! ambayo yalichapishwa mnano Juni mwaka huu.
Mbali na kuwa mke wa Bernardo, Ines anatambulika na wengi kama mwanamitindo na mtu mwenye ushawishi katika mitandao ya kijamii. Kitendo cha kumuunga mkono mumewe katika kazi yake ya soka kimefanya mashabiki wengi kupenda kufuatilia maisha yake. Katika ukurasa wake wa Instagram, Ines kila mara huposti picha na video kuhusu mitindo mipya ya mavazi, maisha yake ya kila siku pamoja na matukio makubwa kutoka ndani ya familia yao. Hata hivyo, suala la ni lini na wapi alikutana na Bernardo kwa mara ya kwanza, limesalia kuwa siri yao.