Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Semenyo alivyokabidhi maumivu yake kwa Jordeen Buckley

SHOWBIZ Pict

Muktasari:

  • Akiwa na jeraha la kifundo cha mgumu, ndipo Semenyo aliona ni wakati sahihi kwa yeye kumvisha Jordeen pete ya uchumba, hatua inayoweza kutafsiriwa ameamua kujitoa kwake kwa asilimia 100 bila kujali anapitia hali gani au watapitia nini maishani.

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Ghana anayekipiga Manchester City, Antoine Semenyo amekabidhi furaha na maumivu ya moyo wake kwa Jordeen Buckley, mwanamitindo ambaye alikubali kuwa naye kabla hajawa staa mkubwa katika soka la kulipwa.

Akiwa na jeraha la kifundo cha mgumu, ndipo Semenyo aliona ni wakati sahihi kwa yeye kumvisha Jordeen pete ya uchumba, hatua inayoweza kutafsiriwa ameamua kujitoa kwake kwa asilimia 100 bila kujali anapitia hali gani au watapitia nini maishani.

Uhusiano wa wawili hao ulianza mwaka 2020, wakati huo Semenyo bado akijitafuta katika soka la England ambapo alikuwa akiichezea klabu ya Bristol City ambayo sasa inacheza ligi daraja la pili, EFL Championship ikipambana kupanda Ligi Kuu England (EPL) ambayo ina mashabiki wengi duniani.

SHOW 01

Baada ya takribani miaka mitano ya uhusiano wao, Semenyo na Jordeen walichumbiana hapo Novemba 2025, ikiwa ni muda mfupi baada ya mchezaji huyo kuondoka katika kambi ya timu ya taifa ya Ghana (Black Stars) ambako alishindwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Korea Kusini kutokana na majeraha.

Semenyo ambaye alikuwa nahodha wa Ghana katika mchezo waliopoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Japan, alipata jeraha kwenye kifundo cha mguu wake wa kushoto. Kutokana na jeraha hilo, mshambuliaji huyo aliruhusiwa kuondoka kambini huku timu ikiendelea na maandalizi ya mchezo wake uliofuata.

SHOW 02

Akiwa katika kipindi cha kuuguza jeraha hilo, Semenyo alitumia fursa kumvisha Jordeen pete ya uchumba ikiwa ni ishara wapo tayari kuelekea kufunga ndoa ingawa hadi sasa bado hawajaweka wazi ni lini hasa watachukua uamuzi huo muhimu.

Baadaye Jordeen aliposti picha za tukio hilo katika Insta Story yake akionyesha kufurahia na kujivunia pete yake ya uchumba, huku akieleza ahadi ya kuwa pamoja milele ni jambo lenye kuvutia zaidi kwa wote wawili.

SHOW 03

Kipindi hicho Semenyo alikuwa akikipiga katika klabu ya Bournemouth, pia alihusishwa kuwa katika rada za vigogo wakubwa wa EPL ikiwemo Liverpool na Manchester United, mwishowe Manchester City chini ya Pep Guardiola ndio waliofanikiwa kumsajili mnamo Januari 2026.

Ilikuwa ni habari njema kwa Jordeen kumuona Semenyo akijiunga na Man City, mrembo huyo alisherehekea hatua hiyo kwa kuandika: Ni ukurasa mpya katika maisha yetu. Ninajivunia kila kitu ambacho umefanya kwa bidii.

SHOW 04

Jordeen alirudia tena ujumbe unaofanana na huo akieleza kujivunia jitihada za Semenyo uwanjani baada ya mshambuliaji huyo kufunga goli la ushindi dhidi ya Chelsea katika fainali ya FA Cup mnamo Mei 2026.

"Ninajivunia sana kuwa na wewe mpenzi wangu," aliandika Jordeen katika ukurasa wake wa Instagram ambao una wafuasi zaidi 151,000, ikiwa ni tangu ajiunge na mtandao huo mnano Julai 2024.

Hadi kufikia sasa Semenyo na Jordeen hawana mtoto na hawajatangaza hadharani mipango yoyote ya kuanzisha familia lakini tayari wameonyesha dhamira ya kufanya hivyo muda si mrefu.

SHOW 05

Je, Jordeen Buckley ni nani hasa?, mrembo huyu ni mwanamitindo, mjasiriamali na mshawishi wa mitandao ya kijamii anayeishi jijini London. Alizaliwa Mei 11, 2000 na kukulia England na ni raia wa nchi hiyo.

Mbali na kuwa mchumba wa Antoine Semenyo, Jordeen ni mjasiriamali na mtengeneza maudhui anayefanya vizuri kwa kutumia jina lake mwenyewe. Kazi zake zinapatikana katika mitandao ya Instagram, TikTok na YouTube kwa jina hilo hilo.

SHOW 06
SHOW 06

Kwenye mitandao hiyo kwa kushirikiana na chapa (brand) mbalimbali, Jordeen hutoa maudhui ambayo yanalenga kueneza uwelewa kwa watu kuhusu sekta ya urembo na mitindo, eneo ambalo ana uzoefu nalo wa muda mrefu.

Vilevile yeye ndiye mwanzilishi na mmiliki wa JRose NailBar, biashara ya kutengeneza kucha iliyopo London ambayo imekuwa ikitoa huduma hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Juhudi zake binafsi katika ujasiriamali pamoja na uwezo wake wa kutumia mitandao ya kijamii, vimemfanya Jordeen kuwa mtu anayefahamika zaidi kupitia jina lake, na si kupitia jina la mchumba wake Semenyo kama ilivyo kwa wapenzi wa mastaa wengine wa soka.