Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luz Mendez: Mkufunzi wa mazoezi aliyefunga ndoa na Brahim Diaz

SHOWBIZ Pict

Muktasari:

  • Diaz na Luz walifanya harusi yao siku ya Jumapili, Agosti 2, ingawa hadi sasa bado haijajulikana ni wapi walipoifanya hafla hiyo pamoja na idadi ya wageni waliohudhuria.

WIKIENDI iliyopita, mshambuliaji wa Morocco na Real Madrid, Brahim Diaz alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Luz Mendez ambaye ni mjasiriamali na mtayarishaji wa maudhui kutokea nchini Hispania.

Diaz na Luz walifanya harusi yao siku ya Jumapili, Agosti 2, ingawa hadi sasa bado haijajulikana ni wapi walipoifanya hafla hiyo pamoja na idadi ya wageni waliohudhuria.

Kwa mujibu wa picha ambazo wawili hao wameziposti Instagram, wote wanaonekana wakiwa wamevalia mavazi ya harusi huku wakisherehekea mwanzo wa safari ya maisha ya ndoa.

SHOW 01

Ikumbukwe harusi hiyo ilifanyika siku moja kabla ya sherehe ya kuzaliwa ya Diaz na alisherehekea kutimiza umri wa miaka 27. Staa huyo wa zamani wa Manchester City, alizaliwa Agosti 3, 1999 mjini Malaga, Hispania.

"Nilipata fursa ya kujihisi kama binti wa kifalme nikiwa nimevalia gauni la harusi nililokuwa nikiliota siku zote. Asante Berta kwa kuzifanya ndoto zangu zitimie," aliandika Luz katika Instagram yake.

Diaz na Luz walitangaza kuchumbiana mnamo Mei, ikiwa ni muda mfupi kabla ya mchezaji huyo kujiunga na timu ya taifa ya Morocco kwa ajili ya Kombe la Dunia la 2026, michuano ambayo walikuja kutolewa hatua ya robo fainali na Ufaransa.

SHOW 02

Wakati huo, Luz aliposti Instagram picha ya pete yake ya uchumba akiwa pamoja na Diaz na kuandika kuwa watakuwa pamoja milele.

Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano tangu mwaka 2020, lakini kwa kipindi chote hicho wameweka usiri mkubwa katika maisha yao binafsi wakikwepa presha inayoweza kuletwa kwao na mashabiki, vyombo vya habari na mitandao.

Hata baada ya Diaz kutolewa kwa mkopo wa misimu mitatu kwenda AC Milan na alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A), uhusiano wao uliendelea kuwepo hadi pale aliporeja tena Real Madrid.

SHOW 03

Kwa mara ya kwanza Diaz na Luz kuonekana hadharani pamoja ilikuwa mwaka 2023 katika sherehe ya wachezaji wa Real Madrid, mabingwa wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) mara 36.

Kuelekea mwaka mpya wa 2025, Luz alieleza katika Instagram ni jinsi gani anavyotamani kuendelea kuwa pamoja na Diaz katika maisha yake.

"Naposti picha hii ya mwisho kwa mwaka huu nikiwa na wewe, mtu ambaye nilitumia nawe kila dakika ya mwaka 2024 na ninataka kuishi nawe katika kila sekunde ya mwaka 2025," alisema Luz.

SHOW 04

Je, Luz Mendez ni nani hasa?, mrembo huyu ni mjasiriamali, mwigizaji, mtayarishaji wa maudhui mtandaoni na mkufunzi wa viungo (pilates) aliyebobea, taaluma ambayo ameisomea.

Luz ambaye alizaliwa katika kisiwa cha Tenerife nchini Hispania, mbali na shughuli zake binafsi ni mmoja wa waanzilishi wa Elements Madrid, mradi unaojihusisha na kuandaa matukio yanayohusu afya na michezo ya kifahari.

Katika mitandao ya kijamii, Luz amejikita kutoa maudhui yanayohamasisha mazoezi ya viungo, mtindo mzuri wa maisha, pamoja na safari zake binafsi katika miradi yake mbalimbali.

SHOW 05

Ukurasa wake wa Instagram ambao una wafuasi (followers) zaidi ya 447,000, mara kwa mara huutumia kuposti video na picha za mazoezi, safari zake, mitindo ya mavazi na maisha yake ya kawaida ya kila siku.

Mbali na kazi zake, Luz amekuwa akimuunga mkono Diaz katika hatua mbalimbali za maisha yake ya soka. Ameonekana mara kadhaa akihudhuria mechi za Real Madrid na timu ya taifa ya Morocco.

Vilevile amewavutia mashabiki wengi wa Morocco baada ya kuonyesha kuukubali utamaduni wao, mathalani katika ziara yake nchini huko kipindi cha AFCON 2025, alivaa kaftan, vazi la asili linalotambulika katika utamaduni wa nchi hiyo.

Baada ya Diaz kufunga goli kwa mkwaju wa penalti katika AFCON dhidi ya Mali katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 11, Luz aliandika: Ilikuwa mechi yenye presha kubwa lakini wenye furaha zaidi duniani. Tunakupenda.

Katika michuano hiyo Diaz alimaliza akiwa Mfungaji Bora baada ya kwenda kambani mara tano. Hata hivyo, kitendo cha kukosa penalti katika fainali iliyokumbwa drama dakika za mwisho dhidi ya Senegal, ni tukio lisilosahaulika na mashabiki wengi.

Lakini bado Diaz ameendelea kuwa mchezaji muhimu wa Morocco (Atlas Lions) tangu alipobadili uraia wake wa kimichezo mwaka 2024 akitokea Hispania na amepata makuzi ya soka akicheza timu za taifa za vijana kati ya mwaka 2017 hadi 2021.