Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzanite yaanza na kichapo Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Tanzania, iliyokuwa ikicheza kwa mara ya kwanza fainali za Kombe la Dunia la U-20, iliingia uwanjani ikiwa na matumaini makubwa ya kuonyesha kuwa kufuzu kwake hakukuwa bahati. Hata hivyo, Brazil, moja ya mataifa yenye historia kubwa katika soka la wanawake, ilitumia uzoefu wake kuwadhibiti vijana hao wa Tanzania.

Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 20, Tanzanite Queens imeanza kwa kipigo kwenye kampeni za Kombe la Dunia baada ya kuruhusu mabao 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wa kundi B uliopigwa Uwanja wa Stadion Miejski, Bielsko-Biała nchini Poland.

Tanzania, iliyokuwa ikicheza kwa mara ya kwanza fainali za Kombe la Dunia la U-20, iliingia uwanjani ikiwa na matumaini makubwa ya kuonyesha kuwa kufuzu kwake hakukuwa bahati. Hata hivyo, Brazil, moja ya mataifa yenye historia kubwa katika soka la wanawake, ilitumia uzoefu wake kuwadhibiti vijana hao wa Tanzania.

Brazil ilianza kwa kasi na kupata bao la kuongoza dakika ya 14 kupitia Thaynara, bao lililoonyesha mapema tatizo ambalo Tanzania ilikabiliwa nalo katika kuzuia mashambulizi ya mpinzani wake.

Pamoja na kufungwa bao hilo, Tanzania haikukubali mchezo uende upande mmoja. Kikosi hicho kilianza kujenga mashambulizi na juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 39 baada ya kupata penalti iliyobadilishwa kuwa bao na Winfrida Gerald.

Lilikuwa bao muhimu kwa Tanzania kwa sababu liliifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa imefufua matumaini na kuwa sare ya 1-1.

Kipndi cha pili Brazil iliongeza kasi, ikaanza kutumia nafasi kwa ufanisi zaidi na kuilazimisha Tanzania kutumia muda mwingi katika kujilinda. Ndipo ubora wa Brazil ulipoanza kuonekana zaidi, huku Tanzania ikishindwa kudhibiti kasi na mabadiliko ya mchezo kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Brazil iliendelea kuongeza presha na kufunga mabao mengine matatu, na kufanya matokeo yamalizike 4-1.

Baada ya mechi hiyo Tanzania itashuka tena uwanjani Septemba 8 kumenyana na England kabla ya kumalizia hatua ya makundi dhidi ya Canada Septemba 11.