Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pole Kaseja utaimarika zaidi kiukocha

KASEJA Pict

Muktasari:

  • Ni mapema sana kwenye Ligi halafu timu inachezea mabao sita kiukweli wengi hatukutegemea kuona ikitokea kwa sasa.

UNAJUA kwa timu kama Kagera Sugar kupigwa sita na Geita Gold ni jambo lililotushtua sana hapa kijiweni.

Ni mapema sana kwenye Ligi halafu timu inachezea mabao sita kiukweli wengi hatukutegemea kuona ikitokea kwa sasa.

Halafu wanangu ukiangalia, wale Kagera Sugar walikuwa wametoka kucheza mechi mbili ngumu na hawakupigwa nyingi.

Lakini wakaja kuanguka migoli kibao kwa wachimba madini wa Geita tena wakizidiwa sana. Mpira huooo.

Sasa kimpira kichapo kile cha Kagera Sugar kitamsaidia sana Kocha wake Juma Kaseja kwani kinamlazimisha afanye tathmini ya kina ili kisijirudie tena katika mechi zijazo.

Asingefungwa goli nyingi, inawezekana angejisahau na kuona timu yake ipo na ubora wa kushindana lakini Geita imempa jibu la tofauti.

Maana kabla ya hapo hakufungwa mabao mengi katika mechi moja aliyocheza na Simba na baada ya hapo Singida Black Stars.

Lakini hizo mechi ni dhidi ya timu kubwa ambazo automatikali wachezaji wenyewe wanakaza bila hata kuhamasishwa kwa vile kuna fursa ya kuonekana na wakajiuza.

Kwa hiyo Kaseja hatakiwi kutoka mchezoni maana ndio kwanza darasa linaanza kwa upande wake.