Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juma Kaseja awafungia kazi mabeki

KASEJA Pict

Muktasari:

  • Kagera ambayo imerejea msimu huu Ligi Kuu, katika mechi tatu ilizocheza mfululizo, imeambulia sare moja huku ikipoteza mbili na kuruhusu mabao tisa sawa na wastani wa mabao matatu kila mchezo.

MABAO tisa waliyofungwa Kagera Sugar katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara msimu huu, yamemuibua Kocha Mkuu, Juma Kaseja akikiri kutokuwa na mwanzo mzuri, akiahidi kuisuka upya safu yake ya beki na kuweka makali mapya kwa straika.

Kagera ambayo imerejea msimu huu Ligi Kuu, katika mechi tatu ilizocheza mfululizo, imeambulia sare moja huku ikipoteza mbili na kuruhusu mabao tisa sawa na wastani wa mabao matatu kila mchezo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaseja amekiri kutoanza vyema akitaja kipigo cha mabao 6-2 dhidi ya Geita Gold akieleza si udhaifu wa timu bali ilikuwa kama bahati kwa wapinzani akieleza kusahihisha makosa.

Amesema mabao tisa waliyoruhusu kwenye mechi hizo si matokeo mazuri akibainisha na yapo makosa binafsi kwa beki na mengine ya timu, hivyo benchi la ufundi limeona na litafanyia kazi.

“Mpira ni mchezo wa wazi, matokeo dhidi ya Geita Gold kila mmoja anasema kivyake kama alivyoona, lakini huenda ilikuwa siku nzuri kwao na si kwamba hatukuwa wabovu kiasi hicho, matukio ya mpira hayajirudii.

“Presha kwetu ni kubwa kwa mashabiki, viongozi, benchi la ufundi wachezaji baada ya kutopata ushindi, lakini tunaenda kujisahihisha na kuboresha ili tuweze kuwa bora kwa mechi zinazofuata,” amesema Kaseja.

Nyota huyo wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars ameongeza kuwa anaamini timu hiyo itafanya vizuri kwakuwa bado wanaisuka timu kutengeneza muunganiko akikiri Ligi Kuu kuwa ngumu kwa timu zote.

Kuhusu mchezo ujao ugenini dhidi ya Mashujaa, kipa huyo wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, amesema kucheza nyumbani au ugenini siyo sababu ya kupata ushindi, akieleza kuwa Kagera Sugar ikiwa kwao haijashinda licha ya kucheza michezo miwili Kaitaba.

“Tunaendelea kurekebisha makosa, lakini suala la kucheza nyumbani au ugenini haiwezi kuwa sababu ya kupata matokeo mazuri, tunaamini mchezo na Mashujaa utakuwa mgumu ila lolote linawezekana,” amesema Kaseja.