Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyepesi nyepesi za Dabi... Hii ndo mechi ya maajabu Dabi ya Kariakoo

MAAJABU Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza na Yanga ilipindua meza kwa ushindi wa 2-1 baada ya kutanguliwa kwa bao la mapema la Adam Sabu 'Gerd Muller' kabla ya kuchomoa bao katika dk 87 kupitia Gibson Sembuli na kuongezwa dakika 30 na Sunday Manara 'Computer' akamaliza kazi dk 97 katika fainali hiyo kali ya Ligi ya Taifa. Timu hizo zilikutana Simba ikitokea Poland na Yanga Romania, na Saad Ally wa Simba alizimia kwa kubabuliwa na mpira wa kombora la Sembuli na alipoangukia, ilivumishwa kiliota kichuguu, huku nyota huyo akivumishiwa kufariki hospitalini, japo haikuwa hivyo.

ZIMEPIGWA dabi kibao, nyingine zikiwa na matokeo ya kustaajabisha ikiwamo ile sare ya 4-4 ya jijini Arusha mwaka 1996, sare ya 3-3 kila timu ikifunga mabao yake kipindi kimoja, mbali na zile za vipigo vikubwa, lakini unaambiwa mechi iliyopigwa Agosti 10, 1974 ndio inayotajwa kama ya maajabu.

Mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza na Yanga ilipindua meza kwa ushindi wa 2-1 baada ya kutanguliwa kwa bao la mapema la Adam Sabu 'Gerd Muller' kabla ya kuchomoa bao katika dk 87 kupitia Gibson Sembuli na kuongezwa dakika 30 na Sunday Manara 'Computer' akamaliza kazi dk 97 katika fainali hiyo kali ya Ligi ya Taifa. Timu hizo zilikutana Simba ikitokea Poland na Yanga Romania, na Saad Ally wa Simba alizimia kwa kubabuliwa na mpira wa kombora la Sembuli na alipoangukia, ilivumishwa kiliota kichuguu, huku nyota huyo akivumishiwa kufariki hospitalini, japo haikuwa hivyo.

Lakini Willy Mwaijibe wa Simba na kipa Elias Michael 'Nyoka Mweusi' wa Yanga waligongana na kutolewa nje nafasi zao zikizibwa na Adam Sekulu na kipa Muhidin Fadhil.


MAAJ 01

Ni Amissi Tambwe pekee

LICHA ya kupigwa mechi 113 za Dabi ya Kariakoo tangu mwaka 1965, ni wachezaji wanne tu waliowahi kufunga mara tatu mfululizo dhidi ya wapinzani, huku Amissi Tambwe wa Yanga akiwa mchezaji pekee wa kigeni kufanya hivyo.

Kitwana Manara wa Yanga ndiye aliyekuwa wa kwanza akifunga mara tatu mfululizo kati ya 1968 na 1972, japo katikati ya mechi hizo kuna mchezo Simba iliingia mitini ikikacha kucheza dhidi ya Yanga.

Madaraka Seleman wa Simba alifuata mwaka 1994 akifunga katika mechi za Julai 2, Novemba 2 na 21 mwaka huo, kisha Amissi Tambwe wa Yanga naye akaingia katika orodha akifunga kati ya Sept, 2015 na Oktoba, 2016 huku Shiza Kichuya akiwa wa mwisho akifanya hivyo kati ya Oktoba 1, 2026 na Oktoba 28, 2017.


MAAJ 02

Simba wazee wa kujiweka

INGAWA beki Seleman Sanga wa Yanga ndiye mchezaji wa kwanza kujifunga katika Dabi ya Kariakoo akifanya hivyo Julai 19, 1977 wakati timu yake ikifa 6-0, lakini mabeki wa Simba ndio wanaoongoza kwa kujiweka kwani tangu Dabi za Ligi ya Bara zianze kuchezwa, jamaa wamejiweka mara tatu tofauti.

Lilla Shomary alijifunga katika kipigo cha 2-0 mechi iliyopigwa Septemba 10, 1983, kisha Mustafa Hoza naye akajiweka jijini Arusha wakati watani walipotoka sare ya 4-4 mchezo ukipigwa Novemba 9, 1994 na Kelvin Kijili, wa Simba pia alijiweka tena timu hizo zilipokutana mara ya mwisho Oktoba 19, 2024.


MAAJ 03
MAAJ 03

Hata mikoani kimepigwa sana

NANI aliyekwambia Dabi ya Kariakoo ni kwa ajili ya mashabiki wa soka wa jijini la Dar es Salaam tu?

Kama hujui hata mikoani wameshashuhudia sana tu, Dabi ya Kariakoo za Ligi ya Bara, rekodi zikionyesha, zimeshapigwa dabi 10 tangu mwaka 1974-2010, huku Mwanza na Morogoro zikiongoza.

Mwanza na Moro kila moja zimeshuhudia Dabi tatu, jijini la Mwanza likifungua na kufunga pazia, kwani imeandaa ya 1974, Yanga ikashinda 2-1, kisha 2001 ngoma ikaisha kwa sare na 2010 ikafunga hesabu kwa Yanga pia kushinda 1-0, wakati Moro iliandaa mara mbili 2005 na 2007 na zote Simba ikitakata.

Mikoa mingine iliyoshuhudia dabi ya Kariakoo ni Arusha 1997 na 2005, Mbeya (1997) na Dodoma (1997).


MAAJ 04

Yanga na msoto wa miaka minane

ACHANA na hizi kelele kwamba Simba imeshindwa kupata ushindi katika mechi nne mfululizo zilizopita, kama hujui Yanga iliwahi kuhenyeka na kusota mbele ya Simba kwa miaka minane. Hujakosea. Miaka minane, Yanga ilicheza na Simba bila kuonja ushindi wowote. Ipo hivi, baada ya Bwana Harusi, Idd Moshi 'Mnyamwezi' kuitungua Simba mabao 2-0 Agosti 5, 2000, Yanga ilicheza mechi 15 mfululizo bila kuonja ushindi mbele ya Simba hadi Mkenya, Ben Mwalala alipoikomboa Oktoba 26, 2008.

Mkenya huyo alifunga bao pekee dk 15 lililoiua Simba na kuikomboa Yanga katika unyonge na aibu hiyo iliyobaki rekodi baada msoto wa mechi 15 mfululizo, ikiambulia sare tisa na vipigo sita tofauti.


MAAJ 05

Wametupia huku na kule

PAMOJA na kuwapo kwa orodha ndefu ya wachezaji waliozitumikia timu zote mbili za Simba na Yanga kwa vipindi tofauti, kama ilivyo kwa sasa kwa Clatous Chama, Jonas Mkude na Israel Mwenda, lakini ni nyota watatu tu waliobahatika kufunga huku na kule.

Nyota hao ni Thomas Kipese 'Uncle Tom', Athuman Abdallah 'China' na Said Mwamba 'Kizota' ambao walianza kutupia mabao katika Dabi ya Kariakoo za Ligi ya Bara wakiwa na Yanga, kisha walipohamia Msimbazi, hawakulaza damu, walifunga vile vile, kuonyesha hawakutaka kucheka na mtu.

Hata hivyo, ni Kizota ndiye mkali wao, kwani alifunga mabao manne, yakiwamo matatu akiwa na uzi wa Yanga na moja alipohamia Msimbazi kwa muda kabla ya kurudi Jangwani.