Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyagawa aishangaza Mbeya, ulemavu haujazuia kutafuta riziki kwa kipaji

Muktasari:

  • Msanii huyo ameeleza pia unazi wake wa soka akiitaja Yanga kuwa chaguo lake akiwa na ndoto ya kukutana na Rais wa timu hiyo, Hersi Said akieleza kuwa licha ya changoto zake, timu hiyo humpa furaha ya kipekee.

PAMOJA na kuzaliwa mlemavu wa miguu na mikono, lakini msanii Leonard Nyagawa ameamua kutumia kipaji chake cha kuimba kuendesha maisha katika harakati zake kila siku.

Msanii huyo ameeleza pia unazi wake wa soka akiitaja Yanga kuwa chaguo lake akiwa na ndoto ya kukutana na Rais wa timu hiyo, Hersi Said akieleza kuwa licha ya changoto zake, timu hiyo humpa furaha ya kipekee.

Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti, Nyagawa mkazi wa Mtaa wa Nanyele, Kata ya Nzovwe jijini Mbeya, ameeleza safari yake ya maisha hadi kuwa na familia ya mke na watoto wawili.

Nyagawa aliyezaliwa Iringa katika familia ya watoto 20, kwa sasa makazi yake ni jijini Mbeya akiwa na mkewe Anna na watoto wawili, Suzan na Magdalena.


MAISHA NA KIPAJI

Nyagawa anasema alipomaliza elimu msingi Tanangozi mkoani Iringa 1996, alianza kutumia kipaji cha kuimba muziki akiwa mkali wa bolingo, lakini baadaye aliachana nao.

Anasema 2011 akiwa katika jukwaa alikutana na mwanamke aitwaye Anna Agustino ambaye alivutiwa naye na kumuomba waanze safari pamoja ya maisha, ombi ambalo lilitiki.

Hata hivyo, pamoja na kukubaliwa na mwanamke huyo, Nyagawa alipewa sharti la kuacha kuimba bolingo badala yake ajikite kwenye nyimbo za dini, suala ambalo alikubaliana nalo.

“Kabla sijamuoa mke wangu nilipokutana naye kwe nye sherehe moja akaniambia niache muziki wa bolingo badala yake nijikite na za dini, sikukataa nikafanya hivyo.

“Nashukuru kupitia muziki huo nilipata pesa iliyonisaidia kulipa mahari na mwaka 2012 nikafunga naye ndoa. Hadi sasa tumefanikiwa kupata watoto wawili Suzan na Maagdalena.

“Nashukuru maisha yangu na jamii tunaishi vizuri, nashirikishwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na majukumu mengine, hali ambayo inanipa kujiamini na kunihamasisha kutafuta riziki,”  anasema Nyagawa.

Anaongeza kuwa kwa sasa ni msanii mzuri wa nyimbo za dini, ambapo kutokana na ubora wake jukwaani, amekuwa akipata fursa ya kutumbuiza kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zikiwamo za kitaifa.

Anasema kupitia kipaji hicho imemsaidia kuendesha vyema maisha yake akisaidiana na mkewe ambapo wote hupiga tarumbeta hali ambayo imeonekana kubadili maisha yao.

“Licha ya kutoendelea na masomo ya ngazi za juu, lakini elimu yangu ya darasa la saba imenifanya kung’amua mambo mengi hadi kuwa katika maisha ya kawaida na jamii naelewana nayo vizuri,”  anasema Nyagawa.


AMTAKA BOSI YANGA

Nyagawa mbali na kupenda muziki pia ni shabiki lialia wa Yanga na mnazi mkubwa wa timu hiyo. Vilevile licha ya ulemavu alionao mara kadhaa amekuwa akionekana Uwanja wa Sokoine wakati timu za Mbeya hasa Tanzania Prisons inapocheza mechi ambapo huwa jukwaani kushangilia na wengine.

Hata hivyo, anabainisha kuwa pamoja na kuipenda Yanga, anasikitika kushuka daraja Tanzania Prisons, akiiombea kurejea tena Ligi Kuu. Pia anaeleza kuwa siku akikutana Hersi atampa ujumbe mzito.

“Kwanza nina ujumbe wake mzito Hersi Said, lakini nampongeza kwa kunipa raha Yanga kile anachofanya. Mataji matano mfululizo ya Ligi Kuu ni furaha kubwa. Nilitamani tamasha la Yanga Day ningekuwepo. Napenda timu zote za Mkoa wa Mbeya ila nilisikitika sana kwa matokeo ya kushuka kwa chama langu Tanzania Prisons, sina namna ila naiombea irudi tena Ligi Kuu,” anasema.


ANACHOSEMA MKEWE

Anna Agustino ambaye ni mkewe anasema tangu ameolewa na Nyagawa ameyaona mabadiliko makubwa akieleza amekuwa mtu tofauti kutokana na kujishughulisha kwake.

“Serikali itoe kipaumbele kwa kundi hili, mume wangu anajishughulisha hivyo hata tukipata Sh1 milioni itatusaidia sana kuongeza mtaji,”  anasema.

Anasema kuwa kupitia kuimba na kupiga tarumbeta, kumewabadilishia maisha akieleza kuwa anafurahia jinsi mumewe anavyojishughulisha bila kukata tamaa wala kutumia udhaifu wa ulemavu wake.

“M w en yewe huwa nashangaa namna anavyobuni njia za kutafuta riziki, kwanza ni mshonaji mzuri wa viatu, lakini anaimba sana. Huwezi kumuona anaombaomba, anajitafutia riziki halali,” anasema Anna.


AKATAA OMBAOMBA

Nyagawa anaeleza kuwa kupitia kuimba kwake kumempa heshima akajenga nyumba kwa kusaidiana na mkewe ambaye wanashirikiana pia kupiga tarumbeta.

“Kwa maana hiyo nikaona kuombaomba siwezi badala yake nitumie kipaji changu Mungu alichonipa kutafuta riziki, naimba sana na kupitia nyimbo zangu nimeweza kujenga nyumba, hii ni heshima,” anasema.

Anaeleza kuwa, hana tatizo lolote kwa jamii ikiwamo kunyanyapaliwa kwa kuwa anashirikiana na kila mmoja, na amekuwa akijichanganya na wengi bila kujali rika au hali ya mtu.

“Changamoto kubwa ni wakati wa mvua huwa nashindwa kufanya mzunguko kuna muda mafuriko yanatokea nashindwa kutembea, jamii naishi nayo vizuri na hawaninyanyapai,”  anasema Nyagawa.

Hata hivyo, anawashukuru baadhi ya wadau akiwamo msherehesahi maarufu mkoani Mbeya, Charles Mwakipesile kwa sapoti yake kumfungulia milango ya kiuchumi.

“Hii nyumba ilitokana na fursa ya Mwakipesile aliyeniita kutumbuiza kwenye maonesho ya Nanenane mwaka 2018, kupitia tukio hilo nilipata fedha zilizonisaidia kunyanyua nyumba na kuezeka,”  anasema.

David Pius ambaye ni jirani wa Nyagawa anasema ni mmoja wa wananchi wenye mchango mkubwa katika mtaa wao kutokana na ushiriki wake wa shughuli mbalimbali za kijamii na hatumii nafasi yake kubweteka.

“Kwanza ni mtani wangu kwa sababu yeye ni Yanga, mimi Simba, tukikutana bandaumiza inakuwa shangwe, kiujumla ni mtu fulani hana makuu, anapenda sana michezo,”  anasema Pius.