Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni kweli kipele kimepata mkunaji, lakini si kila wakati

Muktasari:

Ninafanya hivyo kwa sababu tofauti na kamwe wawili hao hawawezi kufanana kwa namna yoyote ile na wale ambao tunao huku uswahilini.

BINAFSI ninawakumbuka watu wawili ambao walikuwa wasemaji wakuu wa sehemu mbili tofauti.

Ninatambua kuwa hata huku uswahilini tunao wasemaji wetu ambao wametokea kuwa maarufu, hasa kwa kauli zao.

Kwa wale waliotimiza vyema wajibu wao, nawapongeza, ila nawakosoa kidogo wale ambao wametumia vibaya nafasi hii wakijitangaza wao, siyo taasisi wanazoziwakilisha.

Nimesema watu wawili, ninaowazungumzia hapa ni Muhammad Saeed al-Sahhaf, Msemaji wa Utawala wa aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein na chama chake cha Kisoshalisti, Ba’ath.

Al- Sahhaf alichomoza na kufahamika zaidi ulimwenguni wakati wa uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003, ambako mtu huyo alikuwa pia Waziri wa Habari.

Wakati ule, Al- Sahhaf ambaye hakujulikana, alitimiza wajibu wake ipasavyo kwa mwajiri, yaani serikali kwa kueleza ukweli ule aliouamini kuwa ulikuwa, ingawa kwa wengine ulionekana uongo.

Aliwatia moyo wananchi wa Iraq kiasi kwamba kipigo kikali cha makombora na ndege za Marekani na maswahiba zake, hasa Uingereza kilionekana kama mchezo wa kuigiza, kwa maana Al- Sahhaf alikiyeyusha kwa maneno na kauli tamu, zenye mvuto.

Mara kadhaa, aliwaeleza wananchi kuwa wanajeshi wa Marekani wameingia kwenye ngome ya Iraq na hawatoki kamwe, kitu ambacho naamini hata yeye hakukiamini.

Yupo pia mtu mwingine, Joaquin Navarro-Valls. Huyo alikuwa msemaji wa makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican ambako alijipatia umaarufu mkubwa hasa wakati ule wa ugonjwa wa Papa Yohani Paulo 11, ambaye kwa sasa ni mtakatifu.

Navarro- Valls, ambaye kitaaluma ni daktari, pia mwandishi wa habari akifahamu hali ya mwajiri wake, kwa maana ya Papa Yohane Paul II, aliwaeleza waumini kuwa hali yake ni shwari, hata kama alijua kwamba alikuwa amedhoofu kwa kiasi kikubwa, hawezi tena kuzungumza au pengine kula na kunywa.

Ni hadi kifo cha kiongozi huyo, Navarro- Valls aliendelea kuwatia moyo waumini wa Kanisa Katoliki, akiwatoa hofu kuhusu maisha yake.

Nimesema tangu awali kwamba hata huku uswahilini kwetu tunao watu kadhaa ambao wamejipatia umaarufu kutokana na kuzimudu vyema kazi zao, zikiwamo za usemaji.

Nielewe vyema kwamba, hapa siwazungumzii waficha habari wale wanaoitwa maofisa mawasiliano wa wizara, idara za serikali.

Hao ni kama alivyowahi kueleza msemaji wa chama tawala, Nape Nnauye akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kwamba maofisa habari wa Serikali ni watu wasiojua vizuri wajibu wao.

Ninakubaliana na Nape, ambaye kitaaluma ni mwanahabari kwamba wasemaji wengi wa idara za Serikali ni kama hawajui nini wajibu wao, wamesahau maana halisi ya habari, ndiyo maana wanaficha habari.

Ninapenda kutumia usemi wa Kiswahili kuwa kipele kimepata mkunaji, ninapowazungumzia wasemaji wa klabu mbalimbali za mpira nchini, zikiwamo za Ligi Kuu.

Kwa bahati nzuri, hawa wako tofauti kabisa na wale wa idara mbalimbali za Serikali ambao kwa jumla ni kama hawajui, hawaoni sababu ya kutoa habari, kiasi kwamba ni warasimu kama walivyo viongozi wengine.

Ninawakumbusha kidogo wakazi wenzangu wa uswahilini jinsi ambavyo wasemaji wa klabu zetu zikiwamo kubwa, Simba na Yanga, wamegeuka wao kuwa habari, ndiyo maana kila jioni hawakosekani kwenye vyombo vya habari ambako wanajinadi wao wenyewe, wala siyo mafanikio ya klabu zao, ambazo wakati mwingine zinafanya vibaya.

Niwakumbushe pia wakati ule Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) lilipoamua kuweka utaratibu wa klabu zetu kuajiri watu mbalimbali wakiwamo wasemaji, makatibu wakuu na wahasibu, kumbe ilikuwa njia ya kuwapa ulaji wengine, ambao ninachelea kusema kuwa hawakustahili.

Tangu kuanza kwa mfumo huo wa kuwa na wasemaji wa klabu, Yanga imekuwa nao, Luis Sendeu, Baraka Kizuguto na sasa Jerry Muro.

Simba ilianza na Clifford Ndimbo, Asha Muhaji, Humphrey Nyasio na sasa Haji Manara.

Wasemaji hao wa klabu hizo mbili kubwa wamekuwa wenye tabia na mazoea ya kutofautiana kwa kiasi kikubwa, ingawa kwa sasa inafaa niwazungumzie kidogo Muro na Manara, ambao wako kibaruani.

Muro na Manara wanafurahisha kwa kiasi chao, ingawa kasoro yao ni kuona hawakosekani kwenye redio hasa zile za FM, ambako ni kama wanaonyeshana ujuzi wa nani msemaji zaidi ya mwingine.

Badala ya kuzisemea Yanga na Simba, wanaonyesha umahiri wa kelele, kejeli na vijembe, jambo ambalo sidhani kama lipo kwenye utaratibu za kazi zao za kila siku.

Naamini, sisi wakazi wa uswahilini, tunawashangaa wasemaji wa klabu hizo mbili, kama ambavyo imekuwa kwa wenzao wa Mtibwa, Thobias Kifaru na Masau Bwire wa timu za kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ruvu kilichoko mkoani Pwani.

Nilidhani kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambalo ndilo mtoto wa Fifa lingewaita na kuwapa angalizo la jinsi ya kutimiza wajibu wao, likiwashauri wauze sura halisi ya klabu zao, si kubadilishana matusi na ubabe.

Sidhani kama sisi wapenzi na mashabiki wa soka huku uswahilini tunapenda kuwasikia kina Muro, Manara, Kifaru, Bwire kila jioni wakiuza sauti zao za kejeli dhidi ya wapinzani wao.

Siamini kama tunahitaji kusikia wasemaji wa klabu zetu wakiwa wababe, wakitishiana wao wenyewe au hata wanahabari kuwa mwenye kuingia katika anga zao, basi ataambulia kipigo!

Sikubaliani hata kidogo na mienendo hiyo ya wasemaji wa klabu zetu, nawashauri wajiangalie upya, watambue klabu hizo zina majukumu mengi kwa umma, zinatakiwa kubadili uendeshaji wake, uwe wa kisasa unaoendana na karne ya 21.

*Ndyesumbilai Florian ni msanifu mwandamizi wa habari za michezo wa Mwananchi