Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndoa za Ronaldo De Lima zilivyopigwa kitu kizito!

DI LIMA Pict

Muktasari:

  • Katika toleo lililopita, tuliangazia ndoa yake ya sasa na mwanamitindo, Celina Locks, 35, ambayo ilifungwa Septemba 2023, ikiwa ni baada ya kuwa pamoja kwa miaka saba.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Inter Milan na Real Madrid kutokea Brazil, Ronaldo De Lima, 49, katika utafutaji wake amefanikiwa kufunga ndoa nne, na tatu kati hizo tayari zimepigwa na kitu kizito, yaani zimevunjika.

Katika toleo lililopita, tuliangazia ndoa yake ya sasa na mwanamitindo, Celina Locks, 35, ambayo ilifungwa Septemba 2023, ikiwa ni baada ya kuwa pamoja kwa miaka saba.

DI 01

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia, kupitia ndoa zake nne na uhusiano na wanawake kadhaa uliovuma sana magazetini, maisha yake ya mapenzi yamekuwa hadharani yakiwa na mafanikio, maumivu na misukosuko.

Kutoka katika ndoa na mwanasoka mwenzake hadi mjasiriamali wa mitindo, kila mmoja wa wake zake aliingia katika maisha ya Ronaldo De Lima kwa wakati tofauti na hata kuondoka kama ifuatavyo.


DI 06

Mwaka 1999, ndipo alifunga ndoa ya kwanza, wakati huo alikuwa katika kilele cha umaarufu akiichezea Inter Milan, akiiongoza timu ya taifa ya Brazil, na akiwa ameshinda tuzo mbili za Mchezaji Bora wa Dunia wa FIFA.

Milene Domingues, 46, hakuwa mtu wa kawaida, bali mwanasoka mwenye kipaji, akijulikana kwa ustadi mkubwa uwanjani na hata kushikilia rekodi ya dunia ya Guinness kwa kupiga danadana zaidi ya 55,000 bila kuangusha mpira.

DI 04

Walimpata mtoto wao wa kwanza, Ronald (2000) aliyezaliwa mjini Milan, Italia, ila siku chache baadaye, Ronaldo alipata majeraha mabaya ya goti yaliyotishia kuiangamiza kabisa kazi yake.

Baadaye Milene alisimulia jinsi alivyoshuhudia tukio hilo akiwa na mtoto mchanga mikononi, akikaa karibu na mama mzazi wa Ronaldo.

"Alikuwa amepata mtoto wake wa kwanza, kitu alichokitamani sana kwa muda mrefu. Kisha ghafla kila kitu kilionekana kuharibika kufuatia majeraha hayo," alisema Milene, mzaliwa wa Sao Paulo, Brazil.

DI 05

Licha ya changamoto za umaarufu na malezi kama familia inayotazamwa na wengi, wawili hao walifanikiwa kulea mtoto wao kwa heshima hata baada ya kuachana mwaka 2003, ikiwa ni miaka minne tangu waoane.

"Unajua hatuwezi kukubaliana kwa kila kitu, lakini heshima ndio hufanya mambo yaende vizuri. Kipaumbele chetu kilikuwa furaha ya mtoto wetu," alieleza Milene baada ya utengano.


DI 03

Daniella Cicarelli

Baada ya hapo, mnamo 2005, Ronaldo alizama katika penzi jipya na mtangazaji wa kituo cha MTV kutokea Brazil, Daniella Cicarelli, 46, ambaye pia ni mwanamitindo mwenye mafanikio.

Wawili hao walifanya harusi ya kifahari katika kasri la Chateau de Chantilly nchini Ufaransa na kuhudhuriwa na watu wengi mashuhuri. Kwa ujumla ndoa yao inatajwa kugharimu zaidi ya Dola 700,000 (wastani wa Sh1.7 bilioni kwa sasa).

Hata hivyo, uhusiano huo ulidumu chini ya mwaka mmoja. Ndoa hiyo ya kusisimua ilivunjika baada ya miezi mitatu tu, huku ikielezwa kuwa Daniella alipata ujauzito ila ukaharibika.

Wakati huo vyombo vya habari viliripoti kuwa migogoro ya mara kwa mara, wivu wa kupitiliza, na madai ya usaliti, ndivyo vilivyoisambaratisha ndoa yao. Daniella alimtuhumu Ronaldo kwa kuchepuka, naye hakukana jambo hilo!

"Nilifanya makosa," alieleza Ronaldo. Uhusiano huo ulimalizika bila mtoto wala kesi ya mgawanyo wa mali, lakini uliishia kwa kujadiliwa sana magazetini. Pia ndoa hii haikusajiliwa rasmi ndio sababu vyanzo vingine vinataja ndoa za Ronaldo ni tatu. 

DI 02

Maria Beatriz Antony (Bia)

Mnamo 2007, Ronaldo akiwa anakipiga AC Milan ukiwa ni msimu wake wa mwisho barani Ulaya kabla ya kurejea kwao Brazil kujiunga na Corinthians, ndipo alikutana na Maria Beatriz Antony (Bia), 41.

Walifunga ndoa mwaka huohuo, na ndoa yao ilidumu hadi 2012 walipoachana wakiwa wamejaliwa kupata watoto wawili wa kike, Maria Sophia (2008) na Maria Alice (2010).

Bia kutokea Brazil pia, ambaye ni mtaalamu wa mahusiano ya umma (PR), alipendelea maisha ya faragha katika ndoa yao, na imekuwa hivyo hata baada ya kuachana. 

Mwaka 2008, Ronaldo alihusishwa na kashfa kubwa ya kutoka na 'wanawake wa barabarani' watatu mjini Rio de Janeiro. Tukio hilo lilivuma sana Brazil. Bia aliondoka nyumbani usiku huo, na Ronaldo baadaye katika mahojiano alikiri makosa.

"Nilifanya kosa kubwa sana, na ilinigharimu karibu kila kitu," alieleza Ronaldo, mshindi wa Kombe la Dunia mara mbili (1994 & 2002).

Licha ya hayo, waliendelea kuishi pamoja kwa muda kabla ya kuachana rasmi. Hata hivyo, Ronaldo ameendelea kuwa karibu na mabinti zake na mara nyingi huonekana nao kwenye hafla mbalimbali.

Kwa ujumla Ronaldo ana watoto wanne - mwingine ni Alexander (2005) aliyezaliwa baada ya uhusiano wake wa muda mfupi na mhudumu wa mgahawa, Michele Umezu ambaye hakufunga naye ndoa. 

Na sasa gwiji huyo aliyekipiga pia FC Barcelona na AC Milan, anaendelea kuishikilia ndoa yake na Celina ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya vipodozi na bidhaa za urembo kwa ajili ya mwanamke.