Real Madrid haijakata tamaa kwa Olise
Muktasari:
- Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Real Madrid imekuwa ikiujadili kila mara mkataba wa sasa wa nyota huyo kuangalia namna inavyoweza kuingia na kuuvunja kwa kutumia fedha nyingi, ikizingatiwa kwamba ndiye mchezaji aliyepo juu kabisa katika orodha ya mastaa wanaotakiwa na Kocha Jose Mourinho.
REAL Madrid inaendelea kumfuatilia winga Michael Olise, lakini Bayern Munich haina nia ya hata kuzungumzia uwezekano wa kumuuza na badala yake inafanya kazi ya kumfunga kimkatata mchezaji huyo wa kimataifa wa Mfaransa.
Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Real Madrid imekuwa ikiujadili kila mara mkataba wa sasa wa nyota huyo kuangalia namna inavyoweza kuingia na kuuvunja kwa kutumia fedha nyingi, ikizingatiwa kwamba ndiye mchezaji aliyepo juu kabisa katika orodha ya mastaa wanaotakiwa na Kocha Jose Mourinho.
Olise aliitingisha Madrid wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi lililopita ambapo ilifikia hatua ya kutangaza kwamba nyota wa kiwango cha dunia alikuwa mlangoni akikaribia kuingi kwenye kikosi hicho, lakini dili likafa ghafla baada ya Bayern Munich kutishia kuifikisha timu hiyo kwenye Mahakama ya Masuala ya Michezo (CAS), kwa kuendelea kumshawishi mwenye mkataba.
Hata hivyo, watu wa karibu na mchezaji huyo walikuwa wameshaanza kumwandalia makazi jijini Madrid iwapo angesaini kuichezea Real Madrid.
Mkataba wa sasa wa Olise unaotarajiwa kumalizika Juni 30, 2029 unamshuhudia akikusanya Pauni 259,000 kwa wiki kutoka Bayern Munich akiwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa kibosi kikosini hapo.
Alejandro Balde
WAKALA wa beki wa kushoto wa Barcelona, Alejandro Balde, amezijulisha Aston Villa, Liverpool na Man Utd masharti ya uhamisho wa mchezaji huyo Januari, mwakani. Bei ya Dola 45 milioni imewekwa, lakini Barca inaweza kuzingatia ofa za mkopo, hasa ikijumuisha kipengele cha lazima cha kumnunua kwa masharti.
Jamie Gittens
ORODHA ya wachezaji wanaolengwa kusajiliwa na Roma katika dirisha dogo la Januari mwakani inaongozwa na winga wa Chelsea, Jamie Gittens, ambaye klabu hiyo ilifanya jaribio la kumsajili katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, ambalo hata hivyo halikufanikiwa. Dello Sport inadai Gittens anaweza kusukuma mpango wa kuondoka London.
Zion Suzuki
KIPA wa kimataifa wa Japan na Aston Villa, Zion Suzuki, amekuwa akifuatiliwa na Liverpool kama mchezaji anayeweza kuchukua nafasi ya Alisson Becker anayeweza kuondoka Anfield mwakani. Arsenal na Manchester City pia zinaendelea kumfuatilia Mjapani huyo, ambaye pia yupo kwenye rada za Real Madrid na PSG.
Levi Colwill
BEKI wa kati wa Chelsea, Levi Colwill, yupo kwenye rada za Barcelona, ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anadaiwa kuwa na nia ya kuhamia Camp Nou. Hata hivyo, Chelsea imeendelea kuwa na kigugumizi kumuachia mchezaji huyo katika dirisha lijalo la usajili mwakani.
Antonio Nusa
KIUNGO wa Arsenal, Martin Odegaard anadaiwa kufanya kazi ya kumshawishi mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Norway, winga wa RB Leipzig, Antonio Nusa, kujiunga naye Emirates. Kwa mujibu wa Daily Briefing, Nusa anaelezwa kuvutiwa zaidi kutua ama Liverpool au Manchester United.
Ebrima Tunkara
ASTON Villa inajaribu kumshawishi kiungo mwenye kipaji kikubwa na umri wa miaka 16, Ebrima Tunkara, ili aondoke Barcelona. Hata hivyo, Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, amedhamiria kutompoteza, ambapo anakusudia kuushawishi uongozi umpe mkataba mpya mchezaji huyo.
Endrick
KOCHA Jose Mourinho yupo tayari kumruhusu mshambuliaji Endrick kuondoka Real Madrid Januari mwakani. Arsenal inataka kumsajili Mbrazili huyo moja kwa moja, huku AC Milan na Manchester United zikiangalia uwezekano wa kumsajili kwa mkopo. Kulingana na Fichajes, Endrick amechoshwa na benchi.
Lisandro Martínez
BEKI wa kati wa kimataifa wa Argentina na Manchester United, Lisandro Martínez, anahitajika na Atletico Madrid pamoja na Barcelona, lakini timu hizo za Hispania zitakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka klabu tatu za Italia ambazo ni Como, Inter Milan na Roma, katika kusaka saini yake.
Aladji Bamba
NEWCASTLE United inadaiwa haitamruhusu kiungo Aladji Bamba kuondoka Januari, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, aliyesajiliwa katika dirisha la majira ya kiangazi lililopita kuendelea kupata dakika chache za kucheza. Bamba ni miongoni mwa wachezaji wanaofuatiliwa sana kwa sasa England.