Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MZEE MPILI: Kauli, mikwara na maisha ya shabiki aliyekuwa nembo ya Yanga SC

MPILI Pict

Muktasari:

  • Huyo alikuwa Haji Omari Ramadhani Mpili, maarufu kama Mzee Mpili, mwanachama na shabiki mkongwe wa Yanga aliyefariki dunia Septemba 27, 2026 akiwa anapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.

ALIKUWA mzee kutoka Ikwiriri, Rufiji, lakini jina lake lilifika mbali zaidi ya mipaka ya eneo aliloishi. Alikuwa si mchezaji, si kocha wala kiongozi wa klabu, lakini kwa miaka kadhaa sauti yake ilikuwa miongoni mwa zilizotengeneza burudani na hamasa katika soka la Tanzania.

Huyo alikuwa Haji Omari Ramadhani Mpili, maarufu kama Mzee Mpili, mwanachama na shabiki mkongwe wa Yanga aliyefariki dunia Septemba 27, 2026 akiwa anapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.

Kifo chake kilifunga ukurasa wa maisha ya shabiki ambaye alijenga umaarufu wake kwa jambo moja kubwa; kuipenda Yanga kwa sauti yake mwenyewe.

Lakini zaidi ya ushabiki, Mzee Mpili alikuwa mhusika wa aina yake katika tamaduni ya soka la Tanzania. Alikuwa na kauli, misimamo, mikwara na ucheshi uliomfanya hata wale waliokuwa upande wa pili wa ushindani wa Simba na Yanga kumtambua.


MPIL 01

ALIVYOLINDA JINA LA YANGA

Miongoni mwa mambo yaliyomtofautisha Mzee Mpili na mashabiki wengine ni namna alivyolichukulia jina la utani “Utopolo”. Hakukubaliana nalo.

Aliona matumizi ya jina hilo kwa Yanga kama dhihaka kwa klabu ambayo kwake ilikuwa na historia, heshima na hadhi yake. Kilichomkasirisha zaidi ni kuona hata baadhi ya mashabiki wa Yanga wakianza kulitumia jina hilo wenyewe.

Mzee Mpili pia alijenga msimamo kuhusu namna klabu yake ilivyopaswa kuitwa. Hakupenda matumizi ya jina la dhihaka “Utopolo” kwa Yanga, akiona kuwa jina hilo halikuwakilisha heshima aliyoiamini klabu hiyo inastahili.

Kwa mtazamo wake, Yanga ilikuwa klabu kubwa yenye historia na haikupaswa kuendeshwa kwa kile alichokiona kuwa “masiala masiala”.

Msimamo huo uliifanya baadhi ya kauli zake kuwa sehemu ya mijadala ya mashabiki, hasa katika kipindi ambacho mijadala ya mitandaoni kuhusu Simba na Yanga ilikuwa ikipamba moto.


MPIL 02

SISI TUNA WATU

Kauli yake ya “Sisi tuna watu” ilipata umaarufu mkubwa katika kipindi ambacho Yanga ilikuwa katika ushindani mkali na Simba. Katika mahojiano ya wakati huo, Mzee Mpili alijitambulisha kama shabiki aliyekuwa na imani kubwa na timu yake.

Mzee Mpili ameondoka akiwa ameacha kumbukumbu ambayo haipimwi kwa idadi ya mechi alizoangalia wala miaka aliyokaa uwanjani, bali kwa namna alivyoweza kufanya sauti ya shabiki mmoja kusikika katika soka la taifa.

“Sisi tuna watu”, “Hatuchezi, hatuchezi” na msimamo wake kuhusu heshima ya Yanga vilimfanya kuwa sura inayotambulika katika utamaduni wa ushabiki wa soka Tanzania.

Kwa mashabiki waliomfahamu, Mzee Mpili hakuwa tu mtu wa kauli kali; alikuwa sehemu ya burudani, hamasa na ushindani ulioufanya mchezo wa soka kuwa zaidi ya dakika 90 uwanjani.

Na alipofika mwisho wa safari yake, watu waliomzunguka walionyesha jambo lile alilolirudia kwa miaka: “Sisi tuna watu.”

Agosti 25, 2021, Yanga ilizindua jezi zake za msimu wa 2021/22 zilizokuwa na ubunifu uliotumia taswira ya watu wengi, ukiambatana na msemo wa Mzee Mpili, “Sisi tuna watu.”

“Msemo wa Mpili watumika kwenye jezi Yanga. Hapo ndipo kauli ya shabiki mmoja wa Ikwiriri ilipogeuka kuwa sehemu ya utambulisho wa klabu kwa msimu huo.

Mzee Mpili mwenyewe alikwenda hatua nyingine kwa kuanzisha chapa iliyotumia jina hilo, akisema Julai 2021 alikuwa akiuza fulana na bidhaa nyingine zenye kauli hiyo.


MPIL 03

HATUCHEZI

Kama “Sisi tuna watu” ilikuwa kauli yake ya kujiamini, “Hatuchezi, hatuchezi, hatuchezi!” ilikuwa sura nyingine ya Mzee Mpili.

Kauli hiyo ilimpa umaarufu mkubwa katika mijadala iliyohusu Yanga na hasa nyakati ambazo aliamini klabu yake haikutendewa kwa namna aliyodhani inastahili.

Kumbukumbu za mwaka 2021 zinaonyesha kauli hiyo ilizunguka sana miongoni mwa mashabiki katika kipindi cha mijadala iliyohusu mechi na uamuzi wa Yanga kutocheza katika mazingira fulani.


MPIL 04

ARDHINI NA ANGANI

Kabla ya baadhi ya mechi kubwa, hasa Dabi ya Kariakoo, Mzee Mpili alijenga utamaduni wa kutoa kauli za kujiamini kupita kawaida.

Miongoni mwa kauli zilizohusishwa naye ni kwamba mambo ya mechi yalikuwa yamekwisha “ardhini na angani.” Kauli hizo ziliwafanya baadhi ya mashabiki wa timu pinzani kumhusisha na imani za kishirikina.

Lakini, katika taswira ya Mzee Mpili, lugha hiyo ilikuwa sehemu ya ucheshi, kujiamini na kutengeneza presha kabla ya mchezo.

Wakati wa mazishi yake, mwanawe Mohamed Haji alieleza kuwa baba yake hakuwa mganga, bali alikuwa mtu aliyekuwa akitumia ujasiri, utani na kujiamini kuongeza ladha katika ushabiki wa soka.

Kwa maana hiyo, “ardhini na angani” ilikuwa sehemu ya lugha yake ya ushabiki, si ushahidi wa taaluma ya uganga.