Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtego mpya wa mafundi wa mipira iliyokufa EPL 2026/27

MTEGO Pict

Muktasari:

  • Soka la kisasa limejikita katika kutafuta faida ndogondogo, huku kila timu ya Ligi Kuu England ikitafuta namna ya kupata ubora zaidi ya wapinzani wake. Kwa sasa, nyingi zimeanza kupitia mifumo ya mipira iliyokufa.

LONDON, ENGLAND: MSIMU mpya wa Ligi Kuu England umewadia. Makocha wanaendelea kuboresha vikosi. Hata hivyo huenda ukawa umeanza huku kila timu ikijiweka sawa katika namna kuicheza na kuidhibiti mipira iliyokufa kwa kuwa itakuwa muhimu sana tena katika msimu wa 2026/27.

Soka la kisasa limejikita katika kutafuta faida ndogondogo, huku kila timu ya Ligi Kuu England ikitafuta namna ya kupata ubora zaidi ya wapinzani wake. Kwa sasa, nyingi zimeanza kupitia mifumo ya mipira iliyokufa.

Zaidi ya nusu ya timu za ligi hiyo sasa zina makocha maalumu wa mipira iliyokufa, huku ambazo hazina zikijihatarisha kubaki nyuma.

Ili kubaini wachezaji wanaofanya vizuri zaidi katika mipira iliyokufa kuna mambo kadhaa yaliyojitokeza msimu uliopita yatakayokuwa ya kuzingatiwa zaidi kitakwimu.


MUHIMU KULIKO WAKATI WOWOTE

Austin MacPhee, mmoja wa makocha wanaoheshimika zaidi katika mipira iliyokufa alihama Aston Villa na kujiunga na Chelsea msimu huu.

Namna uhamisho wake ulivyoelezwa inaonyesha umuhimu unaoongezeka wa eneo hilo la mchezo, ambapo BBC Sport iliripoti kwamba kocha huyo raia wa Scotland mwenye umri wa miaka 46 alijiunga na Chelsea kwa ada isiyowekwa wazi iliyotokana na kifungu cha kuvunja mkataba wake alipokuwa akiwindwa pia na timu nyingine za Ligi Kuu England na Saudi Pro League.

Takwimu zinaonyesha kwamba makocha wa mipira iliyokufa wanaweza kuwa na athari kubwa kama ilivyo kwa usajili wa wachezaji. Katika msimu wa 2025/26, asilimia 27.4 ya mabao yote yalitokana na mipira iliyokufa bila kuhusisha penalti, ikiwa ni kiwango cha pili kwa juu katika historia ya misimu 34 ya mashindano hayo. Msimu uliotangulia kiwango hicho kilikuwa asilimia 20.6.

Mabao yaliyotokana na mipira ya kona pia yalifikia kiwango cha juu yakichangia asilimia 18 ya mabao yote kutoka asilimia 12.1 msimu uliotangulia. Huenda isiwe mwenendo unaopendwa zaidi, lakini ushahidi uko wazi; mapinduzi ya mipira iliyokufa yamefika na yanaonekana.

Kujua ni wachezaji gani wanapiga mipira iliyokufa na ni nani wanaolengwa zaidi ndani ya boksi haijawahi kuwa muhimu zaidi kwa makocha.


TIMU BORA KATIKA MIPIRA ILIYOKUFA

Kwa kuhusisha kona, mipira ya adhabu isiyo ya moja kwa moja, mipira ya adhabu ya moja kwa moja na ya kurusha kutoka pembeni, huku penalti tukizuondoa mabingwa Arsenal waliongoza katika mipira iliyokufa msimu wa 2025/26.

The Gunners walifunga mabao 25 kutokana na mipira iliyokufa bila penalti, huku wakiruhusu manane pekee kwa njia hiyo, hivyo kuwa na tofauti chanya ya mabao 17. Kwa kushangaza, Tottenham Hotspur licha ya kumaliza nafasi moja tu juu ya eneo la kushuka daraja ilikuwa timu ya pili bora katika mipira iliyokufa msimu uliopita, ikiwa na tofauti chanya ya mabao 10.

Kocha wao wa mipira iliyokufa, Andreas Georgson, alijiunga na klabu hiyo pamoja na Thomas Frank, lakini amebaki Spurs licha ya mabadiliko mbalimbali ya makocha yaliyofanyika. Unaweza kuona kwamba Georgson ndiye sababu kubwa iliyowafanya Spurs wasiwe timu ya Championship kwa sasa. Coventry City ndiyo timu iliyofanya vizuri zaidi katika mipira iliyokufa kwenye Championship msimu uliopita.

Walifunga mabao 29 bila penalti na kuruhusu 13, hivyo kuwa na tofauti chanya ya mabao 16 ambayo ingeifanya iwe ya pili katika Ligi Kuu England msimu uliopita. Ni wazi kwamba hawataweza kurudia takwimu hizo, lakini ni nguvu yao muhimu na wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa zaidi katika eneo hilo miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja.

Bournemouth, Crystal Palace na Liverpool, kila moja ikiwa imeruhusu mabao 20 kutokana na mipira iliyokufa bila penalti, ndizo zilizoruhusu mabao mengi zaidi katika njia hiyo msimu uliopita. Crystal Palace ilikuwa na tofauti hasi ya mabao tisa, ikiwa mbaya zaidi katika ligi.

Jambo la kuvutia ni kwamba kocha Andoni Iraola na kikosi chake cha makocha wa mipira iliyokufa wametoka Bournemouth kwenda Liverpool, jambo linaloashiria kwamba matatizo ya The Reds katika eneo hilo huenda yasitatuliwe haraka.


ONGEZEKO KONA ZINAZOINGIA NDANI

Kulikuwa na kona 2,643 zilizopigwa zikiingia ndani msimu uliopita, ikilinganishwa na 541 zilizopigwa zikitoka nje. Hii ina maana kwamba timu nyingi zilipendelea kutumia wachezaji wanaopiga kwa mguu wa kushoto kutoka upande wa kulia na wanaopiga kwa mguu wa kulia kutoka upande wa kushoto.

Mchezaji anayetarajiwa kupiga kona kutoka upande wa kulia wa Manchester United anaweza kuwa Bryan Mbeumo au Luke Shaw, ambao wote wanatumia mguu wa kushoto. James Garner wa Everton, ambaye anatumia mguu wa kulia, alipiga kona nyingi zaidi katika Ligi Kuu England msimu uliopita. Hata hivyo, kati ya kona zake 110, ni 10 tu alizopiga kutoka upande wa kulia.

Mchezaji mwenzake anayetumia mguu wa kushoto, Kiernan Dewsbury-Hall, ndiye aliyekuwa akipiga kona kutoka upande wa kulia, huku kona zake zote 43 msimu uliopita zikitoka upande huo. Kwa kuwa timu zinaonekana kuthamini zaidi kona zinazoingia ndani, wachezaji wapya waliosajiliwa wanaweza kuwa na athari kubwa kwa wachezaji waliopo.

MTEG 04

SZOBOSZLAI NI LAZIMA KUWA NAYE?

Staa wa Liverpool, Dominik Szoboszlai ni mwingine anayestahili kufuatiliwa, ambapo raia huyo wa Hungary mara nyingi alipiga kona kutoka pande zote mbili za uwanja msimu uliopita. Alishirikiana majukumu ya kona za upande wa kushoto na Cody Gakpo, na kulia na Mohamed Salah.

Kwa kuwa Salah ameondoka na Gakpo anahusishwa na uhamisho kwenda Spurs, matarajio ya kawaida ni kwamba idadi ya kona za Szoboszlai itaongezeka zaidi. Hata hivyo, ujio wa kocha Iraola na kikosi chake cha makocha wa mipira iliyokufa unafanya suala hilo kuwa tata.

Bournemouth ya Iraola ilitumia kona zinazoingia ndani mara nyingi zaidi kuliko timu nyingine yoyote katika ligi hiyo msimu uliopita, kwa asilimia 96.4, ikiwa mbele kidogo ya Arsenal.

Kwa sasa Szoboszlai anaonekana kama mchezaji anayetarajiwa zaidi kupiga kona kutoka pande zote mbili Liverpool. Ni vyema ikaeleweka kwamba Liverpool haina wachezaji wengi wenye mguu wa kushoto wenye ubora baada ya kuondoka kwa Salah, hivyo huenda machaguo yakawa machache.

Lakini, zingatia kwamba kuendelea kwa mfumo uliotumiwa na Iraola na makocha wake unaweza kuwa na athari halisi kwa takwimu za Szoboszlai.

Eneo ambalo Szoboszlai yuko salama dhidi ya kubadilishwa ni mipira ya adhabu. Msimu uliopita ingawa mashuti ya mipira ya adhabu ya moja kwa moja yalipungua kukiwa na 251 pekee ikilinganishwa na 621 msimu wa 2003/04, Szoboszlai alifanya kila awezalo.

Alipiga mipira 14 ya adhabu ya moja kwa moja msimu uliopita, idadi kubwa zaidi ya mchezaji yeyote. Muhimu zaidi, alitumia nafasi hizo vizuri akifunga mara nne.

Ni David Beckham 2000/01 na Laurent Robert 2001/02 pekee wote wakiwa na mabao matano waliowahi kufanya vizuri zaidi katika msimu mmoja wa ligi hiyo.

Szoboszlai ni mchezaji muhimu sana kwa Liverpool na anaongoza timu katika maeneo mengi. Kuna hata uwezekano wa kupiga baadhi ya penalti msimu huu kutokana na changamoto za uimara wa kimwili wa Alekander Isak.


MTEG 01

GUIMARAES ANATISHIA THAMANI YA RICE?

Uhusiano wa mchezaji wa kati na uzalishaji katika mipira iliyokufa ni jambo ambalo Szoboszlai anahusiana na Declan Rice wa Arsenal.

Rice aliwaongoza wachezaji wote wa Arsenal msimu uliopita katika kona, akiwa na 95; mipira ya adhabu isiyo ya moja kwa moja 130; mipira ya adhabu iliyotokana na krosi 45; mipira ya adhabu ya moja kwa moja, mitano; na kurusha mipira ndani ya eneo la penalti mara 24.

Lakini, hata Rice hawezi kupingana na taratibu kali za upigaji kona zinazotumiwa na kocha wa Arsenal wa mipira iliyokufa, Nicolas Jover.

Alipiga kona 87 kutoka upande wa kushoto, lakini ni nane tu alizopiga kutoka upande wa kulia. Kona za upande wa kulia badala yake zilikwenda kwa Bukayo Saka aliyepiga 65, na Noni Madueke 38. Hakuna hata mmoja kati yao aliyepiga kona kutoka upande wa kushoto.

MTEG 03

Je, usajili wa Bruno Guimaraes unaweza kuwa na athari kwa takwimu za Rice? Arsenal ilifunga rekodi ya mabao 19 kutokana na kona msimu uliopita, hivyo haina sababu ya kubadilisha mfumo wake. Hata hivyo, Mbrazili huyo ana uwezo wake katika mipira iliyokufa.

Miongoni mwa wachezaji saba waliopiga angalau kona 20 msimu uliopita kwa Arsenal na Newcastle United, mipira ya Guimaraes iliishia kwenye shuti mara nyingi zaidi ikiwa ni kila baada ya kona 1.9. Jambo la muhimu zaidi ni kwamba pia alifunga penalti zake zote mbili alizopiga kwa Newcastle 2025/26.

Saka, aliyefunga penalti moja kati ya moja aliyopiga na Viktor Gyokeres aliyefunga tatu kati ya tatu, walishughulikia penalti za Arsenal msimu uliopita. Lakini, kutokana na uwezekano wa dakika za Saka kugombania na Gyokeres wakigawana muda wa kucheza na Kai Havertz, Arsenal inaweza kuhitaji mchezaji wa tatu wa kupiga penalti. Hapo ndipo mfumo huo pia unapoweza kuzingatia wachezaji wapya waliosajiliwa.


MTEG 05

THIAGO VIPI?

Mchezaji ambaye ana uhakika kwamba hatapoteza jukumu la kupiga penalti ni mshambuliaji wa Brentford, Igor Thiago, ambapo Mbrazili huyo alijipatia umaarufu msimu uliopita baada ya kufunga mabao 22 katika Ligi Kuu, akiwa wa pili nyuma ya Haaland aliyefunga 27.

Kutokana na kiwango hicho, alipata nafasi katika kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia mbele ya Joao Pedro. Hata hivyo, mchezaji huyo wa Chelsea alimzidi Thiago kwa mabao yasiyohusisha penalti, 15 dhidi ya 14.

Lakini ni wazi kwamba sehemu kubwa ya ubora wake inatokana na penalti ambazo siyo rahisi kutabirika. Alipiga penalti tisa msimu uliopita na kufunga nane. Cole Palmer wa Chelsea na Bruno Fernandes ndio wachezaji wengine pekee waliopiga penalti zaidi ya tano. Katika historia ya Ligi Kuu England kumekuwa na matukio manane tu ambapo mchezaji alipiga penalti zaidi ya tisa katika msimu mmoja.

Kwa sasa, Erling Haaland, Fernandes, Palmer na Pascal Grob wanatarajiwa kupiga penalti nyingi zaidi kuliko Thiago katika mechi 10 za kwanza.

Hata hivyo, Thiago bado anaonekana kuwa bora miongoni mwa washambuliaji akiwa na uhakika mkubwa wa kucheza dakika 90 kila mchezo bila kubadilishwa, na anatarajiwa kupata pointi nyingi zaidi kuliko Isak katika mechi 10 za kwanza.


MASTAA WANAONUFAIKA NA MIPIRA ILIYOKUFA

Baada ya kuzungumzia wapigaji wa mipira iliyokufa, sasa tuangalie kwa haraka mastaa wataoweza kunufaika zaidi na mipira hiyo, ambapo Pascal Struijk ambaye amejiunga na Brighton akitokea Leeds msimu huu ndiye aliyegusa kwanza mipira mingi zaidi ya kona iliyovuka ndani ya boksi msimu uliopita, mara 19.

Hata hivyo, alishindwa kufunga katika mashuti yake yote 16 yaliyotokana na mazingira hayo, huku Gabriel Magalhaes wa Arsenal alikuwa chini kidogo akigusa kwanza mipira 13 ya kona iliyovuka ndani ya boksi, iliyozalisha mashuti manane na bao moja.

Lakini ni nahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk alijitokeza zaidi katika eneo hili akifunga mabao manne, idadi kubwa zaidi katika ligi baada ya kugusa kwanza mipira ya kona iliyovuka ndani ya boksi. Kwa kuzingatia takwimu za Opta inaonekana kwamba makocha wamekuwa wakipanga wachezaji kwa kuzingatia mabao yanayotarajiwa kutokana na mipira iliyokufa, bila kuhusisha penalti kama walivyofanya msimu uliopita.

Kadri mipira iliyokufa inavyoendelea kuchangia sehemu kubwa zaidi ya mabao ya Ligi Kuu England, kuelewa nani anayepiga mipira hiyo na nani anayenufaika nayo kunazidi kuwa muhimu sawa na kufuatilia mabao na pasi za mwisho.