Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MKALI WENU: Nilimtambulisha mke wangu kwa bosi akamchukua

KAMERA Pict


WASANII wakongwe wa Bongo fleva,Ferooz,Juma Nature na Solo Thang walikuwa mbele ya muda kuimba wimbo wa Boss, ambao unaendelea kuwa halisi kwenye maisha ya watu, ambao wamepigwa na matukio ya mahusiano.


Wakati wimbo huo unaachiwa miaka 22 iliyopita tangu Agosti 13, 2004, mchekeshaji maarufu nchini Miraji Supakila 'Mkali Wenu' ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 24, alikuwa na miaka miwili, ila kwa sasa wimbo wa Boss umebeba maisha halisi kwake.


Nyuma ya Kamera wiki hii, limepiga stori za hapa na pale na Mkali Wenu, hakutaka kuficha kujiona ndiye mchekeshaji namba moja Tanzania anayeongoza kwa kupigwa matukio ya usaliti na kuachwa.

"Ukitaja wasanii wanaoongoza kwa kuachwa nadhani ni mimi, ujue wanawake wakituona katika mitandao ya kijamii, akija kwenye maisha yako halisi ya kuamka naye kila siku, anaanza kukuona wewe ni mtu wa kawaida sana," anasema Mkali Wenu na kuongeza;

"Kuna wengine wanakuja wakiwa na malengo kwamba nikimuomba Sh.300,000 inapatikana kirahisi, wakati mwingine Sh.100,000 hata mimi nakuwa naitafuta kwa tochi, sasa ukiombwa mara ya kwanza hauna, mara ya pili huna anakuona mbabaifu."

Ana matukio mengi yaliyosalia kumbukumbu na maumivu moyoni mwake, lakini Nyuma ya Kamera anasimulia mawili yaliyoondoa imani ya upendo wa kweli kuuamini kutoka kwa mwanamke.

KAME 01

"Kuna mwanamke nilimpenda akiwa katika hali ya ugonjwa, ambapo alikimbiwa hadi na marafiki zake, baada ya kuumwa sana, nilitumia pesa zangu na muda kumuuguza hadi akapona, nyama nyama zikaanza kurudi kwenye mwili wake, amebarikiwa shepu," anasema na kuongeza;

"Nilienda kwa wazazi wake kutoa posa, tuliishi miaka miwili pamoja, sasa DM zilipoanza kujaa wanaume wenye pesa kila siku wakimsifu kwa uzuri, mimi aliyekuwa ameniahidi ni mwanaume wake wa maisha wa kufa na kuzikana, niliyemvumilia kwenye shida wakati kila mtu kamkimbia, akaanza kuniona kama kinyago, akaniacha na kwenda kwa hawa anaowaona wa maana kwake."

KAME 02

Tukio lingine ni la aliyekuwa mke wake aliyemuoa kwa ndoa, kilichotokea anaeleza alimtambulisha kwa bosi wake kazini, ambaye baadaye ndiye aliyemnyang'anya mwanamke huyo.

"Baada ya kumtambulisha bosi akawa anakuja nyumbani kwangu, anamuachia pesa na kumpa misaada ya hapa na pale, siku ya siku mke wangu akaanza kusema nataka talaka, nikamwambia shida ni nini, maana sioni kitu ambacho kinataka kututenganisha," anasema na kuongeza;

"Ilichukua muda mrefu kutoelewana, akasema anahitaji kwenda kupumzika nyumbani kwao, siku nikaenda ofisini bila kumtaarifu bosi, nikamkuta amekaa kwenye ofisi ya mtendaji mkuu, nikamuuliza unatafuta nini kwenye ofisi za watu, akanijibu mimi ni mke wa bosi wako ondoka.

KAME 03

"Sikukubali nikampigia bosi simu, imekuaje mke wangu ambaye ulikuwa unamsaidia na unanishauri tukiwa tumekosana, kumbe umemchukua wewe, akanijibu ndiyo kijana tafuta pesa acha kulialia, iliniumiza sana, hiyo ni sababu ya kutoamini katika mapenzi ya kweli.

"Nilichokifanya niliachana na kazi, nikatafuta sehemu nyingine ambayo ilikuwa na amani na moyo wangu, kitu kinachoniponza nikimpenda mtu nampenda kutoka moyoni, nakuwa sina mambo mengi ya kandokando, nadhani hicho ndicho wanachokitumia kama udhaifu wa kunipiga matukio kila wakati, hayo ni machache kati ya mengi."

KAME 04

Anasema mwanamke anayetamani kuwepo kwenye maisha yake, awe yule ambaye amebeba picha ya maisha ya mtandaoni, ajue kutofautisha kazi na maisha halisi, jambo ambalo wanawake wengi hawana, badala yake wamejaa tamaa.

"Mwingine anakuja kwenye maisha yako ili ajulikane na kupata koneksheni ya kupata wanaume wa ndoto zao, ndiyo maana inakuwa ngumu kumjua anayekuja kwenye maisha kama ni mtu sahihi au la." anasema mchekeshaji huyo pia ni bondia.