Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MICHAEL CARRICK; Rekodi safi uwanjani, mkwanja mrefu benki

ATM Pict

Muktasari:

  • Juzi Jumamosi usiku, miamba hii ya Old Trafford iliichapa Chelsea bao 1-0 ugenini na kuendeleza rekodi za ushindi kwa Kocha huyo ambaye ni nyota wa zamani wa kikosi hicho.

MANCHESTER, ENGLAND: WACHEZAJI wa Manchester United huwaambii kitu kwa Michael Carrick. Mashabiki wanasubiri tu wakubwa waamue kumpa timu, kwani amekuwa mkombozi wao na sasa wanatembea vifua mbele kutokana na timu kupata matokeo mazuri.

Juzi Jumamosi usiku, miamba hii ya Old Trafford iliichapa Chelsea bao 1-0 ugenini na kuendeleza rekodi za ushindi kwa Kocha huyo ambaye ni nyota wa zamani wa kikosi hicho.

Baada ya Ruben Amorim kuchemka, Man United ilimwamini na kumkabidi timu na sasa inakamata nafasi ya tatu hali iliyorejesha matumaini ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kibarua cha Carrick United ni cha muda mrefu, lakini hilo halimzuii kuingiza mkwanja wa kutosha huku pia akiendelea kuingiza nje ya kazi hiyo kutokana na mikataba ta udhamini aliyoingia wakati anacheza soka na sasa akiwa kocha.

AT 05

ANAPIGAJE PESA

Kwa sasa, Carrick anapata mkate wake wa kila siku kutokana na ajira yake ya muda katika kikosi hicho.

Licha ya kutotolewa kwa taarifa rasmi, lakini vyanzo vya ndani vinadai anakunja Pauni 60,000 kwa wiki ikiwa ni ongezeko la Pauni 20,000 kutoka katika mshahara wake aliokuwa anaupokea akiwa na Middlesbrough FC, alikokuwa analipwa Pauni 40,000.

Alikusanya mpunga wa kutosha pia akiwa kama mchezaji wa zamani katika kikosi cha Manchester United na mshahara wake uliwahi ni zaidi ya Pauni 120,000 kwa wiki katika kipindi chake cha mwisho.

Akiwa mchezaji pia alikuwa akipata takribani Pauni 1 milioni kwa mwaka kutokana na mikataba ya udhamini wa Kampuni ya Nike.

Kocha huyu pia amewekeza hisa katika kampuni mbalimbali na anafanya biashara ya kukodisha majengo.

Kijumla anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 16 milioni, uliotokana na mjumuisho wa mali zake kwa sasa.

AT 04

MIJENGO

Anamiliki nyumba inayokadiriwa kuwa na thamani inayofikia Pauni 6.2 milioni iliyopo maeneo ya Prestbury, Cheshire huko Manchester.

Pia ana mjengo mwingine maeneo ya Macclesfield.

Mbali ya nyumba hizo, staa huyu pia anamiliki nyumba nyingine mbalimbali zaidi ya nne ambazo amezikodisha.

Nyumba yake iliyopo, Cheshire ndani yake ina Gym binafsi, bustani kubwa na Sehemu ya kupumzikia.

AT 02

NDINGA

Range Rover – Pauni 90,000

Audi Q7 – Pauni 70,000

BMW 5 Series – Pauni 60,000


MSAADA KWA JAMII

Kupitia Michael Carrick Foundation, amekuwa akisaidia vijana katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, michezo na kuendeleza vipaji kwa kutoa vifaa vya michezo na katika elimu taasisi yake imekuwa ikijenga shule katika nchi kadhaa za Afrika.

Kwa kiasi kikubwa taasisi yake imejikita zaidi katika kusaidia vijana hasa watokao maeneo ya Kaskazini mwa England.

AT 03

FAMILIA, MAISHA BINAFSI

Michael Carrick yupo katika ndoa na mke wake Lisa Roughead tangu mwaka 2007 na wana watoto wawili, wa kiume, Louise na wa kike, Jacey.

Kwa asilimia kubwa Carrick sio mtu wa starehe na hupendelea sana kuwa nje ya mitandao ama kuzungumziwa. Pia watu wake wa karibu wanaeleza kuwa ni mtu mpole sana.