Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgosi anavyomtumia Elizabeth kama silaha

ELIZA Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mkabaji alijiunga na Simba Queens iliyokuwa na viungo kama Ester Mayala, Odama Amarachi, Mabinty Camara, Brice Zanga lakini licha ya ubora wa viungo hao Mkuki ameendelea kupewa nafasi kutokana na kile anachokifanya.

MIONGONI mwa makinda walioonyesha kiwango bora kwenye Ligi Kuu ya Wanawake msimu uliopita ni Elizabeth Joseph Mkuki (18) anayekipiga Simba Queens huu ukiwa msimu wake wa pili akitokea Alliance Girls ya Mwanza ambako alikuwa nahodha wa timu hiyo.

Kiungo huyo mkabaji alijiunga na Simba Queens iliyokuwa na viungo kama Ester Mayala, Odama Amarachi, Mabinty Camara, Brice Zanga lakini licha ya ubora wa viungo hao Mkuki ameendelea kupewa nafasi kutokana na kile anachokifanya.

Kwa macho ya kawaida unaweza kumuona mchezaji wa kawaida lakini ni silaha ya siri ya kocha Mussa Hassan ‘Mgosi’ anayoitumia hususani kwenye mechi kubwa zenye presha na ushindani wa kutafuta pointi tatu muhimu dhidi ya wapinzani wagumu kama JKT Queens na Yanga Princess.


ELI 01

VS JKT QUEENS (FAINALI NGAO)

Dhidi ya JKT Queens kwenye fainali iliyopigwa Oktoba 03,2026 kwenye Uwanja wa KMC Complex wanajeshi walijaribu mbinu ya kutumia mipira ya juu na kasi ya mashambulizi kupitia kwa Bahati Steven na Fatuma Muhibu.

Kwenye mechi hiyo Mkuki alisimama kama skrini mbele ya safu ya ulinzi. Alipora mipira 14 iliyokuwa ikitoka kwenye miguu ya viungo wa JKT Queens, Elizabeth John na Joyce Lema na kukata pasi 11 zilizokuwa zikielekezwa kwa washambuliaji wa wapinzani.

Katika mchezo huo, zaidi ya 70% ya mashambulizi ya JKT Queens yaliyopitia katikati yaliishia kwenye miguu yake, hali iliyowafanya JKT Queens watoke nje ya mchezo na kucheza kwa nidhamu mbovu hadi beki wa timu hiyo, Ester Maseke kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 59.


ELI 02

MUUAJI WA KIMYA KIMYA

Dhidi ya JKT Queens, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-1, Mei 23, 2026 wekundu hao wakiwa ugenini Uwanja wa Mej Gen Isamuhyo na nyota huyo alikuwa injini ya kurejesha mpira kwa haraka pale Simba walipopoteza.

Katika bao la kwanza la Simba Queens, Corazon alipoweka mpira wa adhabu kwa haraka, Elizabeth alipokea mpira na kuutuliza kwa umakini kabla ya kupiga krosi  iliyozua taharuki kwenye eneo la hatari la JKT Queens, na kuzaa mpira uliomkuta Aisha Mnunka na kufunga.

Elizabeth alionyesha uwezo wa kipekee kwa kupokea mpira na kuingia mwenyewe kwenye boksi la JKT Queens na kupiga shuti kali lililookolewa na golikipa Najat Abbas na kuwa kona. Kijumla alipora mipira 12 na kukata pasi tisa za hatari za JKT Queens.


ELI 04

DHIDI YA YANGA

Kwenye mechi ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga Princess ndiye mchezaji aliyeongoza kwa muchezewa rafu nyingi. Ndiye mchezaji aliyepora mipira mingi zaidi katikati ya uwanja akifanya hivyo mara 11. Aliziba mianya nane ya pasi za Yanga Princess zilizokuwa zikielekezwa mbele.

Asilimia 84 ya pasi nyingi zilikuwa za kuanzisha mashambulizi kwenda kwa Vivian Corazone na Senaf Demise.

Kwenye mechi hiyo Mkuki akikuwa na kazi tatu kwanza kuvunja mfumo wa Yanga katikati. Wananchi walipoanza mchezo kwa presha, kiungo huyo alicheza mbele ya mabeki wa kati kama ukuta. Alikata pasi 8 za Yanga na kuwalazimisha wacheze mipira mirefu ya juu na mabeki wa Simba waliiokoa kwa urahisi.

ELI 05

Kumlazimu nahodha wa Yanga kupewa kadi nyekundu. Shinikizo kubwa la Mkuki na ushirikiano wake na Mary Siyame katikati ya uwanja liliwafanya viungo wa Yanga, Ritticia Nabbosa na Joan Nabirye kupoteza utulivu. Hali hii ilimfanya nahodha na kiungo mchezeshaji wa Yanga, Nabbosa kufanya faulo za mara kwa mara na kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kisha kadi Nyekundu dakika ya 37, jambo lililoimaliza kabisa Yanga Princess.

Kumpa Uhuru Senaf Demisse na Vivian Corazone. Kwa sababu Mkuki alibeba kazi yote ya kulinda na kupora mipira (aliyoirejesha mara 11), viungo wenzake  Corazone na Demisse walipata nafasi na utulivu wa kwenda mbele.

Matokeo yake, Corazone alifunga bao la kwanza na Senaf Demisse akafunga bao la pili kwa shuti la mbali kwenye ushindi wa mabao 3-0.


ELI 03

MBINU ZA MGOSI

Kocha Mussa Hassan Mgosi anamtumia Mkuki kama silaha ya siri kwa sababu ya kuharibu kasi ya mpinzani (Tempo Control): Pindi mpinzani anapopata mpira na kuanza kukimbia, Mkuki ndiye mchezaji wa kwanza kufanya presha  na kumnyang’anya mpira au kulazimisha apige pasi ya nyuma.

Baada ya mabeki wa Simba Queens kuokoa mipira ya juu, Mkuki ndiye anayehakikisha mipira hiyo yote ya pili inakusanywa na Simba Queens ili kuendelea kumiliki mchezo.

Kwa kuangalia takwimu hizo Mkuki anaonekana kuwa zaidi ya kiungo anayelinda eneo lake.

Ni mchezaji anayefanya kazi ambayo wakati mwingine haionekani kwenye vichwa vya habari, lakini ipo kwenye namna Simba Queens inavyoweza kudhibiti wapinzani wake.