Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya miaka 10 ya uhusiano wa Rodri, Laura

SHOWBIZ Pict

Muktasari:

  • Rodri, nahodha wa timu ya taifa ya Hispania, hatumii mitandao ya kijamii, hivyo hivyo na kwa mpenzi wake, Laura, kitu ambacho si cha kwa kawaida kwa wake na wapenzi wa mastaa wa soka (WAGs).

LICHA ya umaarufu na mafanikio makubwa katika soka, bado Rodrigo Hernandez maarufu kama Rodri, amechagua kuishi maisha ya tofauti pamoja na mpenzi wake wa muda mrefu, Laura Iglesias ambaye walikutana wakiwa masomoni.

Rodri, nahodha wa timu ya taifa ya Hispania, hatumii mitandao ya kijamii, hivyo hivyo na kwa mpenzi wake, Laura, kitu ambacho si cha kwa kawaida kwa wake na wapenzi wa mastaa wa soka (WAGs).

Hata hivyo, bado kuna mengi ya kuzungumza kuhusu uhusiano wa Rodri na Laura hata kama hawatumii mitandao ambayo imekuwa sehemu ya mastaa wengi duniani kuonyesha mapenzi yao, familia na mafanikio.

SHOWB 01

Rodri ambaye msimu huu amejiunga na FC Barcelona akitokea Manchester City ambapo alicheza kwa mafanikio makubwa kwa misimu saba, kwa miaka mingi amekuwa akipata sapoti kutoka kwa Laura.

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza wakati wakisoma Chuo Kikuu cha Jaume I (UJI) kilichopo Castellon, mashariki mwa Hispania. Rodri alikuwa akisomea usimamizi wa biashara, huku Laura akisomea udaktari.

SHOWB 02

“Kwangu mimi kusoma chuo ilikuwa ni kipindi bora zaidi cha maisha yangu. Kutumia muda mwingi na vijana wenzangu, kusoma na wakati mwingine kutoka nje, lilikuwa jambo zuri zaidi... Kilikuwa kipindi kizuri,” alisema Rodri mwaka 2022 na kuendelea:

"Kuhusu kukutana na Laura, ni jambo la kuchekesha kwa sababu nilikutana naye kwenye makazi ya wanafunzi (hostel) na wakati huo ndipo tu naye alikuwa ameanza kusomea udaktari."

Kadiri Rodri alivyoanza kupata mafanikio katika soka la kulipwa, Laura aliendelea kuwa mmoja wa watu waliomuunga mkono. Rodri aliwahi kusema kuwa Laura ambaye alikuwa akisoma kwa bidii, alimsaidia kupunguza presha aliyokuwa akikabiliana nayo uwanjani kila wiki.

SHOWB 03

“Msichana aliyekuwa akisoma kwa bidii masomo ya udaktari, ndiye aliyenisaidia sana kuondoa presha niliyokuwa nikikabiliana nayo kila wikendi kwa kucheza ligi. Ilikuwa presha kuanza kuwa mchezaji muhimu katika kikosi na kuanza kuichezea timu ya taifa ya Hispania... Alinisaidia sana," alisema.

Rodri alisema alivvyokutana na Laura, mwanzoni mrembo huyo alishangaa sana kumuona akiishi hostel wakati tayari alikuwa mchezaji anayefamika na mtu mwenye uwezo wa kuishi katika nyumba binafsi.

“Alikuwa kama, ‘huyu jamaa anafanya nini hapa?’ Hivyo nilimfahamu Laura wakati nilipokuwa kwenye timu ya Villarreal ya chini ya miaka 21 (U21), ni kipindi ambacho tayari nilikuwa katika njia ya kuelekea soka la kulipwa," alisema Rodri.

SHOWB 04

Alieleza kuwa mazingira hayo yalikuwa na wanafunzi wengi, hivyo Laura alijaribu kulinda zaidi maisha yao binafsi, na ukizingatia pia alikuwa mtu mwenye aibu.

"Yeye alikuwa mwenye aibu kidogo kwa sababu hakutaka watu wamzungumzie. Unajua tu mambo ya chuo yanavyokuwa, tulikuwa kama wanafunzi 400 hivi katika eneo moja,” alisema.

Baada ya Rodri kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2024 kufuatia kufanya vizuri akiwa Man City chini ya kocha Pep Guardiola, alimshukuru Laura na kufichua kuwa siku hiyo walikuwa wakitimiza miaka minane tangu walipokutana.

“Kwanza kabisa, ningependa kumshukuru mtu muhimu zaidi katika dunia yangu, naye ni mpenzi wangu Laura. Leo ni miaka minane tangu tulipokutana, ni kumbukumbu ya siku yetu. Bila wewe, safari hii isingekuwa kama ilivyo,” alisema Rodri.

SHOWB 05

Kauli ya Rodri inaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza walikutana mwaka 2016, kitu ambacho ni sahihi kabisa kwa mujibu wa maelezo yake ya awali kwani mwaka huo bado alikuwa akiichezea Villarreal B ingawa mwaka huo huo alipanda timu ya wakubwa.

Laura ambaye kwa sasa bado anaendelea na chuo akisomea kuwa daktari bingwa wa upasuaji wa binadamu, si mtu wa kuonekani mara kwa mara kwenye mechi za Rodri kutokana na ubize wake, lakini pia kwa ajili ya mtindo wa maisha aliyouchagua.

Kipindi Rodri akiwa Man City aliwahi kueleza kuwa Laura huwa anajirekodi akishangilia akiwa nyumbani, kisha yeye hutazama video hizo akiwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

“Wakati ninapofunga goli, huwa natumiwa video na Laura akishangilia goli hilo akiwa nyumbani, na huwa naitazama nikiwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo,” alisema Rodri.

Mwaka huu ambao wanahadhimisha miaka 10 ya uhusiano wao, ndio mwaka ambao Rodri akiwa nahodha wa Hispania alibeba Kombe la Dunia la Fifa 2026 huko Marekani, na pia alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa michuano hiyo. Laura naye alikuwepo uwanjani na walisherehekea pamoja mafanikio hayo ya juu zaidi katika soka.