Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi anavyoumba namba zake MLS

MESSI Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa utaratibu wa MLS, uwanja utakaotumiwa kwa ajili ya mchezo huo bado haujajulikana, kwani sheria za ligi hiyo zinasema fainali itaandaliwa na timu iliyokuwa na ufaulu mzuri zaidi wakati wa msimu wa kawaida au timu zingine zinazoshiriki hatua ya mtoano.

MIAMI, MAREKANI: LIGI Kuu Marekani (MLS), inaingia katika hatua nyingine wiki hii, ambapo timu zilizofuzu hatua ya mtoano kutoka kanda ya Mashariki na ile ya Magharibi zitakuwa zikusaka ubingwa wa maeneo yao kabla ya kukutana katika fainali Jumamosi, Desemba 19, 2026 saa 7:00 usiku.

Kwa mujibu wa utaratibu wa MLS, uwanja utakaotumiwa kwa ajili ya mchezo huo bado haujajulikana, kwani sheria za ligi hiyo zinasema fainali itaandaliwa na timu iliyokuwa na ufaulu mzuri zaidi wakati wa msimu wa kawaida au timu zingine zinazoshiriki hatua ya mtoano.

Hata hivyo, wakati hivi sasa macho ya ulimwengu wa soka kwenye ligi hiyo yakisubiri kuanza kwa mechi za mtoano keshokutwa, Alhamisi,

nahodha wa Inter Miami, Lionel Messi, ameonyesha makali yake katika MLS baada ya kutwaa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu 2026, akiwa amefunga mabao 26 katika msimu wa kawaida wa ligi hiyo.

MESS 01

Mafanikio hayo yamemfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi hiyo kutwaa tuzo hiyo kwa misimu miwili mfululizo, ambapo nyota huyo wa Argentina amemaliza akiwa na tofauti ya mabao manne mbele ya mshambuliaji wa Dallas, Petar Musa, aliyefunga 22, huku straika wa Vancouver Whitecaps, Brian White, akishika nafasi ya tatu kwa mabao 20.


NI NAMBA TU

Pia, Messi amekuwa mchezaji wa sita pekee katika historia ya MLS kutwaa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu zaidi ya mara moja. Katika msimu wake wa nne tangu ajiunge na MLS, Messi alimaliza akiwa kinara wa wafungaji licha ya kucheza mechi 31 pekee za msimu wa kawaida.

Mabao yake 26 yaliambatana na asisti 17, hivyo kufikisha jumla ya mchango wa mabao 43, idadi inayoshika nafasi ya tatu kwa wachezaji wote waliowahi kurekodi mchango mkubwa wa mabao katika msimu mmoja wa MLS.

MESS 02

Mche zaji huyo mwenye umri wa miaka 39 aliongoza ligi kwa wastani wa mabao kwa kila mechi (0.87), huku akilingana na wachezaji wengine katika rekodi ya kufunga mabao zaidi ya moja kwenye mechi moja, baada ya kufanya hivyo mara sita. Pia alishika nafasi ya pili kwa wastani wa mabao kwa kila dakika 90, akiwa na wastani wa mabao 0.91.

Moja ya mambo yaliyovutia zaidi katika msimu wake ni uwezo wake wa kufunga mabao katika mchezo wa wazi (open play), kwani ya mabao 26 aliyofunga, ni moja pekee alilofunga kwa mkwaju wa penalti, huku 25  yakitokana na mchezo wa kawaida.

MESS 03

Idadi hiyo inashika nafasi ya pili kwa mabao mengi zaidi yaliyofungwa bila penalti katika msimu mmoja wa MLS, na rekodi hiyo inashikiliwa na Messi mwenyewe, aliyefunga mabao 28 bila penalti mwaka 2025. Tuzo yake ya hivi karibuni ya Kiatu cha Dhahabu imeendeleza rekodi yake ya kuvutia ya ufungaji mabao.

Baada ya kufunga mabao 29 mwaka 2025, Messi amekuwa mchezaji wa pili pekee katika historia ya MLS kufunga angalau mabao 25 katika misimu miwili mfululizo ya kawaida ya ligi.

Katika misimu mitatu iliyopita, Messi amefikisha mabao 75 katika mechi za msimu wa kawaida, idadi inayomfanya kushika nafasi ya pili kwa wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi ndani ya misimu mitatu katika historia ya ligi hiyo. Pia, ni mchezaji wa pili akimfuata Denis Bouanga, kufunga angalau mabao 20 katika misimu mitatu mfululizo.

MESS 04

HUKU PIA YUPO

Ushawishi wa nahodha huyo wa zamani wa Argentina katika kikosi hicho hauishii kwenye kufunga mabao pekee, ambapo mchango wake wa mabao 43 mwaka 2026 umemfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya MLS kurekodi mabao 40 au zaidi katika misimu miwili mfululizo.

Ubora wa Messi unaonekana zaidi katika miaka mitatu iliyopita kuanzia 2024 hadi 2026, amehusika na mabao 127, ikijumuisha mabao na asisti.

Idadi hiyo ni kubwa kwa tofauti ya michango 28 ya mabao ikilinganishwa na mchezaji anayemfuatia, Evander, aliyehusika nayo 98 kipindi hicho.

Kwa kutwaa tena tuzo ya Kiatu cha Dhahabu, Messi ameendelea kuimarisha nafasi yake kama mmoja wa wachezaji wenye ushawishi mkubwa zaidi katika safu ya ushambuliaji ya MLS, huku akiongeza tuzo nyingine binafsi katika maisha yake marefu ya soka.