Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matola makocha wanakuja na kumuacha Simba

KISTAAJABU ya Mussa utayaona ya Firauni; hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Kocha wa Simba, Zorani Maki kuondoka huku akikimbizana na rekodi ya aliyewahi kuwa Kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic anayeshikiria rekodi ya kudumu kwa muda mchache kwenye timu.

Kocha Krmpotic alidumu Yanga kwa siku 37 ambazo ni sawa na mwezi mmoja na siku saba.

Juzi Septemba 6, Simba imetangaza kuachana na Zoran Maki ambaye aliingia mkataba wa mwaka mmoja baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Kocha huyo amedumu kwa siku 70 sawa na miezi miwili na siku 10 huku kiungo na nahodha wa zamani wa Simba SC, Kocha Msaidizi, Seleman Matola akijijengea ufalme ndani ya timu hiyo kwa kuiongoza timu kwa muda mrefu akiwa kocha msaidizi.

Matola ambaye amewahi kukinoa kikosi cha vijana cha timu hiyo, ameweka rekodi ya kuwaongoza makocha sita wa kigeni ambao wamepita Simba akiwasaidia kazi kama kocha msaidizi.

Mwanaspoti linakuletea makocha waliopata nafasi ya kufanya kazi pamoja na Matola huku wao wakitupiwa virago kutokana na kushindwa kufikia malengo.


ZORAN v MATOLA

Ni kocha aliyedumu kwenye nafasi hiyo kwa muda mchache zaidi alitambulishwa na Simba Juni 28 akichukua mikoba ya Pablo Franco amedumu kwenye nafasi hiyo kwa siku 70.

Zoran Maki alitambulishwa Jumanne, Juni 28 na juzi Septemba 6 aliachana na klabu hiyo akiwa ameiongoza timu hiyo kwenye mechi tatu za mashindano ikiwamo Ngao ya Jamii aliyopoteza kwa mabao 2-1 mbele ya Yanga na mbili za Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar aliyoshinda 2-0 na Geita Gold aliyoikuba na ushindi wa 3-0 na kumkuacha Matola akiisimamia timu akimsubiriwa kocha mpya.


PABLO v MATOLA

Simba ilithibitisha kuvunja mkataba na Kocha Pablo Franco Martin baada ya kutoa taarifa hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii huku pia wakimtakia kila la heri kocha huyo kwa kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kuondoka kwa Pablo kulikuja siku chache baada ya timu hiyo kuondoshwa kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano Kombe la Shirikisho (ASFC) baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Baada ya kufikia makubaliano hayo, sasa kikosi cha timu hiyo kilikuwa chini ya Kocha Matola katika kipindi cha kumaliza msimu huo.

Pablo alitua nchini akichukua nafasi ya aliyekuwa Kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa aliyetimuliwa Oktoba 26, mwaka jana.

Mafanikio ambayo Pablo anaweza kujivunia ni kuipa Simba ubingwa wa nne wa michuano ya Mapinduzi 2022. Kisha kufikisha robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.


GOMES v MATOLA

Oktoba 26, 2021, timu hiyo ililiridhia ombi la aliyekuwa Kocha Mkuu, Didier Gomes Da Rosa la kuachana kuanzia siku hiyo baada ya tathmini na majadiano ya kina, pande zote zikaafikiana kwa mujibu wa mkataba na manufaa ya wote.

Kuondoka kwa Gomes kulikuja siku chache baada ya timu hiyo kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana ilipokubali kichapo cha mabao 3-1, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Gomes alitua nchini akichukua nafasi ya Kocha, Mbeligiji Sven Vandenbroeck ambapo alikiongoza kikosi cha Simba kwenye mechi 33 huku akishinda mechi 25, sare nne na kupoteza nne.

Kutokana na hatua hiyo, aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Thierry Hitimana, ndiye aliyechukua mikoba ya Gomes akisaidiwa na Seleman Matola.

Gomes alikuja nchini siku chache baada ya Sven kuachana na vigogo hao Januari 7, kisha kutimkia FAR Rabat ya Morocco, saa chache tu baada ya kuiongoza Simba kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga FC Platinum ya Zimbabwe.

Gomes ambaye ni raia wa Ufaransa akakabidhiwa mikoba ya kuwanoa wababe hao wa Msimbazi na kilichofuata ni historia na rekodi ‘baab-kubwa’ ndani na nje ya nchi akiwa na chama hilo ambalo linawatisha hata vigogo wa Afrika kwa sasa.


SVEN v MATOLA

Uongozi wa Simba uliachana na Sven Vandenbroeck ikiwa ni siku chache baada ya kushinda 4-0 Uwanja wa Mkapa dhidi ya FC Platinum kwenye Ligi ya Mabingwa na kusonga hatua ya makundi na timu kuwa chini ya Matola kwa muda.

Aliondoka Simba ikiwa nafasi ya pili kwenye ligi baada ya michezo 15 na pointi 35 ikifungwa mbili na sare mbili ikishinda 11 na kutimkia FAR Rabat ya Morocco na Januari 24 Simba ikamtangaza Didier Gomes kama kocha mkuu akitokea El Mereikh ya Sudan


AUSSEMS v MATOLA

Patrick Aussems ambaye alichukua mikoba ya Mfaransa Pierre Lechantre, alitokea kuwa kipenzi cha mashabiki wa Msimbazi tangu alipoanza kukinoa rasmi kikosi hicho na hata kufikia hatua ya kumpachika jina la utani ‘Uchebe’.

Mr Uchebe ameondoka akiwaachia mashabiki wa simba kumbukumbu zenye msisimko wa kipekee, haswa kumbukumbu nzuri ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kupenya hadi robo fainali msimu wa 2018/2019.

Aussems alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara. Pia mwanzo mwa msimu huo na alifanikiwa kutwaa Ngao ya jamii. Mafanikio ya Aussems ndani ya Simba ambayo ni vigumu kusahaulika ni kufika robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika. Licha ya kupangiwa vigogo kutoka kaskazini mwa Afrika Simba haikupoteza mchezo hata mmoja katika uwanja wake wa nyumbani Dar es Salaam, ingawa pia alipata changamoto ya kupoteza mabao mengi kwa mechi za ugenini, Katika kundi la Simba kulikuwa na vigogo kama AS Vita ya DR Congo, Al Ahly ya Misri, JS Saoura ya Algeria.

Alipotimuliwa timu ilikuwa chini ya Matola hadi alipoletwa Gomes kuendelea alipoishia. Hakuna anayejua kocha mpya ajaye Msimbazi, naye akaondoka na kumuacha Matola au la, tusubiri tuone!