Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliowahi kukiwasha Yanga Day

Muktasari:

  • Yanga imekuwa na historia ya kufanya vizuri katika mechi hizo za kilele cha Wiki ya Mwananchi na safari hii tumekuandalia nyota ambao walifanya vizuri kwenye matamasha hayo na kuwa mhimili mkubwa wa timu.

KILA msimu mpya kuanza Yanga huwa wanafanya sherehe za kilele cha wiki ya Mwananchi ambayo kwa mwaka 2026 inafanyika leo, Agosti 09 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Yanga imekuwa na historia ya kufanya vizuri katika mechi hizo za kilele cha Wiki ya Mwananchi na safari hii tumekuandalia nyota ambao walifanya vizuri kwenye matamasha hayo na kuwa mhimili mkubwa wa timu.

Mabingwa hao watetezi na wanafainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2023 msimu huu wamesajili baadhi ya wachezaji akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Mamelodi Sundown, Peter Shalulile na wengineo ambao watatoa burudani kwenye tamasha hilo lililoanzishwa mwaka 2019.


CELESTINE ECUA

Winga huyo alikiwasha haswa kwenye kilele cha wiki ya wananchi na Yanga ilicheza na Bandari ya Kenya ikaondoka na ushindi wa bao 1-0 ambalo alifunga nyota huyo.

Ecua aliyewahi kung’ara akiwa Zoman FC na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Ivory Coast, tamasha hilo lilimtambulisha rasmi kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakimuona tu mitandaoni.


LASSINE KOUMA

Miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango cha kuvutia mara tu baada ya kutambulishwa kwenye Yanga Day ni kiungo mshambuliaji, Lassine Kouma.

Raia huyo wa Mali alitua kwa wananchi akitokea Stade Malien, moja ya klabu kongwe nchini humo, akiwa na sifa ya ubunifu, uwezo wa kutengeneza nafasi na kufunga mabao kutoka eneo la kiungo.

Katika mechi yake ya kwanza ya Yanga Day, Kouma aliwavutia mashabiki kwa utulivu wake akiwa na mpira, pasi zake za mwisho na uwezo wa kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji, jambo lililomfanya aanze kujenga matumaini makubwa kwa mashabiki kabla ya msimu kuanza.


DUKE ABUYA

Kiungo huyo raia wa Kenya, jukwaa la kilele cha wiki ya wananchi lilimtambulisha baada ya kupewa dakika 45 na kuzitendea kwa haki. Kabla ya kucheza mashabiki walikuwa na mashaka Abuya atacheza eneo gani?.

Abuya ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2024/25 akitokea Singida Black Stars aliingia kwenye mioyo ya mashabiki baada ya kuonyesha kwango bora kwenye tamasha hilo ambalo linakutanisha mashabiki kutoka sehemu mbalimbali.


PACOME ZOUZOUA

Msimu wa 2023/24 licha ya kikosi hicho kuwa na nyota wengi wenye ubora Pacome Zouzoua aliibuka kinara kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha na kuwa gumzo kwa mashabiki.

Walikuwa nyota kama Clatous Chama ambaye kabla hajatimkia Singida, Stephane Aziz Ki alianzia benchi, Duke Abuya, Maxi Nzengeli na Prince Dube nyota wa mchezo akawa Pacome na ndiye aliyetambulishwa wa mwisho wakati wa utambulisho wa nyota wa kikosi cha timu hiyo.

Kwenye mchezo huo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 bao la utangulizi kutoka kwa wapinzani lilifungwa kipindi cha kwanza huku mabao mawili ya Yanga yakiwekwa kambani na Mudathir Yahya na Stephane Aziz Ki aliyekwamisha mpira nyavuni kwa mkwaju wa penalti.


KENNEDY MUSONDA

Hili ndilo tamasha la mwisho lililofanyika Julai 22, 2023 na bao la Mzambia, Kennedy Musonda lilitosha kuipa timu hiyo ushindi wa pili baada ya ule wa mabao 2-0, dhidi ya Aigle Noir kutoka Burundi, mchezo uliopigwa Agosti 30, 2020.

Tamasha hili lilinogeshwa na mastaa wengi huku na aliyeteka hisia za mashabiki ni aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mahlatsi Makudubela ‘Skudu’ aliyesajiliwa akitokea Marumo Gallants ya kwao Afrika Kusini.

Yanga iliingia katika mchezo huo ikiwa na kocha mpya Muargentina, Miguel Gamondi aliyetambulishwa Juni 24, 2023 kuchukua nafasi ya Nasreddine Nabi aliyejiunga na FAR Rabat ya Morocco.


HERITIER MAKAMBO

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Aigle Noir, msimu wa 2024/25 Yanga ikaduwazwa kwa kuchapwa 2-1, dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Tamasha hili ndilo liliibua ushangiliaji wa aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo kabla ya kutimkia Namungo msimu wa 2024/25 Makambo ambaye baadae alikuwa kipenzi cha mashabiki wa jangwani.


PATRICK SIBOMANA

Hili lilikuwa pambano la kwanza la ‘Wiki ya Mwananchi’ kwa Yanga na ilicheza mchezo na Kariobang Sharks ya Kenya.

Katika mchezo huu uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na Kariobang ilipata bao la utangulizi dakika ya 49 lililofungwa na Patrick Otieno kisha dakika sita mbele, Patrick Sibomana aliisawazishia Yanga kwa penalti.

Sibomana ulikuwa ni usajili mpya na alikuwa mshambuliaji kiongozi wa Yanga kwa msimu huo kutokana na mchezo huo wananchi waliamini wamepata jembe na aliitumikia kwa msimu huo na baadae kuachwa na timu hiyo.


TUISILA KISINDA

Yanga ikionekana timu tishio, ilicheza mechi ya pili dhidi ya Aigle Noir kutoka Burundi na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Winga Tuisila aliibuka nyota wa mchezo kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na aina ya uchezaji wake akiwakimbiza mabeki wa timu pinzani na alitupia bao kwenye mchezo huo.

Mabao kwenye mchezo huo yalifungwa na Mghana, Michael Sarpong katika dakika ya 59 kwa kichwa kutokana na krosi ya Ditram Nchimbi huku la pili likifungwa na winga Kisinda ‘TK Master’.

Makambo alianza kuifungia Yanga bao la utangulizi dakika ya 30 ya mchezo baada ya kupokea pasi ya Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Zanaco ilisawazisha kupitia kwa Ackim Mumba dakika ya 60, kisha Kelvin Kapumbu akaipatia bao la ushindi dakika ya 76.


BERNARD MORRISON

Agosti 6, 2022, Yanga ilifanya vibaya tena katika sherehe hizo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Vipers ya Uganda.

Mabao ya Vipers katika mechi hiyo yalifungwa na viungo, Milton Karisa na Anukani Bright.

Licha ya Yanga kufungwa na timu hiyo mashabiki wa timu hiyo walifurahishwa na aina ya uchezaji kwa baadhi ya wachezaji wao huku Morrison akiwa sehemu yao pamoja na kwamba alianzia benchi lakini aliwapa burudani.