Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makata alivyoirejesha Polisi Tanzania Ligi Kuu na rekodi kibao

MAKATA Pict

Muktasari:

  • Uongozi wa kikosi hicho cha maafande, ulimpa mkataba wa miaka miwili Makata, baada ya kocha huyo kutokuwa na timu yoyote tangu mara ya mwisho alipoachana na Tanzania Prisons, Desemba 28, 2024, kutokana na mwenendo mbaya katika Ligi Kuu Bara.

MATUMAINI ya Mkoa wa Kilimanjaro kupata timu ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2026-2027, yalitimia rasmi Julai 16, 2026, baada ya maafande wa Polisi Tanzania kupata nafasi hiyo muhimu kutokana na kiwango bora chini ya Kocha Mkuu, Mbwana Makata.

Uongozi wa kikosi hicho cha maafande, ulimpa mkataba wa miaka miwili Makata, baada ya kocha huyo kutokuwa na timu yoyote tangu mara ya mwisho alipoachana na Tanzania Prisons, Desemba 28, 2024, kutokana na mwenendo mbaya katika Ligi Kuu Bara.

Makata alikiongoza kikosi hicho katika jumla ya mechi 14, za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2024-2025, ambapo kati ya hizo alishinda mbili tu, sare tano na kupoteza saba na alikiacha kikishika nafasi ya 15, kwenye msimamo na pointi 11.

MAKA 01

Kutokana na mwenendo huo usioridhisha, mabosi wa maafande waliachana na Makata na nafasi yake kumpa Kocha Amani Josiah aliyejiunga na timu hiyo Januari 2, 2025 kwa mkataba wa miezi sita akitokea Geita Gold iliyokuwa Ligi ya Championship.

Baada ya Josiah mkataba wake kuisha akajiunga na Dodoma Jiji ingawa msimu wa 2026-2027, ataifundisha Mashujaa FC, huku Prisons ikimteua Mkenya Zedekiah ‘Zico’ Otieno, kisha kuondoka na nafasi yake kuchukuliwa na Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’.

Prisons ilimwondoa Makata kwa kuhofia kuishusha daraja kutokana na mwenendo wa timu hiyo msimu wa 2024-2025, ingawa moja ya jambo la kushangaza ni kumwona pia kocha huyo akikishusha kikosi hicho cha maafande ila akiwa na klabu nyingine.

Sasa wakati kocha huyo alipotambulishwa kukiongoza kikosi hicho kwa msimu wa 2025-2026, Mwanaspoti linakuletea makala ya rekodi mbalimbali za kuvutia alizoziandika, akiwa ni miongoni mwa makocha bora watakaoendelea kuzungumzwa kila kukicha.

MAKA 02

MSIMU WA MATUMAINI

Tangu Polisi ishuke daraja msimu wa 2022-2023, ilikuwa haijawahi kumaliza katika nne bora kwenye Ligi ya Championship, japo msimu wa 2025-2026, kikosi hicho kilimaliza nafasi ya tatu na kucheza mechi za Play-Off ya kupanda Ligi Kuu Bara.

Msimu wa 2025-2026, timu hiyo ilimaliza nafasi ya tatu na pointi 66, baada ya kushinda mechi 20, sare sita na kupoteza nne na kucheza Play-Off ya kupanda Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya Kwanza iliyomaliza ikishika nafasi ya nne na pointi 61.

Katika mechi za Play-Off, Polisi Tanzania ilianza kwa kishindo kwa kuitoa Mbeya Kwanza kwa jumla ya mabao 7-1, baada ya kushinda kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora mabao 4-0, kisha kushinda kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi mabao 3-1.

Baada ya hapo, Polisi ikacheza mechi nyingine ya Play-Off dhidi ya maafande wenzao wa Tanzania Prisons iliyoshika nafasi ya 13 na pointi 32 katika Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026 na kikosi hicho kilishinda kwa jumla ya mabao 4-1.

Katika mechi ya kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Ushirika, Polisi iliifunga Prisons mabao 4-0, Julai 12, 2026, kisha marudiano kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya ikachapwa bao 1-0, Julai 16, 2026 na kurejea Ligi Kuu kwa jumla ya mabao 4-1.

Maafande wa Prisons imeshuka daraja kupitia Play-Off, baada ya kumaliza nafasi ya 13 na pointi 32, ikianza kucheza dhidi ya kikosi cha Mbeya City kilichomaliza kikishika nafasi ya 14 na pointi 30 na timu hiyo kutolewa kwa jumla ya mabao 2-0.

Prisons ilikuwa ni timu ya tatu ya Ligi Kuu Bara kushuka daraja na kwenda kushiriki Championship kwa msimu wa 2026-2027, ikiungana na Mtibwa Sugar iliyomaliza ya 15 na pointi 27 na KMC FC iliyoburuza mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi tisa.

Polisi imeungana na Kagera Sugar kucheza Ligi Kuu Bara msimu wa 2026-2027, baada ya kumaliza nafasi ya pili na pointi 72 na mabingwa wa Ligi ya Championship kwa msimu wa 2025-2026, timu ya Geita Gold iliyomaliza ikiwa ni vinara na pointi 77.

MAKA 03

AWEKA REKODI POLISI TANZANIA

Makata aliyetambulishwa rasmi Julai 9, 2025, Jijini Dodoma na mwenyekiti wa kikosi hicho, Kamishna wa Polisi Jamii, CP Faustine Shilogile ameandika rekodi nyingine ya kuvutia baada ya kuipandisha timu hiyo Ligi Kuu Bara kwa mara ya pili.

Makata aliyejiunga na Polisi Tanzania akichukua nafasi ya Kocha Mkuu, Mussa Rashid kwa mara ya kwanza aliipandisha timu hiyo Ligi Kuu Bara msimu wa 2019-2020, kisha akaipandisha tena 2025-2026, baada ya kushuka daraja msimu wa 2022-2023.

Msimu wa 2022-2023, Polisi ilimaliza Ligi Kuu ikishika nafasi ya 15 na pointi 25, ikishinda mechi sita tu, sare saba na kupoteza 17, ikifunga mabao 25 na kuruhusu 54, ikiungana na Ruvu Shooting na Mbeya City, iliyorejea msimu wa 2024-2025.

MAKA 04

TIMU SABA LIGI KUU BARA

Jambo lingine ambalo uongozi wa Polisi ulizingatia kwa Makata, ni kutokana na rekodi zake zinazombeba za kupandisha timu kutoka Championship hadi kwenda Ligi Kuu Bara, kwani tofauti na kikosi hicho ila, ameshafanya hivyo, akiwa na nyingine.

Baada ya kuipandisha Polisi Tanzania Ligi Kuu msimu wa 2025-2026, Makata amefikisha jumla ya timu saba kwa sasa, akianza na Mji Mpwapwa FC ya Dodoma mwaka 1999, kisha akaipandisha Twiga Sports ya Kinondoni, jijini, Dar es Salaam mwaka 2002.

Makata akaipandisha Alliance FC ya Mwanza Ligi Kuu Bara msimu wa 2018-2019, ingawa ilishuka 2019-2020, baada ya kumaliza nafasi ya 17 na pointi 45, ikiungana na Lipuli ya Iringa, Ndanda ya Mtwara na Singida United zilizoshuka moja kwa moja.

Baada ya hapo akaipandisha Polisi Tanzania msimu wa 2019-2020, japo ilishuka msimu wa 2022-2023, ilipomaliza nafasi ya 15 na pointi 25, kufuatia kushinda mechi sita, sare saba na kupoteza 17, huku ikifunga jumla ya mabao 25 na kuruhusu 54.

Makata akaendeleza tena rekodi yake nzuri ya kuzipandisha timu kutokea Ligi ya Championship hadi Ligi Kuu Bara na alifanya hivyo, msimu wa 2020-2021, alipoipandisha Dodoma Jiji, ambayo hadi leo hii inaendelea kutesa ikiwa haijashuka.

Rekodi nyingine ya kuvutia kwa Makata ni pale alipoipandisha Pamba Jiji FC Ligi Kuu msimu wa 2023-2024, baada ya miaka 23, tangu iliposhuka mwaka 2001, ikiungana na timu nyingine saba zikiwemo za Lipuli FC ya Iringa na Reli ya Morogoro.

Timu nyingine zilizoshuka mwaka 2001, zilikuwa ni Kagera Stars ambayo kwa sasa ni Kagera Sugar iliyoshuka Ligi Kuu msimu wa 2024-2025 na kurejea tena kwa msimu wa 2025-2026, Milambo FC ya Tabora, Majimaji ya Songea na 44 KJ ya Mbalizi Mbeya.

Baada ya hapo akaipandisha tena Polisi Tanzania msimu wa 2025-2026, ikiwa ni timu ya saba kwake kuipandisha kutoka Ligi ya Championship hadi Ligi Kuu Bara, ikiwa ni mara ya pili kwake, baada ya kuipandisha mara ya kwanza msimu wa 2019-2020.

MAKA 05

KAULI YA MAKATA

Akizungumza na Mwanaspoti, Makata anasema mojawapo ya siri kubwa ya kuendeleza rekodi bora za kuzipandisha timu daraja kutoka Championship hadi Ligi Kuu Bara, ni kutokana na ushirikiano mzuri kati yake, wachezaji na viongozi mbalimbali.

“Kila mtu katika nafasi yake anamtegemea mwenzake pia, mimi siwezi kufanikiwa ikiwa sitapata ushirikiano wa wachezaji na viongozi husika ambao ndio wanaofanya usajili, kwangu ni jambo ninalojivunia timu zote nilizofundisha,” anasema Makata.