Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MAGOFU: Viwanja hivi imebaki historia

MAGOFU Pict

Muktasari:

  • Lakini kama ilivyo kwa mchezo wa soka wenyewe, kuna muda timu huwa bora kiasi cha kuchukua makombe, lakini ghafla huanguka na zisiweze kunyanyuka tena na mwisho zikafutika kabisa.

DONBAS, UKRAINE: SOKA ni mchezo wenye historia ndefu. Viwanja vinavyotumika huwa ni sehemu ya alama ya historia hiyo ambapo watu hushuhudia furaha, huzuni na kumbukumbu zinazoishi milele.

Lakini kama ilivyo kwa mchezo wa soka wenyewe, kuna muda timu huwa bora kiasi cha kuchukua makombe, lakini ghafla huanguka na zisiweze kunyanyuka tena na mwisho zikafutika kabisa.

Hapa tunakuletea baadhi ya viwanja ambavyo vilijengwa kwa gharama kubwa na baadhi vikawa sehemu ya historia, lakini sasa havitumika na vimebaki kuwa magofu yenye wadudu, ndege na miti.

MAGO 01

STADIO OOSTERPARK, UHOLANZI

Uwanja huo ulikuwa maskani ya klabu ya Uholanzi, FC Groningen hadi ilipohama mwaka 2006.

Hapa ndipo ambapo Johan Cruyff akiwa kijana alipachika bao katika mchezo wake wa kwanza akiwa na Ajax. Pia, ilikuwa ni uwanja ambapo Arjen Robben alipofahamika mara ya kwanza mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Baada ya kuachwa kwa muda mrefu na hali ya hewa, viti vimeharibika. Uwanja huo ulikuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 20,000, lakini sasa hautumiki tena.


ARENA DA AMAZONIA, BRAZIL

Uwanja huo ulijengwa kwa ajili ya mashindano ya  Kombe la Dunia la 2014 lililofanyika Brazil. Ulitumika katika mchezo ambao ulishuhudia England ikipoteza 2-1 dhidi ya Italia katika hatua ya makundi. Ulitumiwa kuchezea mechi nne katika mashindano hayo.

Hata hivyo, miaka 11 baada ya michuano hiyo kupita, uwanja huo wenye kuingiza mashabiki 40,000 umebaki kama gofu mara chache sana wenyeji wa mji walikuwa wakienda kucheza mechi zao hapo, ambapo mashabiki hawakuwa wanafikia hata 1,000.

Kwa ujumla eneo la kuchezea limeharibika, viti na paa kwa sehemu kubwa vimeng’oka na inadaiwa uliigharimu serikali ya Brazil karibu Pauni 200 milioni katika ujenzi.

MAGO 02
MAGO 02

STADIO FLAMINIO, ITALIA

Nyumbani kwa muda kwa timu za Lazio na Roma katika msimu wa 1989/90

Stadio Flaminio uliopo jijini Roma ulijengwa mwishoni mwa miaka ya 1950 wakati Italia inataka kuandaa michezo ya Olimpiki iliyofanyika 1960.

 Uwanja huo ulitumika kuandaa mechi ya fainali ya  Olimpiki ambapo Yugoslavia iliifunga Denmark kwa mabao 3-1. Hadi kufikia 2011 ulikuwa ukitumiwa na  timu ya taifa ya  raga ya Italia.

Wakati wa msimu wa 1989/90 pale uwanja wa Olimpiki  ulipokuwa ukiendelea na ukarabati ulitumika kwa muda na Roma na Lazio.

 Mwaka huo, Napoli ya Maradona ilishinda Serie A, na yeye alipachika bao.


STADION ZA LUZANKAMI, JAMHURI YA CZECH

Mwaka 1995 Uwanja wa Za Luzankami ulitumika kuchezea mchezo wa kirafiki kati ya Czech na Finland, ambapo wenyeji waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 baada ya mabao mawili ya mfungaji wa zamani wa Liverpool na Aston Villa, Patrick Berger.

Kutokana na uwanja huo kutotumika  kwa mchezo wowote tangu 2012, umebaki kuwa gofu lisilo na kitu na miti pamoja na wadudu wameufanya kuwa nyumba yao.

Uwanja huu ulikuwa ukitumika kama nyumbani na timu ya FC Zbrojovka Brno, ambao 1977 walishinda taji la Czech baada ya kuifunga Dukla Prague, lakini walilazimika kuachana nao kwa sababu haukuendana na kanuni mpya za Fifa.

MAGO 03

AVANHARD STADIUM, UKRAINE

Uwanja wa Avanhard uliopopo Ukraine katika Mji wa Chernobyl haujawahi kutumika tangu 1986 baada ya mlipuko kutokea katika Kiwanda cha Nishati ya Nyuklia cha Chernobyl kilicho karibu na Jiji la Pripyat ambalo baadaye liliingizwa kwenye eneo lililozuiwa kwa sababu lilionekana hatari kwa maisha ya binadamu.

Jiji la Chernobyl bado halikaliwi na mtu yeyote hadi  sasa kutokana na maagizo ya serikali. Jambo la kusikitisha ni kwamba uwanja huo ulijengwa mwaka huohuo wa maafa, hivyo haukuwahi kuandaa mchezo wowote. Kwa sasa katika eneo la kuchezea imeota miti mirefu.


CATHKIN PARK, SCOTLAND

Uwanja huo uliopo Glasgow uliwahi kutumiwa na timu ya Third Lanark. Uwanja huo kwa sasa umebaki kuwa kama bustani ambayo ina miti iliyozungukwa na ndege.

Inaripotiwa kwamba Scotland iliifunga England katika uwanja huo 1896 katika mchezo ambao ulishuhudiwa mashabiki 20,000 wakiingia kuutazama.

Mara ya mwisho kutumika ilikuwa 1967 ambapo Third Lanark ilicheza mechi  ya mwisho. Licha ya uwanja huo ambao ulifunguliwa 1886 kuwa hautumiki kwa sasa, viti na majukwaa vimeendelea kuwepo hadi leo.

MAGO 04

GUANGZHOU FC STADIUM, CHINA

Guangzhou FC walitarajia kujenga uwanja mkubwa zaidi duniani. Uwanja huo wa viti 100,000 ulionekana kuwa wa kisasa kupitia ramani yake na pengine ingekuwa mahala pazuri kwa  Guangzhou  ambayo imeshinda taji la Ligi Kuu China mara saba mfululizo kati ya 2011 na 2017, lakini ajabu hadi sasa haujakamilika.

Inaelezwa moja ya sababu zilizosababisha usikamilike ni wamiliki wa klabu walikumbana na shida kubwa za kifedha kutokana na madeni yanayokadiriwa kufikia takriban Pauni 220 bilioni.

Timu ilianza kufanya vibaya na baadaye ikashuka kwenda Ligi Daraja la Kwanza  2022 ambako ilicheza kwa miaka miwili kabla ya timu kuvunjwa Januari 6, 2025.

Kilichobaki kwa sasa  ni jengo kuukuu ambalo halina matumaini ya kuendelezwa.


ESTADIO SANT’ELIA, ITALIA

Uwanja huo ulikuwa ukitumiwa na Cagliari. Vilevile ulitumika katika Kombe la Dunia 1990 ambapo England ilicheza mechi zake zote tatu za makundi.

Kwa ujumla ulikuwa na uwezo wa kubeba mashabiki 60000. Uwanja huo unapatikana katika kisiwa cha Sardinia nchini Italia kilomita kadhaa kutoka bahari ilipo.

Tangu 2017 hautumiki baada ya Shirikisho la Soka la Italia kudai haukidhi vigezo vya kuchezewa mechi za Serie A jambo lililoilazimu Cagliari kuhama ikiwa ni baada ya miaka 47 tangu ianze kuutumia.

Licha ya kupewa nafasi ya kuurekebisha uwanja huo mamlaka eneo hilo zilikataa kwa sababu zinaamini unahitaji ukarabati mkubwa. Hadi sasa umebaki kuwa gofu tu baada ya kutotumika kwa muda mrefu.

MAGO 05

DONBAS ARENA, UKRAINE

Ni uwanja wa zamani wa Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine. Uwanja huo haujachezewa mechi yoyote kwa muda mrefu. Donbas Arena sasa haionekani kama ilivyokuwa hapo awali.

Uwanja huo uliachwa 2014 baada ya kuibuka kwa mzozo kati ya Urusi na Ukraine na tangu hapo haukuwahi kutumiwa teana na Shakhtar Donetsk pamoja na timu nyingine.

Uwanja huo ulifunguliwa 2009  na mbali ya kutumiwa na Shakhtar pia ulitumika kwa ajili ya michuano ya Euro 2012, ukiandaa mchezo wa England na Ukraine ambao ulimalizika kwa wageni kushinda bao 1-0 kupitia kwa  Wayne Rooney.

Pia zilipigwa mechi mbili za nusu-fainali ambapo mojawapo ilikuwa ile ya Hispania dhidi ya Ureno iliyomalizika kwa Hispania kushinda mabao 4-2.

Uwanja huo pia umeathiriwa na mashambulizi ya hivi karibuni na njia zilizokuwa safi zinazoelekea uwanjani kwa sasa zina majani na magugu yanayoongezeka kila siku.

MAGO 06

NOU MESTALLA, HISPANIA

Uwanja mpya wa Valencia ambao haujakamilika

Huo ni uwanja wa Valencia ulioanza kujengwa tangu 2008. Wakati unaanza kujengwa ulitajwa kuwa moja kati ya viwanja bora zaidi duniani. Hata hivyo, kutokana na anguko la kiuchumi lililotokea Hispania kuanzia 2008 lilisababisha ujezi kusimama na iliripotiwa kwamba Valencia ilikuwa na deni la Euro 550 milioni.

Mwaka 2009 klabu hiyo iliachana na ujenzi wa uwanja huo ingawa hadi sasa Valencia bado ina matumaini kwamba uwanja unaweza kukamilika siku zijazo pale itakapopata pesa za kujenga upya, lakini kwa sasa uwanja huo uliotabiriwa kuwa wa kisasa na kuvutia umebaki kuwa gofu linalokaliwa na wadudu na ndege.