Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namba zinavyowapa ubingwa wababe Ulaya 2026-27

NAMBA Pict

Muktasari:

  • Ligi ya Mabingwa Ulaya inarejea kwa msimu wa 2026-27 ikiwa na ratiba nyingine iliyojaa michezo katika mfumo wake wa awamu ya ligi wenye timu 36, huku mechi za kwanza zikianza leo Jumanne, Septemba 8, 2026.

LONDON, ENGLAND; NANI kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2026-27? Je, PSG itaweza kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo? Je, Arsenal hatimaye inaweza kushinda taji ambalo limekuwa likiikwepa siku zote? Je, Real Madrid inaweza kuondolewa kwenye kinyang’anyiro? Kipute kinarudi upya na vita ni vita muraaa!

Ligi ya Mabingwa Ulaya inarejea kwa msimu wa 2026-27 ikiwa na ratiba nyingine iliyojaa michezo katika mfumo wake wa awamu ya ligi wenye timu 36, huku mechi za kwanza zikianza leo Jumanne, Septemba 8, 2026.

Kutokana na matokeo ya michezo minane, timu zitapangwa katika msimamo wa ligi, huku nane za juu zikifuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora. Wapinzani wa timu hizo nane wataamuliwa kupitia hatua ya mchujo itakayoshirikisha 16 zitakazomaliza nafasi ya tisa hadi ya 24 katika awamu ya ligi. Kuanzia hapo, mambo yatakuwa rahisi zaidi; mfumo wa kawaida wa mtoano wa mechi mbili utatumika kuzipunguza timu hadi kubaki mbili za mwisho, na hatimaye bingwa atakayetangazwa kwenye Uwanja wa Metropolitano mjini Madrid, Juni 5 mwakani.

Lakini ni timu zipi zitamaliza katika nafasi nane za juu kwenye awamu ya ligi? Ni zipi zina uwezekano mkubwa wa kubaki salama katika hatua ya mchujo? Na ni nani ataondoka na ubingwa? Supercomputer ya Opta imebashiri na haya ndiyo majibu iliyokuja nayo. Kumbuka kwamba msimu uliopita haikupatia utabiri wake kwa usahihi baada ya kutabiri Liverpool ingeshinda taji hilo.

Lakini, Liverpool ilitolewa katika hatua ya robo fainali na PSG, ambao hatimaye walitwaa ubingwa licha kuwekwa nafasi ya tatu kwa nafasi kubwa ya kushinda. Arsenal, ambayo ilifungwa na PSG katika fainali ilikuwa ya pili katika utabiri wa kompyuta hiyo. Kwa hiyo, utabiri haukuwa mbali sana, lakini haukuwa sahihi kabisa. Twende pamoja!


NAMB 01

WANAOPEWA NAFASI UBINGWA 2026-27

Baada ya kukaribia kutwaa ubingwa msimu uliopita na kuangukia kwenye mikwaju ya penalti, Arsenal sasa inaonekana kuwa timu inayopigiwa nafasi zaidi msimu huu. Ilimaliza kileleni mwa awamu ya ligi msimu uliopita ikiwa timu ya kwanza kuwahi kushinda mechi zote nane.

Na ingawa ndiyo inayopigiwa upatu wa kushinda mashindano, ni timu ya pili yenye uwezekano mkubwa zaidi wa kumaliza kileleni mwa awamu ya ligi kwa mtazamo wa Opta, ikiwa na nafasi ya asilimia 18.5 kufanya hivyo. Wakati msimu uliopita ikiwa na moja ya ratiba rahisi zaidi za wapinzani katika awamu ya ligi kwa mujibu wa uchambuzi, safari hii ina ratiba ngumu zaidi. Ina uwezekano mkubwa sana wa kufuzu hatua ya mtoano, ikifanya hivyo katika asilimia 93.1.

Hata hivyo, ukweli kwamba italazimika kucheza ugenini dhidi ya Bayern Munich utabiri unawapa mabingwa hao wa Ligi Kuu Ujerumani nafasi kubwa katika awamu ya ligi. Bayern ilimaliza kileleni katika utabiri wa alama nyingi zaidi ikiwa na asilimia 19.8, kuliko timu nyingine yoyote, na pia ndiyo iliyofuzu hatua ya mtoano mara nyingi zaidi, ikiwa na asilimia 93.5. Hata hivyo, ina uwezekano mdogo wa kushinda mashindano yote kuliko Arsenal, ikiwa na nafasi ya asilimia 19.9, kwa sababu Arsenal ndiyo timu yenye nguvu zaidi duniani kwa sasa kwa mujibu wa Opta.

Kwa upande wake, Manchester City inapewa nafasi ya asilimia 12 ya kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili, baada ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza 2022-23. Hata hivyo, katika misimu mitatu tangu ilipotwaa ubingwa, imefika robo fainali, hatua ya mchujo ya mtoano na ya 16 bora; hivyo itahitaji kuboresha kiwango chake kwa kiasi kikubwa ikiwa inataka kwenda hadi mwisho.

Zaidi ya hapo, kati ya timu zinazowania ubingwa, ina ratiba ngumu zaidi katika awamu ya ligi, hivyo itahitaji kufanya vizuri ili kufuzu katika timu nane za juu. Hata hivyo, supercomputer bado inaipa City nafasi ya asilimia 86.3 ya kufuzu hatua ya 16 bora. Mabingwa watetezi PSG ni wa nne kwenye orodha ya wanaopewa nafasi ikiwa na asilimia 7.7 ya kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo. Real Madrid ndiyo timu pekee iliyowahi kushinda ubingwa huo mara tatu mfululizo, wakati Real Madrid, Ajax na Bayern zote zilifanya hivyo pia katika enzi ya Kombe la Ulaya.


NAMB 02

WENGINE HAWA HAWAPA

Barcelona haijashinda Ligi ya Mabingwa tangu 2015, lakini kwa mtazamo wa Opta ina nafasi ya kufanya hivyo msimu huu. Imepewa asilimia 7.0 ya kushinda. Kwa upande wa Real Madrid, haiwezi kamwe kuondolewa linapokuja suala la Ligi ya Mabingwa ikiwa imeshinda mara mbili katika misimu mitano iliyopita na mara 15 kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na enzi ya Kombe la Ulaya.

Lakini, nafasi yake ndogo ya asilimia 5.1 ya kutwaa ubingwa inaonyesha kwamba haijashinda taji kubwa tangu ilipotwaa Ligi ya Mabingwa msimu wa 2023-24, na katika misimu miwili iliyopita haikufanikiwa hata kuvuka robo.

Liverpool pia ina historia kubwa Ulaya na haipaswi kuwekwa nje. Ilifika fainali mara tatu katika misimu mitano kati ya 2017-18 na 2021-22. Kwa sasa inapewa nafasi sawa na Madrid ya kushinda tena mashindano hayo, ikiwa na asilimia 5.1, na nafasi ya asilimia 11.2 ya kufika fainali.


NAMB 03

HAWA PIA WAPO

Je, huu unaweza kuwa msimu ambao Manchester United itarudi vyema kwenye kundi la timu bora zaidi duniani kwa kufanya safari ya kushtukiza hadi kutwaa ubingwa wa Ulaya? Imerejea katika mashindano hayo baada ya kukosekana kwa miaka miwili, lakini licha ya kushinda mara tatu, ushindi wake wa mwisho ulikuwa 2007-08, na haijawahi kuvuka hatua ya robo fainali tangu ilipomaliza ikiwa mshindi wa pili 2010-11.

Opta inaichukulia United kama timu isiyopewa nafasi kubwa ya kushinda ubingwa Ulaya msimu huu, ikiwa na asilimia 3.7, lakini ina nafasi nzuri ya kufika robo fainali kwa asilimia 37.4 au hata nusu fainali kwa asilimia 19.1.

Inter Milan pia haiwezi kuondolewa katika kipute cha kusaka taji la Ulaya baada ya kufika fainali katika misimu miwili kati ya minne iliyopita na safari hii inapewa nafasi ya asilimia 8.3 ya kufika tena fainali, ingawa nafasi yake ya kubeba ubingwa ya asilimia 3.4 inaonyesha jinsi ilivyo nje ya kundi la wanaopewa nafasi.

Aston Villa ni timu ya 10 yenye uwezekano mkubwa wa kushinda Ligi ya Mabingwa msimu huu, lakini nafasi yake inakadiriwa kuwa asilimia 2.0 pekee. Mwanzo wake mbaya katika Ligi Kuu England baada ya kuondokewa na wachezaji wengi muhimu katika dirisha kubwa la usajili  unaonyesha kwamba inaweza kukutana na wakati mgumu katika mashindano makubwa zaidi ya Ulaya.

Timu zingine na nafasi zake ni Borussia Dortmund (1.8%), Roma (1.4%), Sporting CP (1.4%) na Club Brugge (1.0%) zinazopewa nafasi ya zaidi.


NAMB 04

HIZI WALA HAZITOBOI

Kuna tofauti kubwa ya ubora kati ya timu bora na dhaifu zaidi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini Opta iliziona kila moja ya timu 36 ikishinda mashindano angalau mara moja zikiwa mbali kubeba ubingwa. Shakhtar Donetsk, Slovan Bratislava na wageni wa kwanza kabisa katika mashindano hayo, Sabah ya Azerbaijan ndizo dhaifu zaidi katika mashindano. LASK na Feyenoord zote zipo huku AEK Athens ikipewa nafasi ya kuvitikisa vigogo.