Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazawa wawabana wageni Ligi Kuu

WAZAWA Pict


MSIMU wa Ligi Kuu Bara 2026-2027 umeanza kwa kasi kubwa katika idara ya ufungaji, huku washambuliaji wakionyesha makali mapema na kufanya kazi ya makipa kusaka clean sheet kuwa ngumu katika hatua hii ya mwanzo.


Baada ya mechi 20, jumla ya mabao 53 yamefungwa, wastani ukiwa mabao 2.65 kwa mchezo, jambo linaloonyesha kasi kubwa ya ufungaji ikilinganishwa na mwanzo wa msimu uliopita.


Kwa upande wa wazawa, Abdul Suleiman ‘Sopu’ wa Azam FC ndiye anayeongoza kwa mabao matatu, akifunga dhidi ya Polisi Tanzania, TRA United na Pamba Jiji.

Nyuma yake wapo Yusuph Mhilu na Richardson Ng’ondya wa Geita Gold, ambao kila mmoja amefunga mabao mawili, yote yakipatikana katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Wafungaji wengine wazawa walioanza msimu kwa bao moja ni Deogratius Mafie, Benno Ngassa, Yusuph Khamis, Anuary Jabir, Crispin Ngushi, Herbert Lukindo, Geofrey Julius, Kassim Haruna ‘Tiote’, Hashim Manyanya, William Thobias na Yahya Mbegu.

WAZA 03

Kwa upande wa wageni, Obrey Chirwa wa Geita Gold anaongoza akiwa na mabao matatu, akifunga bao moja dhidi ya Mbeya City kabla ya kutikisa nyavu mara mbili dhidi ya Kagera Sugar.

Jonathan Sowah wa Singida Black Stars, Maxi Mpia Nzengeli wa Yanga na Clatous Chama wa Simba wanafuata wakiwa na mabao mawili kila mmoja.

Kwa jumla, wageni 18 tofauti wamefunga mabao 23, huku wazawa 26 tofauti wakifunga mabao 30, hali inayoonyesha kuwa mchango wa wazawa katika ufungaji umeonekana zaidi katika hatua hii ya msimu.

Utofauti huo pia unaonyesha ushindani wa mapema katika kuwania ufalme wa ufungaji, huku Sopu na Chirwa wakianza kujitengenezea nafasi katika mbio hizo.

Si mabao pekee ambayo yameanza kupatikana kwa kasi, bali pia pasi za mwisho zimekuwa sehemu muhimu ya mwanzo huo wenye mvuto.

Libasse Gueye wa Simba ndiye anayeongoza kwa asisti nne, akitoa pasi mbili zilizozaa mabao dhidi ya Kagera Sugar, kabla ya kufanya hivyo pia katika michezo dhidi ya Pamba Jiji na Singida Black Stars.

Housseine Zakouani na Chadrack Boka wa Yanga, Jeancy Mboma wa Singida Black Stars na Vicent Aboubakar wa Geita Gold wanafuata wakiwa na asisti mbili kila mmoja.

WAZA 01

MAKIPA WANATESEKA

Wakati washambuliaji wakifurahia mwanzo mzuri, hali ni tofauti kwa makipa ambao wamekuwa na kazi ngumu katika kulinda nyavu zao.

Licha ya kwamba hakuna mchezo uliomalizika bila bao katika mechi hizo 20, jumla ya clean sheet nane zimepatikana, zikigawanywa na makipa nane tofauti.

Frank Faustine wa Geita Gold, Metacha Mnata (Singida Black Stars), Mussa Malika (Mashujaa), Mahamadou Tanja Kassali (Simba), Ibrahim Parapanda (Fountain Gate), Suleiman Said Abraham (Namungo), Toba Kutisha (Mbeya City) na Christopher Nyakanda (Polisi Tanzania) kila mmoja ameweka lango lake salama katika mchezo mmoja.

WAZA 02

Kinara wa msimu uliopita, Djigui Diarra wa Yanga aliyemaliza na clean sheet 18, mechi mbili za kwanza kabla ya jana, alikuwa ameruhusu bao dhidi ya Namungo na Coastal Union, hivyo bado anajitafuta.

Hii inaifanya vita ya makipa kuwa ya aina yake kwani si tu kuokoa mabao, bali pia kusaka mchezo mmoja ambao wanaweza kumaliza bila kuruhusu bao.

Kwa kasi ya mabao 2.65 kwa mchezo, kazi hiyo imekuwa ngumu zaidi, huku kila kosa la safu ya ulinzi likionekana kuwa na nafasi kubwa ya kugeuka kuwa bao.

WAZA 05

TOFAUTI NA MSIMU ULIOPITA

Moto ulioanza msimu huu unaonekana wazi zaidi unapolinganishwa na msimu uliopita.

Baada ya mechi 20 za msimu uliopita, yalikuwa yamefungwa mabao 31 kupitia wafungaji 29 tofauti, wastani ukiwa bao 1.55 kwa mchezo.

Kwa sasa, baada ya idadi hiyo hiyo ya mechi, zimefungwa 53, wastani ukiwa 2.65 kwa mchezo.

Hiyo ni ongezeko la mabao 22, huku wastani wa ufungaji ukipanda kwa 1.10 bao kwa mchezo.

Msimu uliopita, Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC na Paul Peter wa JKT Tanzania walikuwa vinara wa ufungaji baada ya kila mmoja kufunga mabao mawili katika mechi 20 za mwanzo.

Msimu huu, Sopu na Chirwa tayari wamefika mabao matatu, huku washambuliaji wengine wakifuatia kwa kasi.

WAZA 03 (1)

WAKUBWA KAZI IPO

Msimu uliopita katika mechi tatu za kwanza, Simba ambayo sasa imeshinda mechi tatu na kukusanya pointi tisa, imekirudia ilichofanya lakini kiwango kimeshuka.

Simba safari hii licha ya kukusanya pointi tisa kwa kushinda mechi tatu za kwanza, lakini imefunga mabao machache ambayo ni sita, huku ikiruhusu mawili, ina clean sheet moja.

Msimu uliopita wakati kama huu ilikuwa imefunga mabao manane, ikiwa na clean sheet mbili, huku ikiruhusu bao moja pekee.

Kwa upande wa Yanga ambayo jana ilishuka dimbani kucheza na JKT Tanzania ikiwa ni mechi ya tatu, lakini zile mbili za kwanza ilikuwa vizuri kwenye ufungaji ikipachika mabao saba, lakini ulinzi una tatizo ikiruhusu mabao mawili, huku moja kila mechi.

Katika kusaka pointi, safari hii Yanga imekuza kiwango kwani msimu uliopita mechi mbili za kwanza ilikuwa na pointi nne ikishinda 3-0 dhidi ya Yanga na 0-0 mbele ya Mbeya City. Mechi hizo Yanga ilivuna clean sheet mbili, hivi sasa imezikosa.

Kwa Azam iliyomaliza nafasi ya tatu msimu uliopita, mechi tatu za kwanza ilikusanya pointi tano, lakini sasa inazo saba, hata hivyo, suala la kujilinda ni tatizo.

Azam haina clean sheet, msimu uliopita mechi tatu za kwanza ilikuwa nayo moja angalau kulinganisha na sasa, hata hivyo bado kuna tatizo eneo hilo.

Timu hiyo ilianza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City, kisha ikatoka 1-1 dhidi ya JKT Tanzania na Namungo ikipata matokeo ya aina hiyo.

Safari hii, Azam imeanza na 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania, ikashinda 2-1 mbele ya TRA United na Pamba Jiji.