Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Machozi tofauti kwa Messi na Lamine Jumapili

PAZIA Pict


UPANDE mmoja hautakuwa na machozi mengi. Upande mwingine unaweza kuwa na machozi mengi. Lionel Messi atashuka katika basi akiingia katika uwanja wa MetLife pale New Jersey huku nyuma yake akiwa amesimama ‘baunsa’ wake ambaye ni mchezaji mwenzake, Rodrigo de Paul.


Hisia moyoni, akili kichwani. Upande mwingine Rodri atashuka katika basi la Hispania na kuingia katika uwanja wa MetLife nyuma yake akisindikizwa na kinda wa timu hiyo, Lamine Yamal. Maisha yameenda kasi kwake.


Lamine ndiye alama ya Hispania kwa sasa. Hakuna maajabu makubwa aliyoyafanya lakini ndio alama ya Hispania kwa sura ya biashara na mvuto. Rodri ndiye ambaye anaonekana kuwa baba mwenye nyumba ya Hispania.

Hakutakuwa na machozi mengi kama Waargentina wakipoteza pambano hili. Watalia, ndio, lakini sio sana. Miaka minne iliyopita kimiujiza walifika katika fainali za Qatar na wakatwaa kombe. Waliwapiga Wafaransa kwa penalti.

PAZ 01

Mwaka huu sikuwapa nafasi. Nisiwe mnafiki. Nilidhani miguu ingemsaliti Lionel Messi. Nilidhani miguu ingewasaliti pia akina Nicolas Otamendi huku Angel Di Maria akiwa ametundika daluga. Sikuona kizazi cha kusisimua cha Waargentina lakini wamefika fainali.

Wailidhaniwa kwamba walikuwa wametengenezewa njia nyepesi ya kufika fainali lakini nusu fainali walikutana na Waingereza na wakatuonyesha kwamba hawapendelewi. Mpira walioupiga katika kipindi cha pili ulitoka katika sayari nyingine.

Hakutakuwa na machozi mengi wakipoteza pambano hili kwa sababu tayari Messi na wachezaji wengi wa kikosi hiki wana medali za kombe la dunia. Zile ambazo walizivaa usiku ule pale Doha.

PAZ 02

Tatizo litakuwa kwa Hispania. Machozi yanaweza kuwa mengi. Hakuna mchezaji ambaye aliwahi kutwaa kombe la dunia miaka 16 iliyopita katika kile kikosi ambacho kiliutwaa ubingwa pale Soweto Johanesburg. Hakuna hata mmoja.

Kila mchezaji wa Hispania anautaka ubingwa wake wa kwanza wa kombe la dunia. Wakiukosa watatoa machozi mengi. Namna walivyoicheza hii michuano wameicheza kikubwa. Walianza kama vile wangekuwa timu ya kawaida wakati walipotoka Suluhu na Cape Verde katika mechi ya kwanza.

Taratibu wakainyoosha fomu yao. Wakaicha dunia mdomo wazi kwa namna walivyocheza pambano lao na Wafaransa. Namna ambavyo akina Michael Olise, Kylian Mbappe na Ousmane Dembele walivyoitisha dunia, usingeamini kwamba walipigiwa ‘tiktak’ nyingi na hawakuonekana uwanjani pale Dallas.

PAZ 03

Kwa taifa zima nje ya akina Lamine kutakuwa na machozi lakini sio mengi. Kama wakichukua huu utakuwa ubingwa wao wa pili. Kama wasipochukua bado walishaingia katika historia ya kuchukua taji hili. Ni miongoni mwa nchi nane ambazo zimewahi kutwaa kombe la dunia.

Kwa Waargentina wana fursa fulani mkononi. Sikufikiria kama ingekuwa mapema hivi. Kama wakichukua taji hili basi itakuwa mara yao ya nne. Walitwaa 1978 wakiwa na Super Mario Kempes, wakatwaa mwaka 1986 wakiwa na Diego Maradona, kisha wakatwaa miaka minne iliyopita wakiwa na Messi pale Doha.

Wakitwaa hili itakuwa mara ya nyingi na msukumo unakuja zaidi pale unapogundua kwamba kama wakitwaa basi watakuwa wamezifikia Italia na Ujerumani katika nafasi ya pili ya timu ambazo zimetwaa kombe la dunia mara nyingi zaidi nyuma ya Brazil ambayo imetwaa mara tano.

Waitaliano na Wajerumani wamezubaa mpaka Argentina wanaweza kuwafikia. Lakini hapo hapo itakuwa timu ya pili kufanikiwa kutetea kombe la dunia baada ya Italia kufanya hivyo mwaka 1934 kisha mwaka 1938. Historia haisahau kitu.

PAZ 04

Argentina ikishinda pia itatuletea maajabu mengine kuhusu Messi. Ghafla anaweza kuwa mwanasoka bora wa dunia. Atakuwa mwanasoka bora wa dunia wa kimaajabu. Mwanasoka bora wa dunia mwenye umri mkubwa zaidi katika historia. Miaka 39.

Anaweza kuwa mwanasoka bora wa kwanza wa dunia kutoka Ligi kuu ya Marekani. Itashangaza. Wanasoka bora wa dunia huwa hawatoki bara lolote zaidi ya Ulaya. Ghafla taji la ulaya halitakuwa na maana yoyote kwa akina Ousmane Dembele kwa maana ya kuwa chanzo cha mafanikio ya kutwaa tuzo hiyo.

Upande wa Messi pia kama akitwaa taji hili atakuwa amewaacha Waargentina katika mkanganyiko mkubwa. Nani zaidi, Messi au Diego Maradona. Waargentina wanamuabudu Maradona. Hata Messi mwenyewe anamuabudu Maradona. Tatizo namba hazisemi uongo.

Messi tayari ameipeleka Argentina katika fainali tatu za kombe la dunia. Mwaka 2014 pale Brazil, kisha miaka minne iliyopita pale Doha na sasa hapa New York. Maradona aliipeleka Argentina katika fainali mbili tu za kombe la dunia. Mwaka 1986 pale Mexico ambako walitwaa, na mwaka 1990 pale Italia ambako walipoteza katika fainali.

Kama Messi akitwaa hili taji ina maana atakuwa ametwaa mataji mawili wakati Maradona atakuwa ametwaa taji moja. Wahafidhina wengi watakwambia kwamba Maradona ni bora zaidi ya Messi lakini Kundi kubwa la watu litakwambia kwamba Messi ni zaidi ya Maradona.

Lakini kama Hispania ikishinda tuzo inaweza kwenda kwa mara ya pili kwa mchezaji anayeitwa Rodri. Ndiye injini ya Hispania. Sawa, hakuchukua ubingwa wa ligi kuu ya England na timu yake Manchester City lakini ghafla ameibuka kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye nafasi ya kutwaa tuzo yenyewe.

Na ana nafasi hasa. Uwanjani naiona Hispania kuwa tishio. Kama wakirudia kile walichowafanyia Ufaransa basi taji linaweza kuwa lao. Kama Waargentina wakiutafuta mpira kwa tochi basi taji linaweza kuwa lao.

Tatizo Waargentina nao sio wajinga. Wana uwezo mkubwa wa kuipindua mechi kimaajabu tu wakiongozwa na mchawi Messi. Wachezaji wao wanajituma hasa. Wao na kocha wao watakuwa wamejiandaa na ubatizo wa moto ambao Wafaransa walikabiliana nao pale Dallas.

Mechi dhidi ya England haikuwa nyepesi kama ambavyo fainali yao na Wafaransa haikuwa nyepesi pale Doha. Hata hivyo walikuja na majibu mazuri tu. Sijui kama watakuwa na majibu mazuri dhidi ya Hispania ambayo mpira wake ndio unaotawala dunia kwa sasa. Sijui.