Luis Figo na rekodi yake Bab’kubwa

Muktasari:

Mara nyingi mashabiki wa kandanda na vyombo vya habari vya Ureno huzungumzia yatima au kiumbe ambaye mchango wake katika mchezo huu ni mkubwa, lakini hautambuliki kama inavyostahiki.

Mara nyingi mashabiki wa kandanda na vyombo vya habari vya Ureno huzungumzia yatima au kiumbe ambaye mchango wake katika mchezo huu ni mkubwa, lakini hautambuliki kama inavyostahiki.

Huyu anayelezewa hivyo ni Luís Filipe Madeira Caeiro Figo aliyecheza kama kiungo au winga wa kulia na kuchangia pakubwa katika mafanikio ya timu nyingi na timu za taifa za Hispania .

Kwanza alikuwemo katika kikosi cha watoto wa chini ya miaka 16 mwaka 1988 na 89, mwaka 1989 aliitwa katika kikosi cha vijana wa chini ya miaka 17.

Baadaye alikuwa na kikosi cha vijana wa chini ya miaka 18 na kutoka 1991 hadi 1994 alikuwa na timu ya taifa ya vijana wa chini ya miaka 21.

Wakati akiwa katika kikosi cha vijana 21 pia aliichezea timu ya taifa kuanzia 1991 na kutokesekana katika timu hio hadi mwaka 2006.

Hispania kila ilipocheza suala lilikuwa wachezaji gani 10 wataungana na Figo aliyeteremka uwanjani na timu hio mara 127.

Hii ilikuwa rekodi katika nchi hio mpaka karibuni ilipovunjwa na Christian Ronaldo.

Figo pia aliacha rekodi nzuri kwa vilabu vyote vya vijana na baadaye timu kubwa alizochezea.

Baada ya kulisakata kabumbu na vikundi vya watoto Figo ambaye sasa ana miaka 49 alijiunga na klabu ya Sporting.

Baadaye alikuwa na vilabu vya Barcelona na Real Madrid na baada ya hapo alikuwa na Inter Milan ya Italia.

Tigo alisifika kwa kuwa mchezaji mwepesi na mwenye ubunifu, lakini zaidi kwa kuwa so mtu anayekata tamaa mpaka inapopulizwa filimbi ya mwisho ya mchezo.

Alipata heshima ya kuwa mchezaji bora wa Ulaya mwaka 2000 na kuchaguliwa na Shrikisho la Kimataifa la Kandanda (FIFA) kuwa mchezaji bora wa dunia wa mwaka 2001.

Alipoachana na Barcelona na kujiunga na mahasimu wao wakubwa Real Madrid mwaka 2000 kwa kitita cha Euro 62 milioni alisema alifanya hivyo sio pesa zilizomvutia na pesa, bali kutaka kuonyesha mchezo wa kandanda ni wa kujenga urafiki na sio kukuza uhasama.

Aliichezea Hispania katika fainali za Kombe la Ulaya mara tatu na Kombe la Dunia mara mbili.

Figo ambaye ndio mtoto pekee wa António Caeiro Figo na Maria Joana Pestana Madeira ika mazingira ya kimasikini.

Timu yake ya kwanza ya mitaani ilikuwa Cova da Piedade, ya mji mdogo wa Almada.

Baadaye aliichezea klabu ya U.F.C. Os Pastilhas kabla ya kujiunga na chuo cha soka cha Sporting Clube de Portugal akiwa na miaka 12.

Wakati aking’ara mwaka 1995 aligombaniwa na timu nyingi kubwa za Ulaya. Miongoni mwao ni Juventus, Parma na Manchester City na hapo ndipo alipoamua kujiunga na Barcelona.

Figo amekuwa akisema alisikitishwa sana siku alipokwenda Barcelona kwa mara ya kwanza na kuona mabango yenye maandishi yaliyoandikwa Msaliti, Malaya na Askari wa Kukodiwa.

Vile vile alirushiwa chupa, mayai viza na machungwa mabovu.

‘’Nilisikitishwa sana. Sikutegemea watu nilioishi nao vizuri kunipa majina kama hayo’’, alisema.

Katika mchezo ule Figo ambaye ni mpigaji kona mzuri siku ile hakufanya hivyo kwa kuhofia kuumizwa kwa kupigwa chuma au mawe.

Figo alijiuzulu kucheza kandanda tarehe 16 Mei, 2009, siku ambayo Inter Milan alipochukua ubingwa wa Italia.

Siku ile Figo alisema; “ Ninaacha kucheza kandanda, lakini sio mapenzi yangu kwa klabu ya Inter Mlan’’.

Aliahidi kutumia ujuzi na uzoefu wake kuisaidia klabu hio, hasa kwa kuwaendeleza vijana chipukizi.

Tigo siku hizi hutumika kwa matangazo ya kuendeleza mchezo wa kandanda, kutangaza kampuni za biashara na ya elimu kwao Ureno na nchi nyengine za Ulaya.

Vile vile alitumika kuitangaza timu ya Iran katika mashindano ya Kombe la Dunia ya 2018.

Mnamo tarehe28 Januari Figo alitangaza nia yake ya kugombea kiti cha Rais wa FIFA kuchukua nafasi ya Sepp Blatter, lakini alijitoa njiani kwa kudai kwepo rafu nyngi katika kugombea nafasi hio.

Siku hizi anaendesha biashara ndogo ndogo, ikiwa pamoja na kumiliki klabu moja maarufu ya pombe katika mji wa Algarve.

Vile vile ni balozi wa kampeni ya kimataifa ya kupambana na maradhi ya kifua kikuu.

Vile vile Figo ambaye anazungumza vizuri lugha tano – Kihispania, Kiingereza, Kireno na Kitaliana - ni balozi wa klabu ya Inter Milan katika Bara la Ulaya.

Siku hizi hukaribishwa na vituo vya radio na runinga kufanya uchambuzi wa michezo.