Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LA LIGA inaanza leo, macho kwenye skrinii!

Muktasari:

  • Hawa hapa wachezaji saba muhimu wasiokuwa na majina makubwa ambao unapaswa kuwafuatilia.

MADRID, HISPANIA;Kabla ya kurejea kwa La Liga leo, Agosti 15, 2026, kuna wachezaji tisa ambao inatarajiwa mashabiki kutoka pande nne za dunia watakuwa wakiwafuatilia kwa karibu katika msimu wa 2026/27.

Hawa hapa wachezaji saba muhimu wasiokuwa na majina makubwa ambao unapaswa kuwafuatilia.


YAN DIOMANDE (REAL MADRID)

Msimu mmoja wa Yan Diomande akiwa RB Leipzig katika Bundesliga ulikuwa wa kuvutia sana, hali iliyomfanya ashinde tuzo ya Rookie of the Season kutokana na kiwango chake bora.

Takwimu zake kuu zilikuwa mabao 12 na asisti nane, huku Lamine Yamal wa Barcelona akiwa mchezaji mwingine pekee mwenye umri chini ya miaka 24 aliyefikisha angalau michango 20 ya mabao katika ligi tano kubwa za Ulaya msimu uliopita, akiwa na mabao 11 na asisti 11.

Kiwango hicho kilimsaidia Diomande kulamba dili la uhamisho mnono kwenda Real Madrid, ikiwa ni chini ya miezi 17 tangu alipocheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa dhidi ya Real Madrid akiwa na Leganes kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu. Hata hivyo, uwezo wake haupaswi kupimwa kwa idadi ya mabao na asisti pekee.

Alikuwa kero kubwa kwa mabeki kutokana na ujasiri na uvumilivu wake anapokuwa na mpira, akifanya majaribio ya kupiga chenga mara 7.7 kwa kila dakika 90, idadi iliyokuwa kubwa zaidi Bundesliga kwa wachezaji waliocheza zaidi ya dakika 900.

Pia alikuwa na kiwango cha mafanikio cha asilimia 55.4 katika chenga hizo, kiwango cha nne kwa ubora miongoni mwa wachezaji 68 waliokuwa na wastani wa angalau chenga 2.0 kwa kila dakika 90.

Uwezo wake wa kutembea na mpira pia ulikuwa sehemu muhimu ya tishio lake la kushambulia. Alikuwa na takriban mikimbio 52 kwa kila mchezo kukokota mpira uliomalizika kwa shuti au kutengeneza nafasi, jambo lililomuweka nafasi ya tano kwenye ligi hiyo.

Uzuri wa kipaji cha Diomande akiwa na mpira ni ana uwezo mzuri miguu yote, anaweza kucheza katika maeneo yenye msongamano na pia kukimbia umbali mrefu, huku akiwa mpigaji pasi mzuri.


ROBBIE URE (SEVILLA)

Straika wa kimataifa wa Scotland aliyetua Sevilla mwenye miaka 22, aliyelelewa Rangers kabla ya kuondoka Mei 2023. Alitumia karibu miaka miwili Anderlecht, ambako kwa kiasi kikubwa alikuwa akicheza timu ya akiba. Machi 2025 alijiunga na Sirius ya Sweden inayoshiriki Allsvenskan ambako msimu wake wa kwanza alifunga mabao 11 ya ligi katika mechi 30, idadi iliyozidiwa na wachezaji watano pekee.

Lakini mwaka 2026 kiwango chake kilipanda zaidi. Kabla ya kuondoka Sirius, Ure alikuwa amefunga mabao 15 katika mechi 15, mabao matatu zaidi ya mchezaji mwingine yeyote katika ligi hiyo. Ure ni mshambuliaji kamili, ni mrefu, ana kasi nzuri na uwezo wa kupiga kwa miguu yote. Anaweza kushuka nyuma, kukimbia nyuma ya mabeki au kusubiri nafasi ndani ya eneo la hatari kama mshambuliaji aina ya ‘poacher’.

Analinganishwa na Benjamin Sesko wa Manchester United. Sevilla imekuwa ikikaribia eneo la kushuka daraja katika misimu mitatu iliyopita, na baada ya kufanya maboresho makubwa ya kikosi, Ure anatarajiwa kuwa sura ya timu mpya.


ANTHONY GORDON (BARCELONA)

Anthony Gordon alifurahia msimu wake bora zaidi wa kufunga mabao 2025/26, akifunga mabao 17 katika mashindano yote akiwa Newcastle United.

Pamoja na hilo, uhamisho wake wa euro milioni 80 kwenda Barcelona uliwashangaza wengi. Hata hivyo, hilo halimaanishi Gordon hana uwezo wa kufanikiwa Hispania.

Kama alivyoonyesha wakati England ilipofika nusu fainali ya Kombe la Dunia ambako alifunga bao pekee la England dhidi ya Argentina ana sifa zinazoweza kuzisumbua safu nyingi za ulinzi.

Akiwa miongoni mwa wachezaji 10 wenye kasi zaidi Ligi Kuu England msimu uliopita, Gordon alifikisha kasi ya juu ya kilomita 36.3 kwa saa.

Miongoni mwa wachezaji waliocheza angalau dakika 1,500 katika ligi hiyo 2025/26, hakuna aliyekuwa na wastani mzuri wa kasi kwa mchezo kuliko Gordon, akiwa na 25.8. Pia ni Yankuba Minteh pekee wa Brighton aliyekuwa na umbali mkubwa zaidi wa kukimbia kwa kasi kwa dakika 90 kuliko Gordon, ambaye alikuwa na mita 475.3.

Katika misimu yake mitatu ya mwisho Newcastle, Gordon alihusika katika mabao 59 akifuga 38 na asisti 26, wastani wa mchango mmoja kila dakika 164.

Takwimu hizo zinaweza kuimarika akiwa Barcelona, timu yenye uwezo mkubwa wa kushambulia, lakini mengi yatategemea muda wa kucheza atakaoupata chini ya kocha Hansi Flick.

Kiwango chake kwenye Ligi ya Mabingwa msimu uliopita kilikuwa cha kuvutia, akifunga mabao 10, idadi kubwa zaidi kufungwa na mchezaji Mwingereza katika msimu mmoja wa mashindano hayo akiwa na klabu ya England, ikiwamo enzi ya European Cup.


GUSTAVO PUERTA (RACING SANTANDER)

Racing Santander imerejea La Liga msimu huu baada ya miaka 14, na raia wa Colombia, Gustavo Puerta, alitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha inarudi kwenye ligi kuu. Puerta alipaswa kujiunga moja kwa moja na Hull City msimu uliopita, lakini dili hilo likavunjika kutokana na zuio la usajili lililowekwa dhidi ya Hull. Baadaye alijiunga na Racing Septemba 1, na ukawa usajili bora sana.

Miongoni mwa viungo waliocheza zaidi ya dakika 900, alikuwa wa nane kwa asilimia ya ukamilishaji wa pasi katika nusu ya uwanja ya wapinzani, akiwa na asilimia 87.3, na wa sita kwa kurejesha umiliki wa mpira kwa dakika 90 akiwa na wastani wa 6.4.

Lakini, kilichovutia zaidi ni uwezo wake wa kuusogeza mpira mbele. Alikuwa na wastani wa mbio 4.1 za kuusogeza mpira mbele kwa zaidi ya mita 10 kwa dakika 90, ikiwa ni idadi ya pili kwa wachezaji waliotajwa kuwa viungo wa kati, ulinzi na ushambuliaji waliocheza zaidi ya dakika 900.

Pia alikuwa wa tatu katika kundi hilo kwa mbio za kuusogeza mpira mbele kwa zaidi ya mita tano, akiwa na wastani wa 8.6 kwa dakika 90. Puerta baadaye aliendelea kuvutia akiwa na Colombia kwenye Kombe la Dunia 2026. Iwapo Racing itabaki La Liga, Puerta huenda akawa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi katika mafanikio hayo.


YEREMAY HERNANDEZ (DEPORTIVO)

Msimu bora unamngoja Yeremay Hernandez mwenye umri wa miaka 23, aliyejijengea jina baada ya kufanya vizuri katika Ligi Daraja la Pili Hispania (Segunda) kwa misimu miwili iliyopita, lakini huu utakuwa wake wa kwanza La Liga. Ni winga wa kushoto mwenye mwili mdogo lakini mwenye kasi na nguvu. Yeremay ana uwezo wa kuwafanya mashabiki wasimame kutokana na uharaka na ustadi wake, huku akiwa pia chanzo cha mabao na ubunifu kwa Deportivo Coruna.

Tangu Deportivo ipande kutoka daraja la tatu 2024, Yeremay amekuwa wa nne kwa michango ya mabao akiwa na 41 katika Segunda. Wachezaji watatu waliomtangulia wamecheza angalau dakika 500 zaidi yake. Kinachovutia zaidi ni mtindo wake wa moja kwa moja na wa ujasiri.

Katika misimu miwili iliyopita Segunda alikuwa na wastani wa majaribio 6.7 ya chenga kwa kila dakika 90 ikiwa ni idadi kubwa zaidi miongoni mwa mastaa waliocheza zaidi ya dakika 1,500.

Pia alikuwa mchezaji anayeongoza kwa michango ya mabao baada ya kukokota mpira, akiwa na 17.

Alikuwa amefikia kiwango cha kuondoka Segunda na huenda angeondoka Deportivo kama timu hiyo isingepanda daraja.


CALA (ESPANYOL)

Alex Calatrava, anayejulikana kama Cala amevumilia kusubiri nafasi ya kunza katika soka la kiwango cha juu. Ingawa aliwahi kutumia miaka kadhaa katika akademi ya La Masia ya Barcelona akiwa mtoto, Cala hakupitia mfumo wa kawaida wa klabu kubwa.

Alikuwa mmoja wa wachezaji wawili pekee waliocheza zaidi ya dakika 900 na kuwa na wastani wa angalau mashuti 3.0 na nafasi 1.7 zilizotengenezwa katika mchezo wa wazi kwa dakika 90 Segunda msimu uliopita.

Michango yake 23 ya mabao akifunga 15 na asisti nane ilizidiwa na wachezaji sita pekee, ambao baadhi walikuwa washambuliaji wa kati. Mzaliwa wa Catalonia, sasa amerejea Barcelona akiwa na Espanyol na alikuwa usajili wa kwanza.


JAVI RODRIGUEZ (CELTA VIGO)

Javi Rodriguez kwa muda mrefu, Celta Vigo haikuwa na matarajio makubwa kwake. Alicheza karibu mechi zote za La Liga za timu ya wakubwa msimu wa 2024/25 na akacheza mara 33 msimu uliopita wakati ilipomaliza ndani ya saba bora kwa misimu miwili mfululizo.

Katika mfumo wa Celta wenye mabeki watatu, Rodriguez amejitengenezea nafasi ya beki wa kati upande wa kulia na kuwa mmoja wa mabeki wanaokuja juu zaidi Hispania.

Bado kuna maswali kuhusu uwezo wake wa kimwili, kwa mfano siyo mzuri sana kwenye mipira ya juu, lakini akiwa na mpira hakuna shaka kuhusu ubora wake.

Ana utulivu na hata umaridadi akiwa nao na ni msambazaji mzuri, hasa anapokuwa katika maeneo ya juu zaidi ya uwanja.

Kiwango chake cha asilimia 80.9 cha pasi zilizofika theluthi ya mwisho ya uwanja msimu uliopita kilikuwa cha tano kwa ubora miongoni mwa mabeki wa kati waliocheza zaidi ya dakika 900.

Wakati huohuo, ni wachezaji sita pekee waliokuwa na wastani bora kuliko pasi zake 9.2 za kuvunja mistari kwa dakika 90. Akiendelea kupiga hatua, uhamisho mkubwa unaweza kuwa kwenye kadi mwakani.


CHUPE (MALAGA)

Carlos Ruiz Rubio maarufu Chupe mwenye umri wa miaka 21 huenda asiwe na kasi kubwa zaidi, lakini vinginevyo ni mshambuliaji wa kati mwenye uwezo mzuri katika maeneo mbalimbali.

Ana uwezo wa kutumia miguu yote, ni mzuri kwenye mipira ya juu, ana ufundi na ni mfungaji bora.

Alikuwa muhimu sana Malaga msimu uliopita. Katika mechi 45 za ligi, ikiwamo hatua ya mchujo alifunga mabao 25 na kutengeneza mengine sita.

Katika msimu wa kawaida, mabao yake 24 yalizidiwa na Sergio Arribas wa Almeria pekee aliyefunga 25. Namna Chupe atakavyozoea La Liga itakuwa na umuhimu mkubwa katika nafasi ya Malaga kubaki ligi kuu.


BUBA SANGARE (ELCHE)

Beki mwenye umri wa miaka 19, Buba Sangare, alitumia nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo kutoka Roma na akaacha nafasi vizuri. Uhamisho wake ulifanywa kuwa wa kudumu msimu huu kwa takribani Euro milioni 4.5, kiasi kikubwa kwa Elche.

Akitumika kama beki wa kati upande wa kulia au wing-back katika mfumo wa mabeki watatu, Sangare alivutia kutokana na utulivu akiwa na mpira na mtindo wake wa ulinzi wa kushambulia.

Uwezo wake wa kutumia mpira ulimfanya kuwa chaguo zuri katika nafasi zote mbili. Alikuwa na wastani wa majaribio 3.0 ya chenga kwa dakika 90, idadi iliyomuweka nafasi ya sita miongoni mwa mabeki kuanzia Februari 2, kwa waliocheza zaidi ya dakika 350. Wakati huo huo, alikuwa pia na uwezo mkubwa wa kiulinzi.