Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuna nini kwa Mzize, Fei Toto?

NONDO Pict


SOKA la kisasa lina mabadiliko makubwa ikichangiwa zaidi na ukuaji wa klabu zetu na kuifanya Ligi yetu kuwa kivutio cha makocha wengi wanaotaka kukua kitaaluma kutamani kupata nafasi ya kufundisha hususani klabu zenye wafuasi wengi za Simba na Yanga.


Hii ni kwa sababu klabu hizo zimekuwa na ushindani katika michuano ya Afrika na hii haiishii kwa makocha tu, inafanya wachezaji pamoja na wasimamizi wao kutamani kutumia klabu zetu kama daraja la kufikia malengo yao kiuchezaji na maisha kwa ujumla.


Hii imeleta neema pia kwa wazawa kuhitajika na klabu kubwa barani Afrika kama ambavyo baadhi ya wachezaji wa kigeni wamekuwa wakija na kutumia klabu zetu kukua kiuchumi na kiuchezaji.

Kwani tumewashuhudia wageni kadhaa wakipata ofa za kuhitajika na kusajiliwa na klabu hizo za nje, huku klabu zetu zikilazimika kuwauza hata kama hazitaki ila imekua tofauti kwa wazawa wanapohitajika kumekuwa na ugumu sana kuondoka.

NOND 01

Kwa mifano ya hivi karibuni kulikuwa na sakata la Clement Mzize kutakiwa nje, lakini dili likafia njiani kutokana na mabosi wa klabu hiyo kuchomoa kabla ya kuibuka tena kwa ishu ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye amekuwa akihusishwa na klabu mbalimbali za nje ya nchi.

Hata hivyo, hadi sasa haijafahamika dili hilo limeishia wapi au ndo imekuwa kama lile ya Mzize, lakini ni ajabu kwa nyota wa kigeni waliuzwa fasta nje ya nchi akiwamo Fiston Mayele, Pape Ousmane Sakho au Stephane Aziz Ki ambao dili zao zilijadiliwa na kuamuliwa mara moja.

Ni sawa tu na ilivyowahi kushuhudiwa kwa Jose Luis Miquissone na Clatous Chama au Heritier Makambo au Tuisila Kisinda walipouzwa na Simba na Yanga miaka kadhaa nyuma.

NOND 02

Ukiangalia kwa mifano hiyo na mingine mingi unaweza kulaumu viongozi kulingana na unavyoona kwa kudhani kama kuna jambo linalowafanya viongozi kuwa wepesi kuwaruhusu nyota wa kigeni kwenda nje na kuwabania wazawa.

Lakini hapo hapo unaweza kubadilisha upepo na kuwatupia lawama wachezaji wenyewe ambao wamekuwa wakiogopa kuondoka kulinganisha na wageni wanapohitajika na klabu za nje ya Tanzania.

NOND 03

Wanaolaumu viongozi wanashindwa kuangalia miradi ya klabu zetu kuhusu timu ni kushindana na kupata heshima au kufanya biashara ya wachezaji?

Kama mradi ni kutengeneza timu ya ushindani na kiongozi ndio msimamizi anawezaje kumuachia mchezaji mzuri aondoke bila kufanya jitihada zozote za kumbakiza ili kusimamia mradi, kazi aliyopewa na wanachama au wamiliki wa klabu?

Ikiwa sio timu ya wanachama, yeye kuzuia biashara yenye athari kwa timu ni kutimiza majukumu yake na hii faida wanaipata kwa wazawa kutokana na aina ya mikataba inayoingiwa.

Na hii inachangiwa zaidi kutokana na uzoefu duni wa wanaosimamia wachezaji, lakini pia hali za wachezaji na familia zao kiuchumi imekuwa ndio fimbo na udhaifu unaotumika katika mikataba.

NOND 04

Wakati mwingine hata ikionekana mameneja kusimamia zaidi maslahi ya wachezaji kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwagombanisha mchezaji na msimamizi husika na kufikia hata kutishia kutowasajili ikiwa hawataachana nao.

Shinikizo hilo linaelekeza hadi wachezaji hao wasimamiwe na watu wengine. Hii imeondoa nguvu ya wasimamizi wa awali kupambana katika vipengele hasa vya kumwezesha mchezaji kuondoka kwa kuuzwa au kununua mkataba wake uliobaki. Wasimamizi wengi wamekuwa waoga kutokana na wachezaji kuhitaji pesa tu, ili kukomboa familia zao wakati mwingine huwaona wasimamizi kama vikwazo, hivyo hukubaliana na viongozi na kuwazunguka simamizi wao au kuwakana kabisa ili kufanikisha dili zao za usajili na kuikomboa familia kubwa inayomtegemea bila kuangalia kesho yake kuhusu kipaji chake.

Wasimamizi wasiokubalika na viongozi ambao huonekana kama vikwazo wanaondolewa katika mfumo na kubaki wale ambao wanawatumikia viongozi na sio mchezaji na hapa ndipo naweza kusema hizi lawama za wachezaji kushindwa kwenda nje wanapohitajika, ni kuwaonea tu!

Kiukweli bado tuna safari ya kubadilisha mazingatio katika vipengele vya mkataba ili kutoa unafuu kwa wachezaji kwani hii kwa kiasi inachangia na kuwakwamisha kutoka bila wengine kujua na kuishia kuwalaumu kwa sababu ya mashinikizo wanayokutana nayo kutoka kwa viongozi.