Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Klabu hazitaki mageuzi, zinaendeleza mazoea yanayoharibu soka letu

ZENGWE Pict


Mechi ya Ligi Kuu Bara ya mkondo wa pili msimu uliopita kati ya vigogo wa Kariakoo, Yanga na Simba ilitakiwa ichezwe Machi 8 lakini hila na njama za klabu hizo kongwe nchini zikasababisha iahirishwe kiholela.


Matatizo yaliyosababisha kuahirishwa kwa mechi hiyo, ambayo mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) alidokeza yangesababisha moja ya timu hizo kushushwa daraja, hayakushughulikiwa na badala yake ikatangazwa tarehe mpya; Juni 15.


Kuanzia hapo mgogoro ukawa mkubwa baina ya Yanga, Shirikisho la Soka (TFF) na Bodi ya Ligi na kusababisha hali ya kuumbuana kuhusu kilichosababisha mechi kuahirishwa hadi kuweka hadharani mawasiliano baina ya klabu hiyo na TFF yanayoonyesha kudaiana.

Msimamo wa Yanga ukawa hawatacheza mechi ya tarehe mpya kwa kuwa walikuwa wamealikwa Rwanda, huku Simba wakisema wako tayari kucheza Juni 15.

ZENG 01

Ni busara tu za Rais Samia Suluhu Hassan ndizo zilizonusuru mechi hiyo kuchezwa baada ya TFF, TPLB na Yanga kutoweza kukaa kimya kufikia muafaka.

Lakini muafaka ambao Rais Samia aliuweka na ambao haujawahi kuwekwa bayana, uliondoka na Steven Mguto, aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Ligi na Almasi Kasongo, aliyekuwa mtendaji mkuu wa chombo hicho kinachosimamia Ligi Kuu na Championship.

Wakati wa mgogoro huo, kuliibuka mambo mengi yaliyoonyesha udhaifu katika dhana ya utawala bora, uendeshaji wa ligi, malipo ya washindi wa mashindano kama Kombe la CRDB na TPLB kutokuwa huru kujiendesha kwa ufanisi.

Tulitegemea mzozo huo uliodumu kwa miezi mitatu ungewafungua macho viongozi wa soka, kuanzia TFF, klabu, TPLB na wadau wengine.

ZENG 02

Tulidhani baada ya msimu kumalizika. Mkutano mkuu wa klabu unaotakiwa kufanyika mwishoni mwa msimu ungetawaliwa na mjadala mkubwa kuhusu udhaifu wa uendeshaji ligi unaosababisha mechi ziahirishwe kiholela na kwa amri kutoka kwa asiyejulikana.

Tulidhani wangejadili kwa kina udhaifu wa muundo wa Bodi ya Ligi unaompa mwenyekiti wa chombo hicho nafasi ya kuwa pia mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, au Kamati ya Saa 72, na nafasi ya kuongoza Kamati ya Uongozi ya TPLB.

Nafasi hizo tatu kwa mtu mmoja zinaondoa dhana ya uwajibikaji na utawala bora, kwa kuwa aliyeahirisha mechi ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Ligi na kamati inayotakiwa imhoji ndiyo anayoiongoza kama mwenyekiti.

ZENG 03

 Kwa hiyo, mwenyekiti hawajibiki kokote zaidi ya kwa TFF na hivyo kutozipa heshima klabu zinazomuweka kwenye kiti hicho.

Tulidhani mijadala iliyoibuka wakati wa mgogoro huo ingewafumbua macho viongozi wa klabu na kuona kwamba Bodi ya Ligi sasa ni kama shirika au kampuni kubwa inayotakiwa iendeshwe na watu wenye tabia na akili ya kibiashara, huku wakitumia miongozo ya uendeshaji kampuni kubwa ili kuhakikisha uwajibikaji na ufanisi unakuwepo.

Tulidhani ni wakati wa kuingiza watu wasio na upande kwenye Bodi ya Ligi kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na kushiriki katika maamuzi yasiyoegemea upande wowote kwa ajili ya afya ya chombo hicho.

ZENG 04

Tulidhani mijadala hiyo ingewasaidiai viongozi wa klabu kufanya utafiti kujua nchi nyingine wanawezaje kuwa na chombo imara kisichotikiswa na siasa za klabu kubwa na kinachoongozwa kwa weledi na uwajibikaji.

Tulidhani viongozi wa klabu wangekutana kujadili na kuteua jopo la watu wachache kutoka nje yao kuchunguza na kuwapa mapendekezo ya kuboresha muundo wa Bodi ya Ligi, usimamizi na uendeshaji wa ligi ili waamue waendelee na mazoea au wafanye mageuzi ili wajiendeshe kisasa.

Lakini mambo ni tofauti. Husikii kiongozi wa klabu akizungumzia mgogoro huo na jinsi ulivyowafumbua macho, badala yake baadhi wamejitokeza kuwania nafasi zilizoachwa wazi kwenye chombo chenye muundo mbovu usioendana na wakati.

Pengine wameona udhaifu wa muundo na kukosekana kwa uwajibikaji ndio maana wamechukua fomu kugombea nafasi za uongozi ili wautumie vizuri udhaifu. Na pengine hawaoni kabisa kama mgogoro wa mechi ya Simba na Yanga ulianika udhaifu mkubwa wa chombo kinachoongoza ligi inayoshika nafasi ya tano Afrika.

ZENG 05

Mazoea yanawafanya waende kwenye uchaguzi bila ya kwanza kushughulika na kasoro zinazowamiza za kuahirisha mechi hovyo, waamuzi kubadilishwabadilishwa, viongozi wa TPLB kujiona wanawajibika zaidi kwa TFF badala ya klabu zinazounda chombo hicho ambao zinatumia fedha nyingi kununua wachezaji, kuwalipa mishahara na posho, kuajiri makocha na wafanyakazi wengine.

Kwa hiyo wanaenda kwenye uchaguzi kama vipofu kwa kuwa hawakioni chombo wanachotaka kukiongoza, bali wanayataka madaraka ya chombo hicho.

Hadi TPLB inazaliwa ni makubaliano ya klabu na TFF yaliyofikiwa mwaka 2007 kwenye Azimio la Bagamoyo na baadaye mwaka 2011 kufanya ufuatiliaji uliozaa Kamati ya Mashindano iliyopewa jukumu la kuandaa uchaguzi ili kuunda chombo hicho.

Kati yam waka 2007 na 2013 wakati Kamati ya Ligi ilipoundwa, kulikuwa na viongozi wenye kufahamu uendeshaji wa kisasa wa ligi na hawa walipigania kuundwa kwa Bodi ya Ligi ili baadaye iwe kampuni inayojitegemea.

Hawa hawapo leo. Badala yake wameibuka viongozi ambao wanakwenda kwenye mkutano mkuu wa TFF kuweka azimio la “minne tena” badala ya kujadili masilahi ya klabu katika uendeshaji mpira wa miguu.

Ni juu yao. Uamuzi wa mwaka 2013 uliipa Bodi ya Ligi mamlaka kamili. Sasa kama viongozi wa klabu wanataka waendelee na mazoea, ni juu yao. Lakini mpira wa miguu hautaki mazoea tena. Unataka akili kubwa zaidi.