KIJIWE CHA SALIM SAID SALIM: Hivi ni zaidi ya vitimbi
KATIKA kila mchezo, yapo mambo ambayo sio ya kawaida na kila pakizungumziwa vituko katika michezo hukumbukwa na watu kubaki wanacheka.
Yafuatayo ni baadhi ya matukio ambayo mimi sidhani kama nitayasahau kila panaposimuliwa vituko vya zamani vya mchezo wa kandanda.
WATU NA NDEGE
Visiwa vya Scilly viliopo nje kidogo ya England kina timu mbili tu za soka, The Gunners na Wanderers, ambazo hukutana kila mwisho wa wiki.
Juhudi za kuunda timu ya tatu katika visiwa hivi vyenye watu 2,200 zimegonga ukuta kutokana na mashabiki kuona timu nyingi zitawakosesha raha ya ushindani mkubwa uliopo kati ya timu hizi.
Timu hizi mbili zinashiriki ligi ya aina yake. Nayo ni ya timu hizo mbili ti ambazo hukutana mara 10 katika msimu ili kupata klabu bingwa.
Kisiwa hiki kina watu 2,100, karibu nusu ya idadi ya ndege wanaoishi katika kisiwa hiki.
Wakazi wake wake wengi ni wenye umri wa makamo na vizee kutokana na vijana kukimbilia miji mengine ya Uingereza kutafuta kazi na strarehe.
Msimu wao wa ligi huanza katikati ya mwezi Novemba hadi mwishoni mwa mwezi Machi.
Vile vile wanayo mashindano mawili ya makombe ya Wholesalers na Foredeck Cup ambayo huchezwa kwa michezo miwili kupata mshindi.
KUPIGA MATEKE
Katika mwaka 1973, wachezaji wote wa timu ya Galilee walilala jela usiku kucha kwa sababu ya kuwapiga mateke wapinzani wao katika michuano ya ligi ya Israel.
Lakini ukweli ni kwamba hi ilitokana na hasara ya Wayahudi kuona timu hii ambayo ni ya Wapalestina watupu lushiriki katika ligi ya Israel kwa mara ya kwanza na kuibuka klabu bingwa.
Matokeo hayo yalipelekea magazeti ya Israel kutoka na vichwa vya maneno kama Aibu na fedha na wengine wakaeleza ushindi huo wa klabu ya Wapalestina kama ni tusi kwa Wayahudi.
Wapalestina nao walisherehekea kwa kutoa kauli kama ‘’ Kama tumewamudu katika kandanda kwa nini tusiweze kwenye mapigano?"
Klabu hii ya kijiji cha Galilee chenye wakazi 25,000 ambayo haina kiwanja cha mpira na zaidi kucheza kwenye viwanja vya mchanga pia ilibeba Kombe la Israel mwaka 2004.
CHUPUCHUPU JELA
Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Liberia mnamo Novemba 23, 1980 waliponea chupu chupu kwenda jela kufuatia kutoka sare bila ya kufungana na Gambia katika mashindano ya Kombe la Mataifa la Afrika.
Hapo kabla, kiongozi wa nchi hiyo Dikteta Sajenti Samuel Doe, aliwaambia wachezaji hao kwamba kama wangelifungwa na Gambia angewafunga jela wachezaji wote na viongozi wao.
Wapo wasaidizi wake ambao walitaka wachezaji hao wakifungwa basi waende jela pamoja na wake zao na watoto kwa sababu ya kulikashifu taifa la Liberia.
Katika kuonyesha kwamba alikuwa hafanyi mzaha Doe alipeleka kikosi cha askari wa magereza waliokuwa na silaha na pingu na gari mbili za kubebea wafungwa kiwanjani.
Gereza Kuu la jiji la Monrovia litakiwa kufanya matayarisho ya kuwapokea wachezaji hao kama wangelipoteza mchezo.
Baada ya mchezo ule na kuona waliponea chupu chupu kupelekewa gerezani baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa walikimbia Liberia na kutafuta ukimbizi nchi za jirani.
Wengine waliamua kustaafu kwa maelezo ya mwili umechoka au walikuwa wanasumbuliw ana majeraha na maumivu ya mwili.
MPIRA NA MSTARI
Timu ya Uingereza ilpocheza na Malta katika uwanja wa Wembley mwaka 1971, mpira ulivuka mara moja tu mstari wa katikati kwenda upande wa timu ya Uingereza.
Uingereza ilishinda 5-0 kwa kupata mabao mawili katika kiipindi cha kwanza na matatu kipindi cha pili. Hii ni rekodi ya aina yake katika soka.
Kipa wa Uingereza katika kikosi kile, Gordon Banks, hakuugusa mpira hata mara moja wakati wote wa mchezo.
Hii ilipelekea mara baada ya mchezo kuukimbilia mpira na kuushika kwa maelezo asingekuw ameutendea haki mpira kama na yeye hakuucheza.
FRIKIKI MARA SABA
Timu ya Kilmarnock kule Scotland ililazimika kupiga mara saba mpira wa adhabu katika mchezo wa ligi wa 1945.
Jinsi ilitokana na mara sita kila mpigaji akisogea kuupiga mpira kipa wa timu ya Patrick alisogea mbele ya mstari wa goli.
Hatimaye mpira wa adhabu ulio sahihi ulopigwa golikipa aliuzuia. Patrick walishinda 5-3.
Wataalamu wa andnda walisema kitendo cha golikipa usumbufu wa golikipa kilimparaganya mchezaji aliyekuwa anapiga penalti
SHABIKI MZEE
Katika mchezo wa ligi ya mpira wa magongo katika mji mdogo wa Congelton, Uingereza, mwaka 1993, wachezaji walikatisha maomblezi ya dakika moja ya kifo wa shabiki mmoja mzee aliyekuwa maarufu kwa mchezo huo.
Hii ilitokana na huyo” marehemu” kufika uwanjani sekunde chache baada ya kupigwa filimbi ya kuomboleza kifo chake.
Alipoingia uwanja na kuambiwa wachezaji walikuwa anaomboleza kifo chake aliingia uwanjani, akampokonya muamuzi filimbi na kuiouuliza ili kumalizika maombolezi.
Mwandishi mmoja alipomuuliza ilikuaje hata pakawepo taarifa ya kwamba alikuwa anamefariki alijibu;’’Mtafuteni ziraili anayetoa roho, labda anajuwa kilichtokea’’.
Mwisho wa mchezo huyu mzee alichangiwa pesa ili akafurahia kukawia kwa kif chake.
TIMU NZIMA KUONYWA
Timu ya Leicester ilicheza mchezo wa Kombe la FA na Northampton Town mwaka 1997 bila ya wacheaji wake kufanya madhambi hata mara moja wala mchezaji yoyote kuonywa. Leicester ilishinda 4-0.
Baadhi ya wachezaji walipoulizwa ilikuaje walikuwa na maelezo ya kufurahisha. Miongoni mwao ni wao ni wastaarabu kuliko wachezaji wa timu nyengine.
MWENDESHA BAISKELI
Akiwa na umri wa miaka 52, Pedro Gatica aliendesha baiskeli maelfu ya kilomita kutoka kijiji chake cha Argentina kwenda Mexico kuangalia fainali za Kobe la Dunia za kandanda.
Alipofika huko alishindwa kumudu kulipia ada ya kuingia mpirani. Wakati anatafuta pesa baiskeli yake ikaibiwa na alipokuwa anakwenda polisi kutoa taarifa ya kuibiwa akakabwa na kunyang’anwa saa na viatu vyake.
Alihangaka kwa zaidi ya miezi miwili kupambana na maisha na hatimaye akapata pesa na kunua baiskeli nyengine na kufunga safari ya zaidi ya wiki mbili ya kilomita 8,000 kurudi nyumbani.
Tokea kupata mkasa ule aliacha kwenda mprani kwa kutumia baiskeli alipokuwa kwao Argentna.
NYAMA YA KITIMOTO
Mchezaji wa kiungo wa kklabu ya Jiiul Petrosani, Romania, Ion Radu aliuzwa kwa klabu ya daraja la pili ya Valcea katika mwaka 1998 kwa kilo 500 za nyama ya nguruwe.
Klabu ya Vacea ambayo inalo zizi kubwa la nguruwe ilikuwa haina pesa wakati ule na kuamua kuipa klabu ya Jiul nyama ya nguruwe ambayo baadaye iliuzwa kwa pauni 1750 za Kiingereza.