Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kifua cha Kylian Mbappe na wenzake kitaamua mengi

PAZIA Pict


KWA kujisikia zaidi. Kila mtu anafunga kwa kujisikia zaidi katika ardhi ya Mexico, ardhi ya Marekani na ardhi ya Canada. Kombe la dunia linaendelea. Nani aliyetarajiwa kufunga na hajafunga? Sidhani. Labda Sadio Mane.


Lakini Lionel Messi amefunga. Cristiano Ronaldo amefunga. Kylian Mbappe amefunga. Vinicius Junior amefunga. Ousmane Dembele amefunga. Erling Braut Haaland amefunga. Kila mtu amefunga zaidi ya mabao mawili.


Kabla ya leo usiku Messi alikuwa na matano, Mbappe manne, Haaland manne, Vinicius manne, Ronaldo mawili. Na watafunga zaidi katika mechi za mwisho. Messi ambaye ameipiku rekodi ya Miroslav Klose na kuwa mfungaji bora wa muda wote akiwa na mabao 18 anaweza kutanua zaidi wigo wake atakapokabiliana na Jordan.

Ukweli mchungu ni namuona Mbappe akiwa na kifua cha kwenda mbali zaidi ya wenzake. Mfungaji bora wa michuano hii anaweza kupatikana kwa timu yake kwenda mbali zaidi katika michuano hii.

PAZ 01

Ndiyo kwanza tunaingia katika hatua ya 32 bora. Katika michuano iliyopita tungeweza kusema kombe la dunia ndio linaanza. Timu zilikuwa 32 tu. Sasa hivi zipo 48. Wakubwa gani wataweza kushikilia bomba?

Wakubwa ambao wataweza kushikilia bomba kwa muda mrefu ndio ambao watafanikisha mambo mawili. Jambo la kwanza ni kutupa mfungaji bora lakini jambo la pili ni kutengeneza historia mbalimbali.

Kwa mfano, Wareno wanataka kumpa Cristiano Ronaldo taji lake la kwanza la kombe la dunia. Baada ya michuano hii Ronaldo anaweza kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa. Anataka awekwe katika kapu moja na Pele, Diego Maradona, Messi kama miongoni mwa mastaa bora waliowahi kucheza soka na walitwaa kombe la dunia.

PAZ 02

Hapo hapo Ronaldo anatamani kuiongoza safari hii kwa kuwa mfungaji bora wa michuano. Tatizo Ureno wanaweza kufanikisha safari ya Ronaldo? Mafanikio yao makubwa ni kuwa washindi wa tatu mwaka 1966. Miaka 60 iliyopita.

Siwaoni Wareno wakifika mbali. Siwaoni wao na Ronaldo wakibebana zaidi. Siwaoni. Kazi inabidi ifanyike kweli kweli kama wanataka kufika walau nusu. Haya yote yanaendelea huku Ronaldo mwenyewe akiwa miongoni mwa matatizo ya timu yenyewe.

Messi na Argentina yake? mungu aliwapa kombe la dunia miaka minne iliyopita pale Doha. Ni kama maandiko yalitimia mwanasoka bora kuliko wote duniani atwae kombe la dunia. Ukikumbuka namna Kolo Muhani alivyotazama na kipa Emilio Martinez dakika za majeruhi na kukosa bao la nne kwa Wafaransa unagundua iliandikwa tu Messi atwae kombe la dunia.

PAZ 03

Kila siku kikosi cha Waargentina kinapungua nguvu. Kina Nicolas Otamendi na Messi mwenyewe wanazidi kuzeeka. Katika michuano hii pia walipata bahati ya kupangiwa timu za kawaida katika Kundi lao la J. Wamepangiwa Austria, Algeria na Jordan.

Ni rahisi kupita huku lakini Argentina wanahitaji maajabu mengine kufika fainali na kutwaa kombe la lenyewe. Wakifanya hivyo watakuwa wamezifikia Ujerumani na Italia kwa kutwaa taji hilo mara nne.

Messi pia atakuwa ametwaa taji lake la pili. Hata hivyo, siwaoni wakifanya hivi. Hii rekodi yenyewe ya Messi naona haitadumu kwa muda mrefu mbele ya Mbappe. Mbappe ana kikosi cha kumfikisha fainali.

Mbappe ana kikosi ambacho kinaweza kumfanya acheze mpaka mwisho. Hauwezi kubishana sana. Ufaransa ya leo inaweza kuwa kama Brazil. Wabrazil waliwahi kufika fainali tatu mfululizo. Mwaka 1994, 1998 na 2002. Wafaransa wana kizazi kinachoweza kufanya hivyo.

PAZ 04

Walifika fainali mwaka 2018 pale Moscow, wakafika fainali za mwaka 2022 pale Doha na kuna uwezekano pia wakafika fainali hizi. Ukiitazama timu yenye Mbappe mwenyewe, Michael Olise na Dembele unaona wana kikosi cha kufanya hivyo.

Sio hawa watatu tu. Wengine katika nafasi mbalimbali kina William Saliba, Dayot Upamecano, Rayan Cherki na wengineo. Kila mmoja anaonekana yupo katika kilele cha ubora wao tofauti na vikosi vingine. Benchi lao pia limesheheni watu wengi ambao wanaweza kuingia ndani na kupambana na timu yoyote duniani.

Halafu kuna rafiki yetu Erling Haaland. Hakuna ambacho hajawahi kuthibitisha linapokuja suala la kuziona nyavu. Kombe lake la kwanza la dunia lilikuwa jukwaa la kutuonyesha huwa habahatishi kuwafunga wazungu wenzake katika ligi za Ulaya pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa.

Hata hivyo, sioni kama Haaland ana timu ambayo inaweza kumfikisha mbali kama Mbappe. Sawa, kando yake ana nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard, ana mshambuliaji mwenzake mahiri wa Atletico Madrid, Alexander Sorloth pamoja na winga mahiri wa RB Leipzig, Antonio Nusa.

Bado siioni Norway ikimpa mechi nyingi Haaland mpaka hatua ya fainali. Uzuri wa Haaland ni yeye mwenyewe ni jeshi la mtu mmoja. Katika mechi hizi hizi mpaka Norway itakapotolewa unaweza kukuta anatupia mabao mechi ndani ya mechi moja.

Kwa wafunga wote waliopo katika kombe la dunia kwa sasa Haaland ndiye hatari zaidi. Tatizo sioni kama Norway itafika mbali zaidi. Mbappe anaweza Kwenda mbali zaidi. Na uzuri wa Mbappe anaweza kufunga katika mechi nyepesi na katika mechi nzito.

Nina hofu kwamba ana kifua cha kuwabeba wenzake mpaka juu zaidi. Na uzuri kwake ni kwamba hata wenzake wana vifua vya kumbeba mpaka mwisho wa safari. Nina hofu huenda Wafaransa wakatwaa taji hili kwa mara nyingine tena. Labda kama kuna maajabu yatatokea mbele ya safari.