Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kibamba amenyooka wagombea Simba SC mjipange

KIBAMBA Pict
KIBAMBA Pict

Muktasari:

  • Yeye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ambalo linamiliki timu ya Pamba Jiji na mwenyekiti wa timu hiyo alikuwa mmoja wa wagombea wawili wa nafasi hiyo moja.

KIOMONI Kibamba ametokea kupata mashabiki wengi hapa kijiweni kutokana na namna anavyotimiza majukumu yake kwa weledi.

Jamaa anaitendea haki sana ile kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa vile ananyoosha mambo na huwa anapoingia yanakaa kwenye mstari na huwa jambo lake linamalizikaga bila vurugu wala purukushani.

Tulipoona kamati yake imeingia kusimamia uchaguzi wa Simba basi tukaona ni vyema tuwakumbushe watu wote wenye nia ya kugombea wahakikishe wanafuata vyema kanuni, taratibu na miongozo ya uchaguzi ya klabu yao na ya TFF.

Wahakikishe wana sifa stahiki kwa nafasi ambazo wataziwania, wajaze fomu vizuri na wawe na weledi katika kufuata muongozo wa mchakato wa uchaguzi vinginevyo yasije kuwakuta.

Wakifanya kinyume na hayo wasitegemee Bwana Kiomoni Kibamba atakuwa na huruma na busara kwao kwani kitakachofuata ni kwamba atawatupilia mbali nje na mchakato huo ambao unasubiriwa kwa hamu.

Kwenye jambo lake, yule Kibamba huwa hacheki na mtu na haangalii mhusika anajuana na nani au ana sapoti kubwa kiasi gani bali yeye anazingatia miongozo inasema  nini.

Mfano kilichotokea juzi katika uchaguzi wa kuwania nafasi moja ya ujumbe wa kamati ya uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kule Dodoma kinaweza kuwa uthibitisho tosha wa namna Wakili Msomi Kiomoni Kibamba alivyo mweledi.

Yeye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ambalo linamiliki timu ya Pamba Jiji na mwenyekiti wa timu hiyo alikuwa mmoja wa wagombea wawili wa nafasi hiyo moja.

Hata hivyo, Kibamba alimuondoa mwenyekiti huyo wa Pamba Jiji na kuacha jina moja tu la Mwenyekiti wa Dodoma Jiji japo yeye na aliyeenguliwa wapo katika taasisi moja.