Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagera Sugar walichemsha kumuacha Chirwa

KAGERA Pict

Muktasari:

  • Ndio alikuwa mchezaji wao bora katika Ligi ya Championship hivyo ndio angepaswa kuwa mchezaji wa kwanza kubakia kikosini baada ya kuingia Ligi Kuu.

KAGERA Sugar walitakiwa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha Obrey Chirwa anabaki baada ya kuwapandisha daraja msimu uliopita.

Ndio alikuwa mchezaji wao bora katika Ligi ya Championship hivyo ndio angepaswa kuwa mchezaji wa kwanza kubakia kikosini baada ya kuingia Ligi Kuu.

Mtu akishakufungia mabao tena 18, maana yake anajua huyo kwa hiyo unatakiwa umlinde kwa gharama yoyote kwa vile tayari anaijua vyema timu na ameshazoeana na wenzake.

Badala yake, Kagera Sugar ikamuacha Chirwa aondoke na akajiunga kwa wapinzani wao kwenye Championship msimu uliopita Geita Gold ambao wameanza kuonja faida ya uamuzi wao wa kumsajili.

Hadi sasa ameshatupia mabao manne kwenye Ligi Kuu na ndiye anaongoza kwa kufumania nyavu akiwatangulia mastaa kibao akiwemo Peter Shalulile wa Yanga.

Angalia sasa Kagera Sugar imeruhusu mpinzani wake Geita Gold kuimarika zaidi huku yenyewe ikizidi kuongeza udhaifu kwenye kikosi chake kwa kumuacha mfungaji wake tegemeo.

Na kuonyesha jamaa aliachwa aondoke kimakosa, hayo mabao manne ambayo amepachika, ni mengi zaidi ya yale yaliyofungwa na Kagera Sugar hadi sasa kwenye Ligi Kuu.

Maana Kagera Sugar imefunga mabao matatu hivyo Chirwa pekee ameizidi kwa bao moja. Emu fikiria kama angekuwapo, maana yake Kagera ingekuwa na mabao saba.