Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya uwanja wa Dabi, Yanga wako sahihi

Muktasari:

  • Katika barua hiyo, Simba wamehoji uhalali wa taarifa ya mabadiliko ya uwanja kutolewa kwanza na Yanga. Februari 15 mwaka huu, Yanga kupitia ofisa habari, Ali Kamwe, ilitangaza mabadiliko ya uwanja kutoka Mkapa hadi New Amaan Complex, Zanzibar.

SIMBA wameandika barua kwenda Bodi la Ligi (TPLB) kutaka ufafanuzi kuhusu uwanja wa mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba itakayofanyika Machi Mosi, mwaka huu.

Katika barua hiyo, Simba wamehoji uhalali wa taarifa ya mabadiliko ya uwanja kutolewa kwanza na Yanga. Februari 15 mwaka huu, Yanga kupitia ofisa habari, Ali Kamwe, ilitangaza mabadiliko ya uwanja kutoka Mkapa hadi New Amaan Complex, Zanzibar.

Baada ya taarifa ya Yanga, ofisa habari wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda, alinukuliwa akikanusha kisha siku iliyofuata, Februari 16, TPLB ikatoa taarifa rasmi kuthibitisha kilichosemwa na Kamwe.

Aidha, Simba imeitaka TPLB kueleza ni kanuni ipi imetumika kuhamisha uwanja huo, ikieleza kuwa kwa mujibu wa kanuni za ligi, taarifa ya kuhamisha mechi inapaswa kutolewa angalau siku 21 kabla ya tarehe ya mchezo husika.

Kiutaratibu, mamlaka zinazoruhusiwa kutangaza uwanja ni Bodi ya Ligi, sio klabu. Lakini Yanga wakatoa taarifa, Bodi ya Ligi wakaikanusha...kisha wakaibariki, na ikawa. Na huo ndio upupu wetu wa leo tutakaoujadili pamoja leo kwenye makala hii. Bismillah...!

Mamlaka zetu za mpira Tanzania, TFF na Bodi ya Ligi zimejitwisha majukumu ambayo kimsingi sio ya kwao. Moja ya majukumu hayo ni hili la kutangaza uwanja wa mechi. Wakati wote, mara zote na miaka yote, Bodi ya Ligi ndiyo hujipa mamlaka ya kutangaza uwanja utakaotumika kwa mechi fulani.

Lakini safari hii Yanga wamewawahi, wametangaza wao. Kwa kuwa Simba hawajazoea utaratibu huo, ndio maana sukari imepanda. Na sasa wanalalamika kwa sababu wanaona utaratibu umekiukwa. Ni kweli kabisa.

Yanga hawakuwa sahihi kutangaza uwanja wa mechi kwa sababu kimazoea hilo ni jukumu la Bodi ya Ligi. Lakini, kwanini Bodi ya Ligi ijitwishe jukumu la kutangaza uwanja wa mechi? Hawakodi uwanja na hawaingii gharama yoyote.

Timu mwenyeji ndio hukodi uwanja kwa wamiliki, hulipia na kufuata taratibu zote. Kimsingi mwenyeji ndiye anapaswa kuutangazia umma kwamba 'mechi yetu itachezwa uwanja fulani', sio Bodi ya Ligi. Kitendo cha Yanga kutangaza uwanja kimewachochea Simba kuandika barua.

Na kitendo cha Simba kuandika barua kitatusaidia kubadilisha utaratibu huo wa hovyo. Ndio maana nasema Yanga wako sahihi na Simba wako sahihi. Mamlaka za mpira ni lazima zitaarifiwe na timu mwenyeji kuhusu uwanja. Ni kweli.

Zikishataarifiwa zitaenda kuukagua na kuona kama unakidhi vigezo. Ni kweli.

Lakini, baada ya hapo kinachotakiwa ni kwa mamlaka kurudi kwa mwenyeji na kuwaambia kwamba uwanja umekidhi vigezo hivyo watangaze. Lakini, wao hawafanyi hivyo, wakishaona uwanja unafaa wanatangaza. Ndio shida ilipo.

Mgogoro huu wa sasa utusaidie kubadilisha hili. Timu mwenyeji anayo haki ya kuwatangazia mashabiki wake uwanja wa mechi. Hii ina faida kubwa kibiashara na kuonyesha nguvu ya klabu kwa bidhaa zake. Mechi ni moja ya bidhaa kuu za timu; kama jezi na vitu vingine.  Klabu iachwe kuwa na mamlaka juu ya bidhaa zake.

Kitendo cha Bodi ya Ligi kuhodhi mamlaka ya bidhaa hii ni ubabe usio na maana yoyote. Taarifa ya uwanja wa mechi ikiwekwa kwa mara ya kwanza katika mitandao ya kijamii ya klabu itavutia uchangiaji mkubwa, na hiyo ndio biashara ya klabu.

Yawezekana Yanga walitoa taarifa hiyo kwa bahati mbaya au tu kiburi cha kiyangayanga, lakini kosa hilo litatusaidia sana kubadilisha utaratibu usio na tija. Na hapo ndipo tunapopaswa kuwapa Yanga kongole. Lakini hata hivyo, yawezekana endapo Simba wasingeandika barua lingepita kimyakimya. Na hapo ndipo tunapopaswa kuwapa Simba kongole.

Kongole Yanga, kongole Simba. Hili sakata la uwanja wa mechi ya watani litatusaidia kupunguza nguvu ambazo mamlaka za mpira zimejilimbikizia.