Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

GOZI LA NG'OMBE: Manara anaposahau jina la filamu

Soka letu ni moja ya tamthiliya bora kwelikweli kuisimulia. Inavukuvutia kwa wakati mmoja na inakukera kwa wakati mwingine lakini ilimradi tu mwandishi wake ameamua kuhusisha wahusika mbalimbali kwa nyakati tofauti ili pande tofauti tofauti ziweze kuishi kwa kupishana pishana na kurithisishana matatizo au faida. Ni rahisi kutabiri ni lini Haji Manara atakuwa kimya huku pia ukiwa na uwezo wa kuandaa maono ya lini Antonio Nugaz atakosa pa kukimbilia. Wakati huohuo ni rahisi zaidi hata kuamua kutabiri bingwa wa nchi kabla ligi haijaanza.

Mtunzi wa tamthiliya hii ya ligi yetu hajawahi kujitokeza hadharani lakini walau tunafahamu imewekeza muda mwingi zaidi Kariakoo kuliko Chamanzi au kuliko hata pale Mwanza ambako timu hazijawahi kufurahia kuishi ndani ya ligi kuu. Ni tamthiliya iliyobeba maisha ya wanaume wawili waliodumu kwa muda mrefu bila kujenga miji yao lakini bado wanajiita na wanaamini kuwa wao ni matajiri. Tamthiliya ambayo ndani yake kuna umaarufu wa wasemaji kuliko wachezaji wa vilabu husika na ambayo pia imebeba uhalisia wa tamu na chungu ya soka letu.

Watizamaji tunaendelea kupata uhondo na hususani hili Jipya la tamthiliya lililopo mezani kwa klabu ya Simba kwa sasa. Tunatizama kipindi ambacho kimewahi kuonekana huko nyuma lakini chenye picha kubwa ya namna gani soka letu lilivyo. Hujuma ndicho kitu kikubwa ambacho kinatajwa na wengi kuwa ndio mkasa uliopo kwenye kipindi hiki na ambao mtunzi anajaribu kutuonyesha. Simba ilipoteza michezo miwili mfululizo bila kuwa na mastaa wake Chama, Kagere pamoja na Mugalu.

Hata hivyo kwenye karatasi za ripoti ziliomba majina kadhaa yaondoke kikosini ambayo ni kocha wa magolikipa Mwarami Mohamed, meneja wa timu Patrick Rweymumu na vijana wa wiwili upande wa kitengo cha maudhui ya mtandaoni ambao ni zao Ally Shatry maarufu kama “Bab Chico” na Jacob. Hata hivyo mtunzi ametuficha ni nani aliyeomba hawa wapumzike na pia wanahusianaje moja kwa moja na timu kucheza vibaya ndani ya uwanja.

Inaenda mbali zaidi na tunaona Manara mwenye mdomo wake amekuwa mkimya kwa sababu mara mbili tofauti amenyamazishwa na amekosa la kusema. Ni simba hii ambayo imekuwa bingwa misimu mitatu mfululizo na bila kubadili kikosi cha kwanza kwa kiasi kikubwa na bado Manara na Mo pamoja na wengine wanahisi timu hii haiwezi kupoteza michezo miwili mfululizo.

Kuna kitu ambacho mtunzi anajaribu kutuonyesha ambacho wengi wanakipuuza lakini kinaitwa njano na kijani. Simba hawataki kupoteza kwa sababu Yanga inashinda. Wangekuwa na matokeo pacha hakuna ambaye angehangaika na hawa akina Mwarami hata kidogo. Simba wanaishi katika presha ya maneno yao wenyewe, kejeli za kikosi kipana na ubingwa wa miaka nane mfululizo.

Hili ni tatizo la vilabu vyetu na wamekuwa wakipokezana kweli. Wanaishi katika dunia ya uongo wakiamini kuwa ndio ukweli wenyewe kwa sababu tu wanaweza kuahidiana maziwa na asali huku wanasahau kuwa wapo katika jangwa ambalo hata ngamia wameadimika. Wameanza akina Mwarami lakini sura ya Sven inaonyesha kabisa kuwa kuna aibu ya ubingwa aliowapa msimu uliopita ndio inayombakisha klabuni hapo. Presha kwake ni kubwa kuliko ilivyokuwa kawaida na lolote linaweza kutokea siku za karibuni.

Hata hivyo hakuna mchawi kwenye hili, timu zote duniani hupata shida zinapopoteza wachezaji wake muhimu. Manchester City ilitoka kuwa bingwa mtetezi mpaka kukabidhi ubingwa kwa Liverpool mapema kwa kumkosa mchezaji mmoja tu ambaye ni Aymeric Laportem beki wao wa kati. Liverpool kwa sasa ilianza kukosa uelekeo kwa kukosa mchezaji mmoja pia. Hali ipo hivi duniani kote na hili halijawahi kuwa jambo la ajabu hususani kwa Simba iliyokuwa inacheza bila mchezaji wake bora, Clatous Chama pamoja na washambuliaji wake wote wa kati.

Hata hivyo tatizo ni moja tu, kwa timu zetu hizi sio sababu za msingi kwa sababu tayari kuna kitu Manara, Mo, Nugaz au Bumbuli wanakuwa wameahidi hapo kabla. Wanaishi katika dunia yao huku timu ikicheza kivyake. Hii tamthiliya haiishi leo, msimu uliopita mtunzi alituonyesha ya Yanga na sasa kaanza kuonyesha vipindi vya Simba. Bahati mbaya Haji Manara na wenzie hawataki hata kusoma “script”, tabu ipo hapa na wanajifanya hawajui jina la tamthiliya wakati wanaiishi. Hata hivyo ukweli ni kuwa amejisahaulisha makusudi tu, kwa sababu mdomo wake unacheza soka kuliko miguu ya wachezaji.

Tatizo lingine kubwa ni kuwa Yanga haichezi vyema mechi nyingi na inapata ushindi, wao wakiwa wanasema kitaalamu “winning ugly”. Uwezekano wa Yanga kukalia kiti cha uongozi ni mkubwa zaidi na huku pia presha hii ikiwa inaelekea kwenye mechi ya watani wa jadi. Simba wana maswali mengi zaidi ambayo wanaandika kwenye vitabu vyao vya “notes” kuliko majibu ya wapi wamekwama baada ya kuwa na imani kubwa.


Imeandikwa na Nicaus Agwanda