Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Folz azua jambo Yanga, afichua siri 12

FOLZ Pict

Muktasari:

  • Katika benchi la ufundi la Yanga la sasa kuna Kocha Mreno, Pedro Goncalves aliyechukua nafasi ya Mfaransa Roman Folz aliyedumu klabu hapo kwa muda mfupi (miezi miwili na siku 25).

YANGA imekuwa na mwendelezo mzuri kwa misimu kadhaa na inachotaka ni kuzidi kupanda na si kushuka. Haya ni sawa na malengo ya kila timu na ili kufanikisha hilo, zimekuwa zikibadilisha vikosi hadi mabenchi ya ufundi mbali na viongozi wa klabu.

Katika benchi la ufundi la Yanga la sasa kuna Kocha Mreno, Pedro Goncalves aliyechukua nafasi ya Mfaransa Roman Folz aliyedumu klabu hapo kwa muda mfupi (miezi miwili na siku 25).

Kuondoka kwa Folz kulitokana na mabadiliko yasiyoridhisha kikosini na hasa kwa mashabiki walioiona timu yao haichezi na hata matokeo siyo wanayoyafurahia ndiyo ukafanyika uamuzi mgumu wa kumwondoa kocha huyo Mfaransa na kutua Mreno.

Folz ni mmoja wa makocha kutoka nje waliowahi kuinoa klabu ya Ligi Kuu Bara, kwani alikuwa na umri wa miaka 35 na baada ya kuondoka na kurudi kwao Ulaya mambo Yanga yanaendelea kama kawaida na iko Zanzibar kujiandaa na mechi ya hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa kesho Uwanja wa New Amaan dhidi ya FAR Rabat ya Morocco.

Hata hivyo, ni wazi kuondoka kwa Folz bila kuongea popote kuliwaacha wadau na mashabiki na maswali wakitamani kumsikia baada ya maamuzi yale na Mwanaspoti lilifanya juhudi kumtafuta na kufanya naye mahojiano maalumu na kafunguka mambo mbalimbali kuhusu maisha yake na soka kwa jumla hasa akiwa Yanga.

FOL 05

UKOCHA NA UMRI MDOGO

Anasema baada ya kucheza soka kwa kipindi kifupi na hasa katika akademi, aliamua kugeukia ukocha ambako ndiko kulikuwa malengo yake ya muda mrefu na alianza kufundisha akiwa na umri mdogo tofauti na makocha wengi ambao hucheza kwa muda mrefu kabla ya kuibukia katika kazi hiyo.

"Ilikuwa akademi ya klabu ya kitaaluma Ligi Kuu Ufaransa (League 1), lakini baadaye nikaamua kubadilika kisha nilianza kufundisha soka nikiwa mdogo sana. Ndani ya miaka 17 tu nikaanza safari hiyo."

“Yalikuwa malengo ya muda mrefu tangu nikiwa kijana mdogo, siku zote nimekuwa na shauku ya kutaka kuelewa mchezo wa soka na jinsi ya kufanikisha hilo kwa ufanisi mkubwa, niliangalia mechi nyingi kadiri nilivyoweza, kuwajua wachezaji wote vizuri, hayo yalikuwa makusudio yangu," anasema kocha huyo raia wa Ufaransa aliyezaliwa katika Jiji la Bordeaux, Kusini Magharibi mwa Ufaransa mwaka 1990.


FOL 07

YALIYOMPELEKA YANGA

Anasema kwake uamuzi wa kutua Yanga ulikuwa sahihi na rahisi kwa sababu kuu mbili, licha ya malengo kutotimia baada ya kutimuliwa.

“Ilikuwa rahisi sana, nilichukua maamuzi kwa sababu kubwa mbili, ya kwanza ilikuwa ni mashabiki kwa sababu nilijua ni namna gani wanaisapoti timu yao na namna wanavyoona fahari kuwa mashabiki wa Yanga, sababu ya pili ilikuwa kuipeleka klabu mbali barani Afrika na niliona inawezekana."


FOL 06

PRESHA ILIVYOMFELISHA

Folz alisaini mkataba wa mwaka mmoja Yanga ukiwa na kipengele cha kuongeza zaidi na katika hilo, kulikuwa na Project (mradi) ya muda mrefu kwa ajili ya kufanya makubwa katika kikosi hicho.

Hata hivyo, anasema pamoja na maelezo aliyoyapata kutoka kwa viongozi na mipango yao ya kuifanya kuwa kubwa Afrika kwake iliishia njiani.

“Nilikubali na kuanza kutengeneza na kuunda karibu kila kitu ili tuweze kufikia malengo, bahati mbaya baadaye niligundua haikuwa projekti ya muda mrefu hata kidogo, tofauti na tulichokubaliana kabla, kulionekana sababu nyingi za wazi na kwangu nilinipa picha ya kuelewa mambo vizuri."


MASHABIKI KUKATAA SOKA LAKE

Katika kuitekeleza projekti hiyo, anasema ilikuwa hatua za mwanzo kabisa na timu ilikuwa haijapoteza mchezo wowote wala kuruhusu bao na ilishinda na kutoka sare, hata hivyo, wakati wakizidi kuimarika ndipo yakatokea ya mashabiki kukataa soka lake hali iliyosababisha kutimuliwa.

“Ile mechi ya mwisho tulipoteza 1-0, tulipoteza kwenye mazingira ambayo naweza kusema yalikuwa ya kipekee sana, haikuwa chini ya udhibiti wangu hata kidogo.

“Kwa upande wa utendaji uwanjani, tulikuwa sawa kulingana na mahali tulipaswa kuwa, kushinda michezo na kudhibiti matukio, tulikuwa tunaendelea kuimarika na kukua ili kuendelea kuwafurahisha mashabiki kila wakati.

"Hiyo ilikuwa hatua ya mwanzo ya mradi huo, ulikuwa mzuri. Hata hivyo, huwezi kuwa na kila kitu na matokeo kuonekana kwa haraka. Hiyo siyo njia nzuri ya kujenga projekti, lakini ukiwa una subira na kujenga kimkakati, matokeo yako ya mwisho yatakuwa makubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

“Kuna mifano mingi duniani kote ambayo inakuonyesha hivyo, hilo ndilo nililokuwa nikijenga ili kupata matokeo mazuri ya muda mrefu na ningefanikisha hilo."


FOL 04

ANAVYOLIONA SOKA LA TANZANIA

Kwa viwango vya ubora Afrika, Ligi Kuu Bara inashika nafasi ya tano na hii imetokana na kuongezeka kwa ushindani unaoletwa na wachezaji wengi wazawa na kutoka nje kama anavvyokiri Folz;

“Ninaiona kama ligi yenye ushindani, yenye wachezaji wazuri na wenye mapenzi makubwa na mchezo pamoja na mashabiki kwa jumla," anasema na kuongeza;

"Bado kuna mambo ya kuboresha na nafasi ipo. Kwa mfano kwenye baadhi ya miundombinu.

"Nimeona Uwanja wa Mbeya (Sokoine) ulipigwa marufuku baada ya sisi kucheza pale tukipata sare ya 0-0, haikuwezekana kucheza kwenye uwanja wenye sura mbovu ya namna ile, maamuzi ya kuufungia nadhani yalitakiwa kufanyika kabla ya sisi kwenda pale, hii nimetoa kama mfano tu.”


KUIFUNGA SIMBA HAIKUWA KAZI NDOGO

Anakumbushia namna walivyojipanga kukabiliana na Mnyama katika mechi ya Ngao ya Jamii na ushindi wa bao 1-0 walioupata haukuja kirahisi na kulikuwa na ishu ya presha kwake.

"Sina shida na presha. Si kitu kwa ninachokipenda na kinachonisukuma."

“Kusema kweli ushindi dhidi ya Simba ulikuwa wa hisia kubwa kwangu, kwa sababu tulimshinda mpinzani wa kihistoria na kuchukua kombe muhimu. Kuna mambo mengi ambayo watu hawafahamu yanayoweza kuwa yameathiri matokeo ya mchezo huo.

“Kwa mfano, miongoni mwa mambo mengine ni hadi tunakwenda kucheza mechi ile kubwa, hatukuwa na kambi inayofaa sana wakati wa maandalizi ya msimu mpya, ilipangwa kikamilifu kwa maelezo lakini iliahirishwa dakika za mwisho kwa sababu ambazo zina uhusiano wowote nazo wakati huohuo Simba wenyewe walikwenda Misri kujiandaa tofauti kabisa na sisi lakini bado tuliwafunga na kucheza vizuri, nilifurahi kuwapa furaha hiyo mashabiki wa Yanga."


FOL 03

ALIYEMSAJILI YANGA

Folz alikuja wakati timu hiyo ikiwa kwenye dirisha la usajili na hapa anafichua juu ya kutohusika kusajili mchezaji yeyote.

“Hakuna, hakuna mchezaji ambaye nilimsajili Yanga, hata nilipopendekeza majina na wasifu kadhaa kwa nafasi maalumu, hakuna ambacho kilifanikishwa na nilielewa tu na kuamua kufanya kazi na nguvu niliyoikuta.

“Nilifanya ukaguzi kamili wa awali, nilitazama kila mchezo uliochezwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kisha nikatuma ripoti na maelezo ya wazi na kueleza sababu juu ya kile kilichohitajika kwa timu."

Alipoulizwa ilikuwaje mapendekezo yako hayakutekelezwa? Folz anajibu;

“Kama nilivyosema, niliweka wazi juu ya kile kinachohitajika na ni nani nilitaka kumuajiri, mapendekezo yangu yote yalikuwa ya kweli yangeleta ubora mwingi kwa timu, zaidi ya hayo, yangeongeza kitu moja kwa moja kwenye projekti kulingana na mchezo niliotaka kuutekeleza msimu huu."

“Sikufuatwa na klabu katika suala hilo na lilikatisha tamaa sana kwa sababu lilikuwa na athari kubwa katika kuchelewesha projekti kulingana na mtindo wa uchezaji."


AIPA YANGA MATAJI

Kama ilivyokuwa kwake malengo ilikuwa ni kubakisha mataji ya msimu uliopita na hapa anaona endapo Yanga itabadilika katika baadhi ya mambo, itafanikisha hilo licha ya kuwepo kwa upinzani msimu huu;

“Wanaweza kubakisha mataji ya ndani lakini kuna ushindani mkali msimu huu. Itahitaji uthabiti katika vipengele vingine hasa kwenye mashindano ya Afrika, lazima kuna mambo yabadilike kwa kukusudia kuyarekebisha kwa kuzingatia na kuheshimu weledi."


ALIVYOFUTWA KAZI

Folz alipoteza kazi yake akiwa nje ya nchi, Malawi mara baada ya timu kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Silver Strikers ya nchini huko. Licha ya timu kushinda mechi tano kati ya saba za kimashindano, haikutosha kumbakiza hasa kutokana na mashabiki kuponda soka lake na kushinikiza atimuliwe.

Katika mechi dhidi ya Silver Strikers aliyopoteza kwa bao 1-0, ndiyo maamuzi ya kumtimua yalitoka kabla hata hajarudi na timu jijini Dar es Salaam. Hapa anaelezea namna alivyopokea maamuzi hayo;

“Mamuzi yalikuja baada ya kupoteza mechi. Hayakuwa mazingira yaliyonihusu na maandalizi ya mchezo yalivurugwa kuanzia ndani na si kwa sababu ya taaluma yangu.

"Sikupingana na maamuzi yao na wasimamizi kupitia mtendaji mkuu alinifahamisha juu ya uamuzi wao baada ya mchezo ule, hakuna kingine."


UJIO WA MABADI

Siku chache kabla ya kufutwa kazi, Yanga ilimtambulisha kocha msaidizi, Mmalawi, Patrick Mabedi na baada ya muda ikaachana na Folz na kuachiwa kikosi kabla ya ujio wa kocha mpya, Goncalves.

Hata hivyo, anafichua ujio wa kocha huyo msaidizi halikuwa pendekezo lake na hakuhitaji mabadiliko yoyote katika benchi lake.

“Hakuja kwa mapendekezo yangu. Nilikuja na msaidizi wangu mwenye taaluma na muungwana sana. Mchango wake kwenye timu ulikuwa wa kiwango kikubwa sana kila siku. Sikuhitaji wala kuomba mabadiliko yoyote."


FOL 02

AWABADILISHA ANDABWILE, MWAMNYETO

Nahodha na beki wa Yanga, Bakari 'Nondo' Mwamnyeto alikuwa akisugua benchi hasa kutokana na uwepo wa Dickson Job na Ibrahim Hamad 'Bacca'.

Hata hivyo, baada ya ujio wa Folz, Mwamnyeto pamoja na kiungo mkabaji Aziz Andabwile walianza kupata nafasi ya kucheza na anakiri hakuwa na tatizo na wachezaji na hata alifurahi kufanya nao kazi na anajivunia kuwabadilisha nyota hao na wengine.

“Ndiyo, kila kitu kilikuwa sawa. Nina furaha na fahari kwa kuwapaa mwanga baadhi yao kama vile Aziz (Andabwile) na kurudisha utawala wa Bakari (Mwamnyeto). Kwangu ni jambo zuri kumfanya kila mtu kujisikia ni muhimu. Hii itabaki hivyo milele," anasema na kukiri maisha ya Tanzania yalkimfanya awe na furaha kwani ni nchi nzuri na alikutana na watu wazuri wengi na kila kitu kilikuwa safi, akikitaja pia Ugali ndiyo chakula kilichomvutia zaidi akiwa nchini.


ISHU YA KUCHEKA NI HIVI

Ilifika wakati mashabiki wa soka nchini wakalipa jina soka lake analofundisha Yanga 'Soka Mnunu'. Ni kwa sababu kocha huyu amekuwa mgumu sana kucheka au kutabasamu hata pale timu inapopata matokeo mazuri na hasa bao linapofungwa katika kushangilia.

Hata hivyo, anafichua aliposhinda Ngao ya Jamii alicheka na kutabasamu na kama angeendelea kuwepo basi wangemwona sana akifanya hivyo na yanayosemwa ni maneno tu.

"Hakuna ishu hapo. Nina tabasamu sana. Kuna wakati wa kutabasamu, pia nilifanya hivyo niliposhinda Ngao ya Jamii. Lakini msijali, mtaniona nikitabasamu mara nyingi katika siku zijazo, usijali," anasema na kuongeza;

“Ninapokuwa kazini, ninafanya kazi, hivyo yaani. Naichukulia kazi yangu kwa uzito  kwa sababu ninaliheshimu soka na malengo. Unajua hii ni biashara, hivyo unatakiwa ufurahie matokeo mazuri na siyo kucheka wakati wa kutafuta mafanikio.”