Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ulipo mtihani wa Yanga CAF ikimkosa Mzize

MTIHANI Pict


ILIANZIA kwa mashabiki wa Yanga kuona kwamba timu imeangukia katika kundi gumu kwenye mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kuthibitisha tathimini hiyo uongozi wa klabu hiyo ukatoa kauli kama hiyo huku ukiweka matumaini kwamba inawezekana kwao kuvuka salama.


Yanga imeangukia kundi D lenye timu kama bingwa wa kihistoria wa mashindano hayo Al Ahly ya Misri, JS Kabylie kutoka Algeria na AS FAR Rabat ya Morocco.


MTI 02

UGUMU WA KUNDI

Katika kundi hilo  ukitazama juu ya rekodi utaona ni Yanga pekee ambayo haijawahi kuchukua ubingwa huo wa Ligi ya Mabingwa kwani utaanzia kwa Ahly iliyochukua taji hilo mara 11 na mara ya mwisho ililibeba mara mbili mfululizo misimu ya 2023 na 2024, JS Kabylie ikilibeba mara mbili miaka ya 1981 na 1990 huku AS FAR ikibeba mara moja (1985).

Ukitazama takwimu hizo kisha ukilinganisha na zile za Yanga utabaini wasiwasi uliopo, lakini uhalisia wa soka unakosa mashiko hayo na kubaki kwamba lolote linaweza kutokea kwani Yanga inaweza kujipanga na kutumia tathimini hiyo ya kuonekana mnyonge, ikajipanga kisha kufanya vizuri bila kujali ukubwa wa wapinzani. Hilo ndilo soka.

Unyonge wa Yanga unaonekana kwenye baadhi ya maeneo katika kujipanga kwani ni lazima iangalie ubora wake uko wapi na upungufu ulipo kisha kufanyia kazi haraka kabla ya kuanza kwa mechi sita dhidi ya wapinzani itakaokutana nao.

Ili Yanga ifanye vizuri inatakiwa kuishi kwa hesabu ikijiongezea ubora kabla ya kuanza mchezo wa kwanza Novemba 21 itakapokuwa wenyeji wa AS FAR Rabat katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar. Hebu tuangalie wapi inatakiwa kurekebisha.


MTI 06

SAFU YA USHAMBULIAJI

Msimu huu tangu uanze Yanga kuna mchezo mmoja pekee ambao imetoka bila kufunga bao na ni ule dhidi ya Silver Strikers ya Malawi iliopoteza ugenini kwa bao 1-0, lakini siyo ishu kwani kufunga imefunga karibu mechi zote saba ambazo imecheza za mashi-ndano.

Shida kubwa ya Yanga ni kupoteza nafasi. Kikosi chake kinatengeneza nafasi nyingi, lakini washambuliaji hawapo kwenye utulivu wa kuzitumia kwa kiasi cha kutosha na kumbuka wanakwenda kucheza mechi ngumu ambazo hazitakuwa na utengenezwaji wa nafasi nyingi.

Mechi za makundi ni ngumu zinatakiwa ukipata nafasi kuanzia moja au mbili utumie zote au moja kati ya hizo huu na ndio mtihani ambao mabingwa hao wa Tanzania Bara wanakabiliana nao.

Mbaya zaidi siku chache kabla ya kuanza mechi hizo inapata taarifa mbaya ya kuumia na kufanyiwa upasuaji kwa mshambuliaji wake mahiri Clement Mzize aliyeumia goti na sasa atakuwa nje kaatika ya wiki nane hadi kumi.

Kuumia kwa Mzize kunaifanya Yanga kubaki na Prince Dube akiwa kwenye presha kubwa ya ukame wa mabao, lakini pia Andy Boyeli ambaye bado hajaonyesha kitu kikubwa tangu asajiliwe dirisha lililopita la usajili akiendelea kujitafuta huku akipata muda mchache wa kucheza.

Kocha wa kikosi hicho, Pedro Goncalves atahitaji utulivu wa akili kuhakikisha anapata dawa ya kuwaongezea ubora washambuliaji alioano kama timu hiyo itashindwa kusajili mshambuliaji mpya mwenye makali kuisaidia kwenye vita ya utupiaji nyavuni. Angalia hesabu za Ahly juzi tu ilikuwa kwenye hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji Ibrahim Diabate kutoka GAIS ya Sweden kwa kiasi cha Dola 1 milioni (takriban Sh2.6 bilioni) ili akaongeze nguvu kikosini.

MTI 03

KIVULI CHA AUCHO

Presha nyingine ya Yanga ni eneo la kiungo mkabaji ambalo timu hiyo imeachana na Khalid Aucho ikiona kama jamaa hawezi kuisaidia akiletwa Moussa Bala Conte, lakini bahati mbaya licha ya kuvuma amechelewa kuwaka na amekuwa akisugua sana benchi kuliko kuanza kikosini. Conte anasugua benchi wakati Aucho aliyeachwa akitwanga sawasawa Singida Black Stars iliyomdaka haraka. Tumaini pekee kwa Yanga linabaki kwa mzawa Aziz Andabwile ambaye angalau ameshtua kwa kuonyesha ubora baada ya kuaminiwa lakini bado naye anakosa nguvu na uwezo wa aina ya Aucho ambaye inawezekana hakuwa mzuri sana kukaba, lakini alikuwa na uwezo wa kusogeza timu mbele kwa pasi murua.

MTI 05

MZIMU WA FOLZ

Yanga inaingia kwenye mechi hizo ikitoka kuachana na kocha Romain Folz iliyeanza naye msimu, lakini ikiligomea soka lake ikiaamini ni kama timu ilikuwa inashinda kwa tabu  tofauti na makocha waliomtangulia. Presha hiyo ya mashabiki wa Yanga bado haijawatoka ikiwa imeshuka tu kidogo huku wakisubiri kuona Goncalves atakuja na kipi ambacho kitawatuliza nafsi na kusema wanakwenda kupambana na Waarabu watatu kisha watoboe.

MTI 04

MAAJABU, REKODI YA GONCALVES

Goncalves si kocha mdogo anajua kipi Yanga wanasubiri kutoka kwake. Bahati mbaya wakati ndio utamtatiza, lakini kama wachezaji wake wakimsikiliza na kumuelewa falsafa zake watabadilisha mambo kwa kucheza mechi za kimataifa kwa mkakati mkubwa.

Goncalves akiwa na timu ya taifa ya Angola rekodi zinaonyesha matokeo bora zaidi dhidi ya timu za Afrika Kaskazini ni sare tu hakuwahi kushinda kama ambavyo mara ya mwisho alipogoma kupoteza dhidi ya Misri  Novemba 12, 2021 akitoka sare ya bao 1-1, lakini wakati mwingine akipoteza. Uzuri ni kwamba Yanga imewahi kuifunga Ahly kwa bao 1-0 mwaka 2014 hapa nchini kwa bao lililofungwa na beki wa zamani Nadir Haroub Cannavaro ukiwa ni ushindi pekee kwao ndani ya mechi 12 walizokutana wakipoteza mechi saba, sare nne lakini wakiwa hawajawahi kukutana na JS Kabylie wala  AS FAR Rabat


PRESHA YA MASHABIKI

Ili kuisadia timu yao wanachotakiwa kufanya mashabiki wa Yanga ni kuwa nyuma ya kikosi hicho kwa kukipa nguvu, kuzitumia mechi za ligi ya ndani kuwajenga wachezaji kwa kutuliza presha ili waende kufanya vizuri mbele ya Waarabu hao.