Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dada usiende kanisani kama ‘mbibi’

Muktasari:

  • Mdada anayejua kuvaa anajua siri kubwa si kuvaa nguo nyingi, bali ni kuchagua vazi linaloendana na mazingira, mwili wake na tukio lenyewe.

KUNA sehemu ukifika unatakiwa ujue umefika wapi, kwa nini umefika na unapaswa kuonekana vipi. Kanisani ni moja ya sehemu hizo, kwa sababu si uwanja wa mashindano ya mavazi, pia si sababu ya kwenda ukiwa umejifunika kuanzia kichwa mpaka vidole kana kwamba unaenda kukutana na baridi kali!

Mdada anayejua kuvaa anajua siri kubwa si kuvaa nguo nyingi, bali ni kuchagua vazi linaloendana na mazingira, mwili wake na tukio lenyewe.

Kanisani unaweza kuvaa kwa heshima, ukawa nadhifu, ukawa wa kisasa na bado ukaonekana smati bila kugeuza ibada kuwa sehemu ya kuonyesha kila kilichopo kwenye kabati.

Wapo wanaodhani kwenda kanisani maana yake ni kuvaa nguo iliyopitwa na wakati, rangi yoyote na viatu vya aina yoyote ilimradi tu mwili umefunikwa.

Hapana! Unaweza kuwa mstaarabu wa mavazi na bado ukawa na mvuto wa kipekee. Siri ipo kwenye uchaguzi wa vazi, mpangilio wa rangi, urefu, viatu na namna unavyoviunganisha.


GAUNI REFU

Gauni refu ni moja ya mavazi ambayo yanaweza kumfanya mdada aonekane mwenye hadhi kanisani bila kuonekana kama amejitahidi kupita kiasi.

Chagua gauni linalokaa vizuri mwilini, lisilobana kupita kiasi na lenye muonekano wa kawaida lakini wa kifahari.

Rangi kama nyeusi, navy bluu, rangi ya maziwa, kahawia, maroon au kijani iliyotulia zinaweza kutoa muonekano wa kuvutia. Unaweza kulivaa na viatu vya kisigino kifupi au vya kawaida, kisha ukaongeza pochi ndogo inayolingana na vazi.


SKETI NA BLAUZI

Kama kuna mchanganyiko ambao hauwezi kukusaliti kirahisi, basi ni sketi na blouse. Sketi ya urefu wa wastani ikiambatana na blauzi yenye muundo mzuri inaweza kukupa muonekano wa mwanamke mwenye mpangilio. Usilazimishe rangi nyingi kwa wakati mmoja. Sketi ya rangi tulivu na blouse yenye rangi inayokamilishana nayo inaweza kufanya kazi kubwa zaidi kuliko kuchanganya kila rangi iliyopo sokoni.


SURUALI

Kwa mdada anayependa suruali, bado unaweza kwenda nayo kanisani na ukaonekana mwenye mvuto. Chagua suruali yenye kukaa vizuri, isiyobana kupita kiasi na iendane na blouse au shati refu.

Suruali ya kitambaa yenye kiuno kizuri inaweza kuonekana nadhifu sana ikiwa imevaliwa na blouse iliyopangiliwa vizuri. Epuka suruali iliyochanika, yenye michoro mingi au inayokufanya ushindwe kukaa kwa utulivu.


KOTI REFU LINAWEZA KUBADILISHA KILA KITU

Wakati mwingine huhitaji kununua nguo mpya ili kupata muonekano wa tofauti. Koti refu (Blazer) zuri linaweza kubadilisha kabisa vazi ulilonalo.

Unaweza kuvaa blauzi rahisi na sketi au suruali, kisha ukaongeza koti refu lenye rangi tulivu. Ghafla, vazi lilelile linapata sura nyingine. Hii ni moja ya siri za mvuto si lazima kila kitu kiwe kipya, bali ujue kukichanganya.

RANGI ZISIZOPIGA KELELE

Kanisani si lazima rangi zote za upinde wa mvua zikukute siku moja. Rangi mbili au tatu zinazokamilishana zinatosha kabisa.

Rangi ya maziwa na kahawia, nyeupe na bluu bahari, nyeusi na pinki iliyotulia na nyeupe ni baadhi ya mchanganyiko unaoweza kukupa mwonekano wa kike, safi na wa kisasa.


VIATU NAVYO VINAONGEA

Unaweza kuvaa nguo nzuri sana, lakini ukachagua viatu visivyolingana nayo na ukaharibu picha nzima. Kanisani viatu vya kisigino kifupi, vya wastani, viatu vya chini au sendo zenye muonekano wa nadhifu vinaweza kufanya kazi vizuri. Muhimu ni viatu viwe safi na uendane navyo bila kuteseka. Mvuto si kuvaa kisigino kirefu kiasi cha kushindwa kutembea vizuri baada ya ibada!


POCHI NZURI

Pochi ndogo au ya wastani inaweza kukamilisha vazi lako. Huhitaji kubeba begi kubwa linalofanana na la safari ya siku tatu.

Chagua pochi inayokwenda na rangi ya vazi au viatu. Kama nguo yako tayari ina michoro mingi, pochi ya kawaida inaweza kutuliza muonekano.

USIACHE HIVI

Pete, hereni, saa, bangili au mkufu vinaweza kuongeza uzuri, lakini usiruhusu mapambo yakaanza kushindana na wewe mwen yewe. Ka ma u mevaa blouse yenye maelezo mengi shingoni, huenda mkufu mkubwa usihitajike. Kama vazi lako ni rahisi, hereni nzuri au saa inaweza kuwa ndiyo kitu kinachokamilisha muon ekano.


NYWELE

Classic haianzi kwenye nguo pekee. Nywele zilizopangiliwa vizuri na makeup ya wastani vinaweza kufanya vazi la kawaida lionekane la gharama. Kwa kanisani, si lazima makeup iwe nzito. Muonekano safi, ngozi iliyopangiliwa, midomo yenye rangi tulivu na nywele zilizotengenezwa vizuri vinaweza kutosha.