Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chilambo na hadithi ya Bocco, Nyoni

CHILAMBO Pict

Muktasari:

  • Jamaa anazima kweli msondo. Ukimpanga beki wa kulia anapiga kazi. Ukimpeleka kushoto anatwanga vile na kuna wakati anaingia hadi kati kupiga pasi za upendo.

WANASIMBA sasa hivi huwaambii kitu kwa huyo mchezaji wao Nathaniel Chilambo waliyemsajili kutoka Azam FV katika dirisha kubwa la usajili.

Jamaa anazima kweli msondo. Ukimpanga beki wa kulia anapiga kazi. Ukimpeleka kushoto anatwanga vile na kuna wakati anaingia hadi kati kupiga pasi za upendo.

Na kwa kuangalia mechi zilizochezwa hadi sasa, hapa kijiweni tumempitisha kama ndio usajili bora wa mchezaji mzawa uliofanywa wakati wa usajili labda huko mbele asionyeshe hiki anachofanya sasa.

Ghafla jamaa mmoja hapa anatukumbusha kule Azam FC, Chilambo hakuwa na uhakika wa namba mbele ya vipenzi viwili kwenye timu hiyo Pascal Msindo na Lusajo Mwaikenda.

Msindo ndio amekuwa akipangwa kushoto na beki wa kulia anapangwa Mwaikenda ambaye ndio nahodha wa timu hiyo jambo ambalo lilimnyima fursa kubwa Chilambo kucheza kikosi cha kwanza.

Mwingine hapo anatushtua kinachofanywa na Chilambo sio kigeni kwa sababu Simba imekuwa na bahati na wachezaji ambao inawachukua kutoka Azam FC.

Mwaka 2017 katika dirisha la usajili, Simba iliwabeba John Bocco, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na Aishi Manula ambao walishindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba na Azam baada ya kuitumikia kwa muda mrefu.

Jamaa waliibeba sana Simba kuanzia katika mashindano ya ndani na hadi ya kimataifa na wakaweka heshima kubwa nchini inayowafanya hadi sasa waonwe kama malijendi wa Simba.

Bocco aliifungia Simba mabao kibao na akawa hadi nahodha na Aishi Manula akawa ndio kipa tegemeo hadi alipoondoka ndani ya timu hiyo.