Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CECAFA acheni mambo ya kizamani bhana

WAKO 01

Muktasari:

  • Kitu kama kilichofanyika katika kuamua timu ipi iongoze kundi C la kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya Umri wa miaka 17 (AFCON U-17) ni jambo la kizamani kwa kweli.

HUU ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kati ndio maana bado uko nyuma kimafanikio kisoka kulinganisha na kanda nyingine Afrika.

Kitu kama kilichofanyika katika kuamua timu ipi iongoze kundi C la kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya Umri wa miaka 17 (AFCON U-17) ni jambo la kizamani kwa kweli.

Eti Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) liliamua kurusha shilingi ili kuamua timu ipi iongoze kundi hilo kati ya Somalia na Tanzania ‘Serengeti Boys’.

Yaani ilivyokuwa ni kwamba timu hizo zimelingana pointi ambapo kila moja imemaliza mechi mbili ikiwa na pointi nne baada ya kutoka sare moja na kushinda moja.

Zimefunga mabao sawa ambapo kila moja imepachika mabao matatu na imefungwa bao moja hivyo CECAFA ikaona irushe shilingi kupata mshindi ambapo Somalia ikaongoza kundi.

Hili sio jambo sahihi na hatusemi hivyo kwa sababu sisi ni Watanzania na timu yetu haijafanikiwa kuongoza kundi ila kinachouma ni namna ambavyo CECAFA inavyoutoa mpira kutoka kuamriwa kwa kinachotokea uwanjani hadi mambo ya mezani.

Kuna njia nyingi ambazo ingeweza kuzitumia kuamua mshindi kama vile kuangalia timu yenye nidhamu nzuri au hata kuchezwa mechi baina ya timu hizo zilizolingana matokeo.

Lakini yenyewe ikaona irushe shilingi utadhani timu zilikuwa zinachagua nani aanzishe mpira au zinachagua magoli kumbe inatafuta timu ya kuongoza kundi.

CECAFA iachane na haya mambo ya kuamua mshindi mezani bhana sisi tumeshavuka huko inakotaka kuturudisha.