Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shilingi yainyima Serengeti Boys tiketi AFCON U-17

Muktasari:

  • Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) liliamua kutumia njia ya kurusha shilingi kuamua timu ipi itaongoza kundi C la mashindano yake ya kuwania kufuzu AFCON U-17.

Uamuzi wa kurusha shilingi umeifanya timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ikose nafasi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U-17) 2027.

Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) liliamua kutumia njia ya kurusha shilingi kuamua timu ipi itaongoza kundi C la mashindano yake ya kuwania kufuzu AFCON U-17.

Hiyo ilikuwa ni baada ya Serengeti Boys na Somalia kuwa sawa kwa idadi ya pointi, mabao ya kufunga na mabao ya kufungwa katika mechi mbili ambazo kila moja ilicheza.

Timu hizo kila moja imemaliza ikiwa imekusanya pointi nne baada ya kushinda mechi moja na kutoka sare moja.

Kila moja imefunga mabao matatu na kila timu imemaliza mechi mbili ikiwa imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara moja.

Kutokana na hilo, CECAFA iliamua kutafuta kinara wa kundi kwa kurusha shilingi ambapo Somalia iliibuka mshindi na hivyo Serengeti Boys kuaga rasmi.

Somalia sasa imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ambayo pia itaungana na timu za Uganda, Rwanda na Ethiopia.

Timu tatu zitafuzu AFCON U-17 2027 ambazo mbili ni zitakazoingia hatua ya fainali na moja itakayomaliza katika nafasi ya tatu.