Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick ana siri gani kuchapa makocha wakubwa

CARRICK Pict

Muktasari:

  • West Ham ndiko mahali Carrick alikobadilishwa na kucheza eneo la kiungo, ambalo amekuwa mahiri na kubeba mataji ya kutosha akicheza kwenye eneo hilo baada ya kujiunga na miamba ya soka ya Old Trafford, Manchester United.

MANCHESTER, ENGLAND: WAKATI yupo shule anasoma, hadi kipindi anakwenda kujiunga na West Ham United, Michael Carrick alikuwa akicheza nafasi ya mshambuliaji wa kati.

West Ham ndiko mahali Carrick alikobadilishwa na kucheza eneo la kiungo, ambalo amekuwa mahiri na kubeba mataji ya kutosha akicheza kwenye eneo hilo baada ya kujiunga na miamba ya soka ya Old Trafford, Manchester United.

Huko Man United, Carrick ni gwiji. Na sasa akiwa amerudishwa kwenye kikosi hicho kama kocha wa muda hadi mwisho wa msimu huu, rekodi zake kwenye ukocha wa kuinoa miamba hiyo ya Old Trafford ndicho kitu kinachoshtua wengi.

Carrick anaonekana kuwa kiboko ya makocha wenye majina makubwa kwenye Ligi Kuu England.

CARR 01

Carrick ameiongoza Man United kwenye mechi nne tu, lakini viwango vyake alivyovionyesha kwenye mechi alizokutana na makocha mahiri, ambao hakuna hata mmoja aliyepata matokeo ya ushindi dhidi yake ni kitu kinachovutia wengi, akishinda mara tatu na sare moja. Ni rekodi ya aina yake na ya kipekee.

Kocha huyo wa Man United amemwongeza mshindi mara sita wa Ligi Kuu England, Pep Guardiola kwenye orodha yake ya makocha mahiri ambao amewachapa wakati Man United ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City uwanjani Old Trafford, Jumamosi iliyopita.

CARR 02

Kama ambavyo alivyobadilika kutoka kuwa mshambuliaji wa kati hadi kucheza kiungo wa kati, Carrick aliibadilisha Man United kwa kasi ya ajabu baada ya kurithi kikosi kilichoonekana kukata tamaa chini ya mtangulizi wake, Ruben Amorim.

Carrick alirudi kwenye mfumo wa kutumia mabeki wanne, huku akimtumia kila mchezaji kwenye nafasi yake anayocheza kwa ubora, ambapo Luke Shaw alicheza beki wa kushoto, Diogo Dalot alicheza beki wa kulia, Kobbie Maino kwenye kiungo ya kati na Casemiro, huku Bruno akicheza Namba 10, Amad kwenye wingi ya kulia, Patrick Dorgu kwenye wingi ya kushoto, huku akimpanga Bryan Mbeumo kwenye nafasi ya Namba 9 bandia, baada ya kuamua kuwaanzishia benchini washambuliaji Benjamin Sesko na Joshua Zirkzee.

Matheus Cunha, naye alianzia benchi kabla ya kuingia na kuleta mabadiliko makubwa mchezoni.

Carrick alichofanya Jumamosi ni mwendelezo wa rekodi tamu dhidi ya makocha mahiri tangu alipoinoa Man United kwa awamu ya kwanza mwaka 2021.

CARR 03

Carrick alipata matokeo mazuri dhidi ya Unai Emery, ambaye kwa sasa ni kocha Aston Villa, kipindi hicho alipokuwa Villarreal ambapo timu yake ilikubali kipigo cha mabao 2-0 katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Carrick pia aligomea Chelsea na kutoka sare ya 1-1 uwanjani Stamford Bridge wakati huo ilipokuwa chini ya kocha wa sasa wa England, Thomas Tuchel, kabla ya kuichapa Arsenal ya kocha Mikel Arteta mabao 3-2 katika Ligi Kuu England ambapo ilikuwa mechi yake ya mwisho kabla ya Ralf Rangnick kuja kukabidhiwa mikoba ya kuinoa miamba hiyo ya Old Trafford. 

Na sasa amerudi tena Old Trafford kwa mara ya pili, akiwa kocha wa muda, Carrick anasubiri nafasi nyingine ya kuendeleza mwanzo wake mzuri wakati atakapokabiliana na Arteta katika mchezo wa Ligi Kuu England utakaofanyika Emirates, Jumapili.

Je, Carrick ataendeleza ubabe wake kwa makocha mahiri? Je, atamtesa tena Arteta na kumtibulia kwenye harakati zake za kukimbizia ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu? Arsenal kwa sasa imeweka pengo la pointi saba kileleni kwenye msimamo wa ligi dhidi ya timu Man City na Aston Villa, huku ikiiacha Man United kwa pointi 15 ikiwa kwenye nafasi ya tano katika msimamo huo. Mambo ni moto.