Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United ugonjwa upo eneo hili!

Muktasari:

  • Wengi walikua ama kwa kuipenda au kuichukia kwa sababu ya utawala wake mkubwa kwenye soka.

MANCHESTER, ENGLAND: KITU kimoja tu kuhusu Manchester United, imechosha. Wote wanaichukulia kama klabu kubwa zaidi England na kwa hoja nzuri, pia inaweza kuwa ya kwanza au ya pili kwa ukubwa duniani.

Wengi walikua ama kwa kuipenda au kuichukia kwa sababu ya utawala wake mkubwa kwenye soka.

Lakini leo hii ni nini? Man United imekuwa kama Mickey Mouse au Banter.

Man United imegeuka kuwa timu ambayo inachekesha ukiwa umeshangazwa na ujinga wa ajabu walioufikia na kuufanya karibu kila wiki.

Kwa mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka 16, Man United ni kichekesho kikubwa. Ni mzaha mtupu.

Wamekuwa wakifanya makosa yaleyale mara kwa mara tangu Sir Alex Ferguson alipoondoka, na sasa wanafanya hivyo tena kupitia Michael Carrick.

Ilichukua muda, lakini Arsenal walipotaka kusonga mbele bila Arsene Wenger, walifanya nini? Alitoweka kabisa.

Mfaransa huyo anaweza kurudi Emirates wakati wowote anapotaka. Lakini hayupo tena kwenye picha ya maamuzi.

Hakuna kivuli kinachoning’inia wala hana sauti katika kinachoendelea chini ya Mikel Arteta.

Ferguson ndiye kocha mkubwa zaidi kuwahi kutokea. Lakini kwa nini viongozi wa Man United wanaendelea kumsujudia kila wakati?

Na bila shaka, kila Man United wanapogonga tawi jingine katika kuanguka kwao, kamera humuangazia gwiji wao akiwa kwenye jukwaa la wakurugenzi, akionekana kukataa kilicho mbele yake.

Darren Fletcher hakuwa na haja ya kumuomba baraka Fergie ili kuchukua kazi hiyo. Je, alifanya hivyo kabla ya kuchukua nafasi ya ukocha kwenye akademi?

Ferguson hafanyi kazi hapo, hana mchango wowote katika uendeshaji wa kila siku wa klabu. Haina maana kabisa.

Wachezaji hawatakuchukulia kwa uzito ukifanya hivyo. Lakini Fletcher na Fergie si tatizo halisi. Tatizo ni wale walioko juu kabisa, wanaofanya maamuzi yasiyosaidia timu na ya hovyo mara kwa mara. Awali walikuwa familia ya Glazer ndio tatizo na alipokuja Sir Jim Ratcliffe alionekana kama shujaa.

Lakini amejenga muundo wa uongozi wa kusikitisha. Man United inapaswa kuwa bora kuliko wote, lakini kwa muda mrefu sana hawajitendei haki hiyo iwe ni uwanjani wala nje ya uwanja. Unatafuta mkurugenzi wa kiufundi? Bila shaka Southampton ambako walimpata Jason Wilcox ndio mahali sahihi kwenda.

Kila mtu huko atakuambia jinsi mambo yalivyokwenda vizuri hivi karibuni. Kisha ilivuka jiji hadi kwa mahasimu wao wakubwa kumnyakua Omar Berrada kama mtendaji mkuu. Man City wanaendeshwa kikamilifu kama mashine. Lakini kama Berrada alikuwa mzuri sana, je, wangemruhusu aende Old Trafford? Bila shaka hapana. Lakini kosa kubwa zaidi lilikuwa Dan Ashworth. Ratcliffe aliweza kuajiri mtu mwenye historia halisi ya kazi, aliyefanya mabadiliko makubwa Brighton, Newcastle na timu ya taifa ya England. Na walifanya nini? Wakamtimua mara tu kulipoibuka harufu ya kutokubaliana maoni ilhali hicho ndicho klabu hii inahitaji hasa. Man United wanamhitaji sana mtu kama Ashworth aingie, avunje kabisa muundo wao na kujenga kitu kinachofanya kazi.

Lakini hapana. Kwa sababu hakubaliani na Wilcox na Berrada, basi tumwondoe na tuendelee na hawa wawili wasiojua wanachofanya.

Hao ndio waliounda vurugu za makocha ambazo Man United wanajikuta nazo leo. Kuanzia uamuzi wa kumfukuza Erik ten Hag baada ya kumpa mkataba mpya na matumizi ya mamilioni ya pesa kwa wachezaji wapya kufuatia ushindi wa Kombe la FA, hadi sasa kuwa na Carrick kama kocha wa muda baada ya kocha wa muda. Lakini hao si watakaobeba lawama.

Kuanzia Ten Hag, hadi Ruben Amorim, na sasa huenda Carrick ambaye licha ya kuwa mchezaji wa zamani wa Man United mwenye taaluma nzuri, amefanya machache sana kustahili nafasi hii. Hata hivyo, si yeye anayepaswa kushambuliwa na mashabiki.

Wakushambuliwa ni wale wale wanaoiendesha Manchester United kama West Ham United. Swali wanalopaswa kujiuliza ni rahisi sana: “Ni ushahidi gani tumeonyeshwa hadi sasa unaotufanya tuamini kuwa umiliki huu na wakurugenzi wa michezo wanaweza kufanya mambo sawa?”

Tupewe hata mfano mmoja tu, ili tuseme: “Hapo wamefanya sawa.” Sote tunasubiri kuona Man United ikididimia siku hadi siku.