Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bado sijamuelewa Gamondi kwa Nado

GAMONDI

Muktasari:

  • Hapa ndio anapowapa nafasi ya kutamba wale ambao waliamini alikosea kwa kutomuita Naldo mwanzoni kwa vile waliyempigania amecheza mbele ya kocha ambaye hakuona haja ya kumuita mwanzo.

MIGUEL Gamondi ametuchanganya sana katika mechi mbili zilizopita za Taifa Stars ambazo ilicheza dhidi ya Nigeria.

Ametuchanganya kupitia fundi wa mpira Iddi Selemani ‘Nado’ ambaye amewaka kinoma msimu huu akiwa na wauza aiskrimu wa Chamazi, Azam FC.

Kwanza alipoita kikosi kwa ajili ya mechi hizo mbili dhidi ya Nigeria, hakulijumuisha jina la Naldo jambo ambalo halikupokelewa vizuri na watu wengi kwa vile jamaa anaonyesha kiwango bora pale Azam hivi sasa.

Baada ya kelele kuwa nyingi, akaamua kumuongeza kimyakimya kikosini mchezaji huyo tukaja kushtukia tayari mchezaji yupo kambini na wenzake wakijiandaa kwa ajili ya mechi hiyo.

Sasa sisi tunavyofahamu, mchezaji kama hajaitwa katika kikosi cha timu ya taifa kwa nyakati fulani, anakuwa hayupo katika mipango ya kocha kwa wakati huo na walioitwa ndio wanakuwa machaguo ambayo benchi la ufundi limejiandaa kuyatumia.

Hivyo hata Nado alivyoongezwa kimyakimya tukajua ni suala la kujaribu kuwatuliza tu mashabiki lakini sio kipaumbele cha kwanza cha kocha kuelekea mchezo husika.

Cha ajabu wale ambao waliitwa kikosini kabla ya Nado wakajikuta wakikaa benchi na mchezaji huyo akaanza kikosini katika mechi moja na nyingine akaingia uwanjani kutokea benchi.

Sasa kinachotuchanganya ni kwamba ilikuaje Gamondi ghafla akamuona Naldo kama mchezaji muhimu hadi akaamua kumchezesha na wakati alipoita kikosi kwa mara ya kwanza hakumchagua?

Hapa ndio anapowapa nafasi ya kutamba wale ambao waliamini alikosea kwa kutomuita Naldo mwanzoni kwa vile waliyempigania amecheza mbele ya kocha ambaye hakuona haja ya kumuita mwanzo.