Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BABA MODEST: Muokoeni mwanangu jamani!

Modest Pict
Modest Pict

Muktasari:

  • Beki huyo wa kushoto wa zamani, kwa sasa yupo hoi kitandani mjini Kigoma na Mwanaspoti lilienda kufanya naye mahojiano maalumu yaliyozaa makala hayo akiomba kupata msaada, lakini akifichua mambo mengi aliyopita hadi wakati huu akikosa kulioa jua kwa miaka mitano kutoka na maradhi aliyonayo.

KATIKA toleo la jana, tuliona namna nyota wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, aliyetamba na timu za Pamba, Simba, Yanga Mlandege, Mtibwa Sugar na Taifa Stars, Alphonce Modest akifafanua sababu ya kupenda kwake kuwa mbali na mitandao ya kijamii.

Beki huyo wa kushoto wa zamani, kwa sasa yupo hoi kitandani mjini Kigoma na Mwanaspoti lilienda kufanya naye mahojiano maalumu yaliyozaa makala hayo akiomba kupata msaada, lakini akifichua mambo mengi aliyopita hadi wakati huu akikosa kulioa jua kwa miaka mitano kutoka na maradhi aliyonayo.

Leo anaendelea kufunguka mambo mengine, lakini akieleza safari nzima ya mafanikio ya maisha ya soka, ambayo yamebaki kuwa historia inayomuumiza kila anapoitafakari wakati akiugulia kitandani, huku baba mzazi wa staa huyo wa zamani na familia kwa ujumla wakitoa kauli nzito juu ya afya ya Modest. Endelea...!


KAULI YA BABA MZAZI

Baba mzazi wa staa huyo, anawaomba Watanzania angalau wamsaidie pesa za kumlipa daktari wa mazoezi na mwanasaikolojia, ili kuirejesha akili yake, licha ya kupitia magumu anaweza akayafurahia tena maisha yake.

“Mwaka 2018 alinipigia simu, baba naumwa kama mtaendelea kukaa kimya na hamtakuja kuniona, basi nikifa msije nitazikwa huku huku, kauli yake ilinishtusha sana. Nikafunga safari hadi Dar es Salaam, nikamkuta anasukumwa kwenye kiti cha wagonjwa, hali iliyonishtua sana, maana niliondoka na Sh150,000 nikijua nakwenda kumchukua na kurejea nyumbani,” anasema Mama Modest na kuongeza;

“Nilikaa jijini Dar es Salaam miezi mitatu, kisha tukachangiwa nauli ingawa kuna mtu aliipiga Sh700,000 ya kwanza kabla haijatufikia na Sh500,000 ambayo pia ilichangwa bila kufika kwetu, hivyo tukaondoka na Sh200,000 ambayo tulikabidhiwa mkononi tukiitumia kama nauli kurudi Kigoma, hao watu siwezi kuwataja, maana mwenyewe hataki kuwaelezea.

“Mimi nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi hapa Kigoma ambayo alinitafutia kabla ya kuanza kuumwa, sasa nimestaafu, nashindwa kupata pesa angalau anapolalamika misuli, tumpate daktari wa kumlipa ili kumsaidia, ndio maana nimeamua kutoka kuomba msaada kwa Watanzania.

“Najua hataki, ila mimi ni mzazi, ninaposhindwa kumsaidia najiona ni bure kabisa, kuna wakati nikikaa dirishani kwake, namsikia akisema Mungu nichukue nimechoka na haya maisha, najikuta naumia sana, ila nikisema nitetereke nitazidi kumchosha, kuna wakati anahitaji kitu, naenda hata kukopa ili tu nimpatie.”

Anasema kijana wake huyo ni mzaliwa wa kwanza, ambaye familia ilikuwa inamtegemea kwa kila jambo, kitendo chake cha kulala kitandani, kimewarudisha nyuma.

Mzee huyo anasema kuna wakati kijana wake huwa anamsimulia ndoto tofauti ambazo wakati mwingine haelewi zina maanisha kitu gani.

“Ukiachana na ndoto yake aliyoota wakati anaanza kuumwa, miezi michache aliniambia, aliota yupo na watu wengi, ila wenzake wana vyeti yeye hana, wakati wanakimbia kuingia katika lango, kuna mmoja akadondosha cheti chake akakichukua yeye, ila alipofika getini kukaguliwa akarudishwa na kuambiwa hicho siyo cheti chako, rudi kakitafute, sasa sielewi inamanisha nini, naishia tu kumuombea kwa Mungu,” anasema.

Anasema kwa sasa anamtegemea binti yake Teddy anayefundisha Shule ya Msingi ya binafsi, akipokea mshahara ndipo chakula kinunuliwe na kufanya matumizi mengine ya kumsaidia kaka yake.


FAMILIA NAYO

Kwa upande wa mdogo wake, Augostino anasema alikuwa anafanya kazi katika kiwanda cha Mtibwa, alikuwa mkusanya data shambani na alitafutiwa na Modest.

“Wakati baba anakuja naye Kigoma, mimi nilirudi Morogoro kazini, baada ya miezi kadha, baba alinipigia simu niache kazi ili nije nimuuguze kaka yangu kama kijana wa kiume, nikafanye hivyo hadi sasa napitia changamoto ngumu ya kiuchumi.

 “Nimekaa na kaka tangu akiwa Mtibwa, nilimuuguza katika hospital ya taifa ya Muhimbili, hivyo najua changamoto alizozipitia, lakini amekuwa hataki kabisa mambo ya media, anasema haina maana tena katika maisha yake, watu kutaka kujua maisha yake.

“Hapa tunapokaa ni yeye alinunua, alikuwa na mpango wa kubakarabati na kujenga nyumba nyingine ya familia uwanja ambao aliambiwa kuna mtu alitangulia kulipa, hivyo pesa yake ikaenda bure.”

Anasema kuna wakati anamwita mdogo wake na kumwambia mikono yake ingekuwa inafanya kazi, siku moja wangemkuta ameshakufa, maana amechoshwa na mateso.

“Kuna hospitali ya hapa Kigoma huwa tunakwenda, tukipata pesa kuna dawa anatumia, kama juzi tulishindwa kulipia matibabu, hivyo akabakia na maumivu yake, ndiyo maana familia iliamua kuweka jambo hilo wazi.”

Mbali na hilo, anasema kipindi mama yao anafariki dunia mwaka 2021, kaka yao alipata maumivu makubwa, maana ndiye alikuwa rafiki yake mkubwa.

“Mama alikwenda kuuguziwa Dar es Salaam, baada ya kusikia msiba wake, ilikuwa ngumu kumwambia kaka msiba huo, ingawa ni kama alikuwa anaweweseka na alikuwa anauliza ni kitu gani kimetokea, alipoambiwa ukweli, alikaa kimya kama wiki nzima, mkienda mnaona machozi yanamtoka tu,” anasema.

Mdogo wake wa kike, Teddy anasema; “Anasema kaka yake aliporudi Kigoma ilikuwa usiku, hivyo nikamuacha alale ili nimsalimie asubuhi, kuamkia nikamkuta anasukumwa katika kiti cha walemavu, nikamwambia kaka simama, akajibu siwezi kusimama mdogo wangu nililia sana na kushindwa kusalimiana naye.

“Nikamuuliza kaka kimekukuta nini, mara ya mwisho nilikusindikiza unaenda Dar es Salaam, ulikuwa mzima, akabakia kainamisha kichwa chini na hakunijibu lolote, baada ya muda akanikumbatia na kunifuta machozi, kisha akaniambia usilie ni mitihani ya Mungu.”

Anasema kitu kinachomuumiza kuna wakati kaka yake, anakuwa analalamika maumivu, kuna wakati wanashindwa pesa ya kumsaidia matibabu.

“Anaweza akakwambia nipashie maji ya kuoga, nikapasha nikimshika anasema niache najisikia kuumia, tofauti na muda ambao alikuwa anafanyiwa mazoezi, alikuwa anajisikia vizuri.”


SAFARI YA MAFANIKIO

Anasema wakati amekwenda kufanya majaribo Pamba, hakuchukuliwa kama mchezaji wa maana na kuna kiongozi alimpa Sh20,000 na akasema kabisa haoni kama ni mchezaji mzuri.

“Nikarudi nyumbani mara moja, wakati narejea kambini ilibidi baba yangu mzazi anipe nauli, kitendo kilichoniuma sana, maana wenzangu walipewa pesa ndefu na niliona, baada ya kufika kambini kocha aliniambia wazi haoni kama nitapata nafasi ya kucheza kirahisi kwani alikuwa haniamini, jambo lililonitia hasira ya kufanya mazoezi sana.

“Nilivyoanza kuaminiwa na safari yangu ya mafanikio kuanza, Pamba ilicheza michuano ya CAF, mechi ya kwanza dhidi ya Al Ahly iliyopigwa Misri, tukafungwa mabao 5-0 mimi sikupangwa, mechi ya marudiano Uwanja wa Kirumba, kocha akanipanga tukatoka suluhu, wakati huo Sanduy Kayuni alikuwa kocha wa Stars, akaniona na akaniambia umecheza vizuri sana,” anasema Modest na kuongeza;

“Baadaye akamfuata Nico Bambaga akamwambia yule kijana ni mchezaji mzuri, wakati anaita kikosi cha Stars likawemo na jina langu na nilichezea tangu mwaka 1991 hadi 1998, hivyo niliichezea miaka tisa, pia nikawa nahodha wa Stars kwa miaka miwili mwaka 1998/99 baada ya kwenda nje na sikucheza Stars na unahodha ukaishia hapo.”

Anaulizwa ni zipi sifa za nahodha? Anajibu “Awe na nidhamu, akubalike na wachezaji wenzake, awe kiunganishi baina ya wachezaji na viongozi, busara, hekima na awe tayari kuyatetea masilahi ya timu, kwangu mimi hizo sifa ni muhimu.”

Alitegemea baada ya kuonyesha kiwango mechi ya marudiano dhidi ya Al Ahly, kocha angepanga mechi ya kwanza ya msimu dhidi ya Yanga ambayo walifungwa mabao 2-1, mechi zote zilizofuata akawa anaanza kikosi cha kwanza.

Kutokana na kiwango chake kizuri, Simba ikavutiwa na uwezo wake mwishoni mwa mwaka 1993 ikamsajili.

“Kiwango nilichokuwa nakionyesha wakati naichezea Simba, mechi za Ligi Kuu na kimataifa, timu nyingi za nje zilileta ofa, ila viongozi hawakuwa tayari kuniachia, hivyo nikazikosa, baadaye nikaenda mimi mwenyewe kuomba kucheza timu ya Township Rollers ya Botswana ambako nilisaini bure miaka miwili na mshahara nikawa napewa Sh 200,000.

“Lengo langu la kusaini Township Rollers nilitaka iwe njia ya kuonekana na timu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini ambayo iliwahi kuhitaji huduma yangu nikiwa Simba, ni kweli ikapendezwa na huduma yangu, ila ikawa ngumu kupata barua ya kuachiwa huru kutoka Bostwana.

“Baada ya kumaliza mkataba na Township Rollers 2001, nikampigia simu Jamal Byser nikamwambia maisha huku ni magumu, nashindwa hata kununua kiatu cha kuchezea, akanitumia Sh1,000,000 ila haikuwa na maelezo, nikamwambia napanda basi narudi, akanishauri kwa kuwa mkeo katoka kujifungua mtoto wa pili apande ndege, mimi nikarudi na basi.

“Baada ya kufika Mtibwa Sugar, kuonana na Byser nikamuuliza pesa uliyonipa ilikuwa ya nini, akajibu ya usajili wa mwaka mmoja, sikuwa na cha kufanya kwa kuwa sikuwa na pesa kabisa, akanisaini mwingine akanipa Sh1,000,000 na akaniahidi nikifanikiwa kupata namba mbele ya wanaocheza, ataongeza masilahi.

“Nikacheza vizuri na kuwaweka benchi waliokuwa wanaanza kikosini, nikamfuata uliniahidi utabadilisha masilahi, akacheka tu na kuniambia tulimalizana.

“Nilistaafu kucheza soka wakati nacheza kikosi cha kwanza na kocha alikuwa ananitegemea mwaka 2003/4, sababu ilikuwa ni timu kushindwa kuchukua ubingwa, sikuona sababu ya kuendelea kucheza Mtibwa.”

Anasema viongozi wa Kagera Sugar, wakampigia simu akaipandishe timu kama kocha na anataja baadhi ya wachezaji aliowasajili ambao ni Vicent Barnabas na Amri Kiemba, ila nikaja nikaondolewa na Shirikisho la Soka kipindi hicho ilikuwa inaitwa FAT, nilikosa vigezo, kwani sikusomea ukocha.

“Baada ya hapo nikarejea zangu kufanya kazi kiwanda cha Mtibwa Sugar, ambako nikaanza dalili za kuumwa miguu hadi kupata ulemavu unaoniona nao hadi sasa naugulia tu kitandani,” anasema.


Itaendelea...