Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Argentina wametufundisha heshima kwa mastaa

ARGENTINA Pict

Muktasari:

  • Maana jamaa walilipa ukubwa jambo lao hadi wakatushawishi dunia nzima tukisubirie kwa hamu ili tuwe mashuhuda hata kupitia tivii na wakafanikiwa kiukweli.

LILE vaibu la Waagentina juzi wakati wa siku maalum ya kumuaga Lionel Messi lilikuwa bab kubwa bhana na lilibamba sana kwao na hata huko kwingine duniani.

Maana jamaa walilipa ukubwa jambo lao hadi wakatushawishi dunia nzima tukisubirie kwa hamu ili tuwe mashuhuda hata kupitia tivii na wakafanikiwa kiukweli.

Kuna wengine tulilazimika kukesha hadi alfajiri ili tulione na kuna nchi waliliona huku kwao kukiwa mchana muda ambao ni watu kutafuta tonge kwa ajili ya kulisha na kuendesha familia zao.

Pasipo kuweka unazi na ushabiki, Waajentina wana haki ya kumuaga kwa heshima yule Messi maana amefanya mambo makubwa sana kwa timu yake ya taifa na amekuwa kiongozi mzuri wa wenzake uwanjani.

Nadhani wote tunayajua mafanikio ya Argentina ambayo wameyapata kutokana na mchango wa Messi hivyo sio jambo la ajabu kwao kumpa heshima yake baada ya kuamua kuacha kuichezea timu yao ya taifa.

Kiufupi tu hapa kijiweni tunaamini tukio la kuagwa kwa Messi linatakiwa kutupa fundisho mataifa mbalimbali juu ya namna ya kuwapa thamani na kuheshimu mastaa wetu wa soka.

Unajua zipo nchi kama hapa Tanzania, zimekuwa zinawachukulia poa wachezaji wao nyota na wanaofanya mambo makubwa tofauti na walichokifanya Argentina kwa Messi.

Mfano ni hapa kwetu Tanzania jinsi watu wanavyomfanyia ndivyo sivyo Mbwana Samatta ambaye amefanya mambo makubwa katika soka la nchi hii na kuhamasisha wengi kupenda kusukuma kabumbu wakiamini watafuata nyayo zake.

Tuachane na wahenga wanaosema nabii hakubaliki kwao na tuwape thamani wanasoka na wanamichezo wetu wanaofanya vizuri.