Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anthony Joshua anavyokabiliana na hisia vifo vya rafiki zake

Muktasari:

Desemba, mwaka jana, Joshua alikuwa abiria wa gari lililohusika katika ajali ya barabarani kwenye barabara kuu nchini Nigeria, pamoja na Ghami na Ayodele, ambapo bingwa huyo wa zamani wa dunia wa uzito wa juu aliachwa na majeraha, huku wenzake wakifariki dunia.

LONDON, ENGLAND: BONDIA Anthony Joshua ‘AJ’ amezungumzia jinsi anavyoendelea kukabiliana na hisia kufuatia vifo vya marafiki zake Sina Ghami na Latif “Latz” Ayodele, miezi sita baada ya kunusurika katika ajali ya gari iliyogharimu maisha yao.

Desemba, mwaka jana, Joshua alikuwa abiria wa gari lililohusika katika ajali ya barabarani kwenye barabara kuu nchini Nigeria, pamoja na Ghami na Ayodele, ambapo bingwa huyo wa zamani wa dunia wa uzito wa juu aliachwa na majeraha, huku wenzake wakifariki dunia.

Tukio hilo lilitokea siku 10 baada ya Joshua kumshinda mwanamtandao wa YouTube, Jake Paul, katika pambano la maonyesho huko Miami, Marekani.

Joshua alirejea haraka mazoezini, na mwezi Aprili ilitangazwa kwamba atapigana na Kristian Prenga, Julai 25, huku pambano hilo litakalopigwa Saudi Arabia likitumika kama maandalizi kwa ajili ya pambano dhidi ya Tyson Fury baadaye mwaka huu.

Na wiki hii, Joshua na Prenga walizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa pambano hilo jijini London, ambapo AJ alianza kwa kuzungumza na The Independent na vyombo vingine vya habari akazungumzia kuhusu alivyokabiliana na matokeo ya ajali ya Desemba. Bondia huyo alisema: “Kila mtu ni tofauti. Kwa upande wangu, lazima niweke hisia zangu pembeni kwa sababu kwa kweli nawafikiria wazazi.

Hisia zangu zinaweza kuja baadaye, lakini nawaangalia sana wazazi wao na kuelewa kwamba lazima hali iwe ngumu zaidi kwao. Kwa hiyo, sifanyi jambo hili kuwa kuhusu mimi; ninafanya liwe kuhusu wao. Ninafanya liwe kuhusu mama na baba wa wale vijana wawili.

“(Kuzifukia hisia) siyo (njia bora) kwa kila mtu. Kila mtu hukabiliana na hali hii kwa njia tofauti, lakini nadhani kwa upande wangu hiyo ndiyo njia bora ninayoshughulikia hali hii. Siyo kuhusu mimi, ni jambo kubwa zaidi kuliko mimi. Vijana wote, kuna baadhi yetu waliomfahamu Latz, waliomfahamu Sina. Ni jambo zuri kuona kwa mtazamo wangu, ni jambo zuri sana kuona walikuwa bora na wanaostahili upendo.”

Joshua alipendekeza, hata hivyo, kwamba kujitoa kwake kwa ajili ya mchezo huo siyo lazima iwe kwamba kumeongezeka anapojaribu kupigana kwa heshima ya marafiki zake waliofariki dunia. “Siku zote nimekuwa nikijitolea. Hakika siku zote nimekuwa najitolea,” alisema bondia huyo mwenye umri wa miaka 36 na kuongeza:

“Sio kuhusu kuwa ‘zaidi’; ni tofauti, hakika ni tofauti. Lakini mimi niko hapo kwa ajili ya wazazi wao. Hilo kwangu mimi ndilo jambo la kwanza. Kuwa mtu mzuri kwa ajili yao. Lazima niwatunze wazazi wa wale vijana.”

Joshua pia alisema kwamba hakuwahi kufikiria kustaafu ndondi kutokana na ajali hiyo, akisema: “Hapana, kwa sababu huu ndio wito wangu. Ndondi siyo nzuri tu kwa upande wa ushindani; pia ni tiba kwa kiasi fulani. Ni kusudio. Sisi wapiganaji tuna kusudi. Hilo ndilo zinanifanyia mimi, na nadhani hapa ni mahali ambapo… najua ni mahali ambapo ninajisikia vizuri zaidi. Zinanipa kusudi (la kupigana) katika maisha yangu. Kwa hiyo ndiyo, nimeridhika kuwa hapa pamoja nanyi. Hapa ndipo ninapojisikia vizuri zaidi.

“Kwa kweli, takriban miezi miwili iliyopita (nilihisi niko tayari kupigana). Nilikuwa nafanya mazoezi, lakini kuna viwango vya mazoezi. Kwa hiyo, karibu miezi miwili iliyopita nilianza kuongeza kiwango kwa kiasi kikubwa. Imekuwa vizuri.”

Alipoulizwa kama kuwa “tayari” kulihusu hali yake ya kimwili au kiakili, Joshua alisema: “Kimwili. Kiakili (najisikia) imara sana, kiakili imara sana. Kimwili lazima ujirudishe katika kiwango cha kufanya sparring, kama nitakuwa mkweli. Bila shaka kutakuwa na usiku mgumu sana, lakini lazima nipitie usiku huu mgumu ili kukamilisha kazi.”

Tarehe ya pambano la Joshua dhidi ya Fury, mwenye miaka 37, bado haijajulikana, lakini linaweza kufanyika katika Uwanja wa Wembley mjini London mwezi Oktoba au Novemba, mwaka huu. Fury alipigana mara ya mwisho mwezi Aprili akimshinda Arslanbek Makhmudov kwa pointi katika Uwanja wa Tottenham Hotspur, ambapo Joshua alitazama pambano akiwa karibu na ulingo.